Watu wanapaswa kufahamu kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani ndani ya mwili kama vile mzio,matatizo ya ngozi au sumu ya mimea au wadudu ambao wanakawaida hiyo.
Mara nyingi muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu huisha wenyewe au muda mfupi baada ya kitu hicho kikiondolewa.Kuondolewa kwa kitu hicho kunakuwa ni matibabu sahihi na kuendelea na njia bora za kujikinga kutopata maambukizi tena.
Vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu.
Ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari.Kukaa na ugonjwa kwa muda mrefu kunaweza sababisha ugonjwa kusambaa mwilini na kuongeza hatari ya kifo.
KISABABISHI;
Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu zingine za mwili.Maradhi ya fangasi husababisha muwasho kwa wanaume wengi ,sababu zingine ni kama ugonjwa wa upele,kuwepo kwa chawa,mzio na maambukizi mengine ya bakteria.Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo cha kuwashwa uume.
FANGASI SEHEMU ZA SIRI;
Maradhi ya fangasi(Candidiasis)husababishwa na vimelea viitwavyo Candida albicans.Vimelea hivi hushambulia jinsia zote ingawa hushambulia zaidi jinsia ya kike kutokana na maumbile yao na hali ya kuwa na unyevunyevu mara nyingi.Mazingira hayo husababisha fangasi kumea vizuri.Watu wengi wana vimelea hivi katika miili yao kwa kiwango kidogo.Kinga ya mwili ikisaidiwa na bakteria walinzi wa mwili huweza kupambana na vimelea hivi.
Mtu anapokunywa dawa za kuua bakteria kutokana na ugonjwa mwingine wa bakteria kama kuhara damu,husababisha bakteria walinzi wa mwili kufa hivyo kuongeza hatari ya mwili kushambuliwa na ugonjwa wa fangasi.Ikiwa kinga ya mwili itashuka kutokana na maradhi kama VVU au lishe duni mwili utakuwa katika hatari zaidi ya kupata maradhi ya fangasi.
Hata hivyo maradhi ya fangasi yanaweza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kuchangia nguo au vifaa vya kuogea na kujamiiana na mwathirika.Wanaume wengi wanasumbukiwa na fangasi sehemu za siri huishi maeneo yenye joto sana kama pwani,lindi,Mtwara,Tanga na Dar es Salaam.
Kuishi sehemu yenye joto pamoja na kuvaa nguo za kubana hasa zisizotengenezwa na pamba kwa asilimia 100kunafanya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu hivyo kutengeneza mazingira mazuri kwa fangasi kuzaliana na kuongezeka.
DALILI ZA FANGASI SEHEMU ZA SIRI;
Sehemu za siri mara nyingi hutumiwa kama maficho ya fangasi.Hizi ni kama vile uume,korodani,katika mapaja,uke,na sehemu za katikati ya makalio.Wakati mwingine fangasi husambaa hadi kwenye mapaja.Kwa wanaume fangasi huweza kusababisha sehemu za siri za mwanaume kubadilika na kuwa nyekundu na hata kuwasha.
Ngozi inayozunguka sehemu hizo huwasha ,kukakamaa na kutoa majimaji ambayo hutoa harufu mbaya.
MATIBABU YA FANGASI;
Ikiwa una dalili za ugonjwa wa fangasi ni vyema kufika kwa daktari kwa ajili ya matibabu na ushauri zaidi.Kutumia dawa bila ushauri wa daktari kunaweza kusababisha kutopona kabisa ,kutopona vizuri au ugonjwa kujirudia baada ya siku chache.Vimelea pia vinaweza kujenga usugu wa dawa.
Kumwona daktari kutasaidia kujua kama una maradhi mengine yanayosababisha upate fangasi sehemu za siri.Ugonjwa wa fangasi usipotibiwa husambaa kwenye damu na kusababisha madhara makubwa mwilini kama kwenye ubongo na mapafu.
Katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunayo dawa iitwayo LMTM/PA19/NA ambayo ni ya kupaka yenye uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo fangasi sugu sehemu za siri.Baadhi ya magonjwa mengine yanayotibiwa na dawa hii ni pamoja na;saratani ya ngozi,vidonda vibichi,vidonda visivyopona kwa namna yeyote ile,bawasiri,majipu,vimbe mbalimbali,maumivu ya magoti kwa kuchua,nywele kukatika,mabaka na michirizi mwilini,kucha kung'ooka kwaajili ya fangasi kuota tena(ni nzuri sana kwa watu wenye ulemavu wa ngozi),mba....n.k
LMTM/PA19/NA |
JINSI YA KUJIKINGA;
Ili kusaidia kuepuka kupatwa na fangasi sehemu za siri ni vyema kuosha vizuri.Kwa wale wanaume ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani a govi.kwa kifupi ni vizuri sehemu za siri kubaki wakati wote katika hali ya usafi na ukavu,kwa maana ya kutokuwa na unyevunyevu unaweza kusababisha maambukizi.
Matumizi ya poda maalum yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali ili kuzuia unyevunyevu.Vaa nguo isiyobana ,iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba.Badili nguo ya ndani angalau kila siku na tumia kinga pale unapokutana kimwili na mtu ambaye hujui hali yake kiafya.
MAWASILIANO;
EMAIL;lmtmherbal@rocketmail.com
mobl;0798353434