Figo ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu,hufanya kazi ya kuchuja damu huku ikiondoa sumu zote mwilini lakini pia figo hufanya kazi ya kurekebisha kiasi cha maji mwilini[electrolyte level].
Kabla damu haijapita katika figo huwa inabeba maji na takataka nyingi sana[urea],lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu na masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwa nakiwango cha maji kilichozidi hupitishwa kwenye mirija miwili [ureters]kuelekea kwenye kibofu [urinary bladder] na kisha kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo[urethra].
Mkusanyiko wa kemikali hizi[chemical crystals]wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga,kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadi wengine hufikia hatua ya kuziba njia za mikojo katika figo yenyewe[nephrone]au kwenye mirija ya kupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu.Hapa ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kuskia maumivu makali.
SABABU ZA KUPATA MAWE KATIKA FIGO[KIDNEY STONES]
-Matumizi ya baadhi ya dawa(medicines),kuna baadhi ya dawa husababisha mtu kupata mawe katika figo pindi anapozitumia kila wakati dawa hizo ni kama vile za kutibu cCANCER na HIV.Antibiotic kama ciprofloxacin(cipro) na ,ceftriaxone(rocephin).
-Utumiaji kwa wingi wa vyakula vyenye kuongeza vitamin A na D,ambavyo huongeza kwa kiasi kikubwa madini joto(calcium) mwilini.
-Mazingira,ikiwa mtu anaishi kwenye mazingira ya joto sana halafu anapaa kiasi kidogo cha maji husababisha kiasi cha kemikali kuongezeka zaidi katika figo na hivyomwisho wa siku zinagandamana na kuletekeza mawe ndani ya figo.
-Viambukizi katika figo endapo mtu alipata yoyote viambukizi vya magonjwa ya figo kama vile (renal tubula acidosis e.t.c)huwa yupo katika hatari kubwa ya kupata tatizo hili.
-Kurithi,tatizo hili la mawe katika figo linaweza kuwa la kurithi ambapo mtu anarithi kutoka kwa wazazi wake ,yaani wanakuwa na homoni[antiduretic hormone]zisizoweza kufanya kazi ya kuchuja damu kikamilifu na mwishowe kutengeneza mawe kwenye figo.
-Utumiaji wa vyakula ,utumiaji wa vyakula vyenye protin zinazotokana na wanyama [animal protiens] na chumvi nyingi [salts] huongeza hatari ya kupata tatizo hili
-unene kupita kiasi[obesity]
DALILI ZA UWEPO WA MAWE KATIKA FIGO
Mtu mwenye tatizo la mawe kwenye figo huonyesha dalili zifuatazo;
1.Maumivu ya mgongo na kiuno
2.Mkojo kutoka ukiwa na rangi ya damu
3.Kutokwa na jasho wakati wa usiku hata kama kuna baridi
4.Kupatwa na homa kali kwa wakati fulani ikiambatana na kutetemeka mwili
5.Kuhisi kicheefuchefu na kutapika
6.Mkojo kuwa na harufu kali
7.Maumivu makali sehemu za mbavu
8.Miguu kujaa maji[kuvimba]
UCHUNGUZI WA TATIZO LA FIGO
-Mgonjwa hufanyiwa x-ray auscan ili kujua kama ana mawe katika figo
-vipimo vya damu[blood test]
-vipimo vya mkojo[urinarysis]
TIBA YA TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO
Ikiwa mgonjwa atagundlika kuwa na tatizo hili hufanyiwa yafuatayo;
a.Extracorporeal shock wave lithotripys(ESWL) hii ni mionzi huelekezwa katika figo ili kuyeyusha mawe (kemikali au sumu zilizogandamana) ambazo huvunjwavunjwa na hii mionzi kisha mgonjwa hukojoa vipandevipande.
b.Percutaneous Nephrolithotomy(PCNL),Hiki ni kifaa chenye mwanga na kamera ambacho huingizwa kwenye kokwa la figo (nephrone) kisha kuvunjaavunja hayo mawe.
c.Ureteroscopy,hiki ni kifaa kingine tena ambacho huingizwa kwenye mrija wa kupitisha mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu ,kuna baadhi ya mawe hukwama kwenye mirija hii na kuzuia mkojo kutoka ,hivyo kifaa hiki huvunja hayo mawe.
d.Stone Removal,hapa sasa mgonjwa anafanyiwa upasuaji (operation)ili kuweza kutoa mawe moja kwa moja.
NB;Kufanya tiba hizi zote ndani yake kuna madhara mengine huzalishwa ila sasa unaumwa inabidi ufanyiwe ,ila sasa kabla hujaendea tiba hatarishi kama hizo tunapenda kuwajulisha kuwa LMTM HERBAL CENTRE inazo dawa zenye uwezo wa kuyeyusha kemikali na mafuta yaliyogandamana katika figo na kuzibua mirija iliyoziba na kurudisha mtiririko wa mkojo kufanyika kama inavyotakiwa .Usisite kuwasiliana nasi kwa ushauri au tiba kupitia ;
mobl:+255776 217417/+255798 353434/+255717 150110 au
email:lmtmherbal@rocketmail.com
Tafuta katika Blogu Hii
Alhamisi, 4 Januari 2018
Jumatano, 3 Januari 2018
GARLIC IN MILK BENEFITS
DO U KNOW THAT THERE ARE SEVERAL DISEASES WHICH CAN BE CURED BY GARLIC AND MILK?? HERE IS SOME OF THEM:;
-ASTHMA
-PNEUMONIA
-TUBERCULOSIS
-CARDIACPROBLEMS
-INAOMNIA
-ARTHRITIS
-COUGH
-JAUNDICE
-CHOLESTEROL
-DIGESTIVE SYSTEM
-IMPOTENCE AND SCIATICA....
-HEART ISSUES
NB;IF YOU WILL NEED TO KNOW HOW TO PREPARE IT TO CURE ANY OF THOSE HEALTH PROBLEM CONTACT US THROUGH+255776217417 OR +255717150110/+255798353434
NB;IF YOU WILL NEED TO KNOW HOW TO PREPARE IT TO CURE ANY OF THOSE HEALTH PROBLEM CONTACT US THROUGH
Jumanne, 6 Septemba 2016
HUDUMA YA KWANZA YA JINSI YA KUOKOA MAISHA YA MTU ALIYEPATA STROKE
Mtu anapopatwa na stroke ni kwamba-vishipa vidogo viitwavyo kitaalam CAPILLARIES za ubongo kupasuka.Ubongo unakuwa haupati oxygen ya kutosha na kusababisha cells za ubomgo kufa au kukauka hivyo basi huhitaji msaada wa haraka wa kimatibabu .NJIA ZA KUPITIA ILI KUOKOA MAISHA YA ALIYEPATA STROKE;
1)Kwanza ni muhimu kutulia/kupanik wala usimsogeze mgonjwa aliyepatwa na stroke.Unachotakiwa kuwa nacho ni sindano na ni vyema kuwa na sindano ya hospitali ila kama huna waweza kutumia sindano ya kawaida.
2)Kama unatumia sindano ya kawaida ni muhimu uhakikishe inakuwa salama ,unaweza pia kusterilize kwa kutumia stove au moto wa mshumaa.
3)Chukua vidole vyote 10 vya mikono karibu na ukucha na toboa haraka iwezekanavyo.
4)Subiri damu ianze kutoka na kama damu haitokibana au minya ili kufanya damu itoke.
5)Damu ikianza kutoka katika vidole vyote mgonjwa ataanza kuzinduka
6)Kama mgonjwa amepinda mdomo upande mmoja chua masikio sehemu laini isiyo na mfupa ambayo hutobolewa na kuwekwa hereni mpaka ibadilike rangi na kuwa nyekundu ili kurahisisha damu kutembea(flow)
7)Choma au toboa sehemu hiyo laini(ear lobe)mara mbili hadi matone mawili ya damu yatoke
8)Baada ya dakika chache baadae mdomo utarudi katika hali yake ya kawaida.
9)Subiri kidogo hadi mgonjwa apate fahamu zake kamili kisha mchukuwe na kumpeleka hospitalini na daktari ataanzia hapo.
-Hii ni njia ya tiba ya asili iliyokuwa ikitumiwa na wachina karne nyingi zilizopita.Wanasema njia hiini salama asilimia100% na itakusaidia kunusuru maisha kutokana na stroke.
Ijumaa, 10 Juni 2016
YAJUE MAGONJWA YANAYOWEZA KUTIBIWA KWA KUTUMIA KITUNGUU MAJI

YAFUATAYO NI MAGONJWA YANAYOWEZA KUTIBIWA KWA KITUNGUU MAJI;
1)Kifaduro
2)Pumu
3)Uvimbe wa mapafu
4)Tezikibofu
5)Kukojoa kwa maumivu
6)Kutia nguvu na nishati
7)Nguvu za kiume
8)Maradhi ya kinafsi
9)Saratani
10)Baridi yabisi
11)Mvilio wa damu
12)Kuunga mivunjiko na kupunguza maumivu
13)Vidonda vya saratani
14)Majipu
15)Sugu/chunjua
16)Vidonda vilivyooza
17)Vidole kuvimba siku za kusi
18)Maumivu ya kichwa
19)Chunusi
20)Ukurutu
21)Saratani ya ngozi
22)Magonjwa ya figo na vijiwe
23)Jongo
24)Kikohozi kwa wakubwa na watoto
25)Kuisafisha damu na mwili kutokana na chumvi
26)Kisukari
27)Donda kuu
28)Mafindofindo
29)Maradhi ya masikio
30)Wengu
31)Kunyonyoka nywele
32)Chawa na mayai yake
33)Kipanda uso[maumivu ya nusu kichwa]
34)Kisunzi/kizunguzungu
35)Maradhi ya macho
36)Maji meupe jichoni
37)Kupunguza uzani
38)Mafua
39)Homo ya mafua
40)Kikohozi
41)Tumbo kushindwa kumengenya
42)Kuondoa gesi(tumboni)
43)Kufunga choo
44)Msokoto wa figo
45)Kuhara
46)Kutoa minyoo
47)Kutia nguvu na nishati
NB;UKITAKA KUFAHAMU NAMNA YA KUTIBUU MAGONJWA MBALIMBALI KWA KUTUMIA KITUNGUUMAJI WASILIANA NASI/TUANDIKIE KUPITIA;
Mobl:+255776 217417/+255789 353434
fax2email+255736 601119
email:lmtmherbal@rocketmail.com
Jumatano, 8 Juni 2016
JE WAJUA ASALI INAWEZA KUTIBU MAGONJWA MBALIMBALI??HAPA INAKULETEA MAGONJWA YANAYOWEZA KUTIBIWA KWA KUTUMIA ASALI;

MAGONJWA YANAYOTIBIWA KWA KUTUMIA ASALI
1.Kujikuna
2.Uzuri wa uso
3.Jeraha(Kidonda)
4.Kuungua
5.Kuua chawa na mayai yake
6.Kukosa usingizi
7.Maradhi ya kinafsi na wazimu
8.Kifafa
9.Magonjwa yote ya macho
10.Asidi/kiungulia
11.Kuhara/tumbo la kuendesha
12.Kufunga choo
13.Kutapika
14.Kidonda
15.Maradhi ya kifua
16.Kutibu harufu mbaya ya mdomo
17.Kupotewa na sauti
18.Homa ya mafua
19.Malengelenge kwenye ngozi
20.Maumivu ya fizi na kuyapa nguvu meno
21.Vena iliyovimba
22.KIdonda kilichooza
23.Kidonda kisichopona
24.Kifua kikuu cha mapafu
25.Kuupa nguvu msuli wa moyo
26.Kutibu uvimbe na tishu za msuli na kwenye moyo na kutetemeka
27.Moyo kubana
28.Uvimbe wa mdomoni na ulimi kufura
29.Maradhi ya masikio na maumivu yake
30.Baridi yabisi
31.Jongo
32.Sugu/chunjua
33.Magonjwa yote ya ini
34.Kutia nguvu,nishati na ujana
35.Maradhi ya wanawake na uzazi
36.Nguvu za kiume
37.Utasa/ugumba
38.Saratani
39.Ukoma
40.Kinga ya sumu
41.Tezi kibofu n.k
-Ukitaka kujua jinsi ya kutumia kulingana na maradhi yeyote kati ya hayo hapo juu wasiliana nasi kupitia;
mobl;+255776 217417/+255798 353434
email;lmtmherbal@rocketmail.com
Ijumaa, 15 Aprili 2016
FANGASI SUGU SEHEMU ZA SIRI NA NAMNA YA KUKABILIANA NAYO;
Watu wanapaswa kufahamu kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani ndani ya mwili kama vile mzio,matatizo ya ngozi au sumu ya mimea au wadudu ambao wanakawaida hiyo.
Mara nyingi muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu huisha wenyewe au muda mfupi baada ya kitu hicho kikiondolewa.Kuondolewa kwa kitu hicho kunakuwa ni matibabu sahihi na kuendelea na njia bora za kujikinga kutopata maambukizi tena.
Vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu.
Ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari.Kukaa na ugonjwa kwa muda mrefu kunaweza sababisha ugonjwa kusambaa mwilini na kuongeza hatari ya kifo.
KISABABISHI;
Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu zingine za mwili.Maradhi ya fangasi husababisha muwasho kwa wanaume wengi ,sababu zingine ni kama ugonjwa wa upele,kuwepo kwa chawa,mzio na maambukizi mengine ya bakteria.Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo cha kuwashwa uume.
FANGASI SEHEMU ZA SIRI;
Maradhi ya fangasi(Candidiasis)husababishwa na vimelea viitwavyo Candida albicans.Vimelea hivi hushambulia jinsia zote ingawa hushambulia zaidi jinsia ya kike kutokana na maumbile yao na hali ya kuwa na unyevunyevu mara nyingi.Mazingira hayo husababisha fangasi kumea vizuri.Watu wengi wana vimelea hivi katika miili yao kwa kiwango kidogo.Kinga ya mwili ikisaidiwa na bakteria walinzi wa mwili huweza kupambana na vimelea hivi.
Mtu anapokunywa dawa za kuua bakteria kutokana na ugonjwa mwingine wa bakteria kama kuhara damu,husababisha bakteria walinzi wa mwili kufa hivyo kuongeza hatari ya mwili kushambuliwa na ugonjwa wa fangasi.Ikiwa kinga ya mwili itashuka kutokana na maradhi kama VVU au lishe duni mwili utakuwa katika hatari zaidi ya kupata maradhi ya fangasi.
Hata hivyo maradhi ya fangasi yanaweza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kuchangia nguo au vifaa vya kuogea na kujamiiana na mwathirika.Wanaume wengi wanasumbukiwa na fangasi sehemu za siri huishi maeneo yenye joto sana kama pwani,lindi,Mtwara,Tanga na Dar es Salaam.
Kuishi sehemu yenye joto pamoja na kuvaa nguo za kubana hasa zisizotengenezwa na pamba kwa asilimia 100kunafanya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu hivyo kutengeneza mazingira mazuri kwa fangasi kuzaliana na kuongezeka.
DALILI ZA FANGASI SEHEMU ZA SIRI;
Sehemu za siri mara nyingi hutumiwa kama maficho ya fangasi.Hizi ni kama vile uume,korodani,katika mapaja,uke,na sehemu za katikati ya makalio.Wakati mwingine fangasi husambaa hadi kwenye mapaja.Kwa wanaume fangasi huweza kusababisha sehemu za siri za mwanaume kubadilika na kuwa nyekundu na hata kuwasha.
Ngozi inayozunguka sehemu hizo huwasha ,kukakamaa na kutoa majimaji ambayo hutoa harufu mbaya.
MATIBABU YA FANGASI;
Ikiwa una dalili za ugonjwa wa fangasi ni vyema kufika kwa daktari kwa ajili ya matibabu na ushauri zaidi.Kutumia dawa bila ushauri wa daktari kunaweza kusababisha kutopona kabisa ,kutopona vizuri au ugonjwa kujirudia baada ya siku chache.Vimelea pia vinaweza kujenga usugu wa dawa.
Kumwona daktari kutasaidia kujua kama una maradhi mengine yanayosababisha upate fangasi sehemu za siri.Ugonjwa wa fangasi usipotibiwa husambaa kwenye damu na kusababisha madhara makubwa mwilini kama kwenye ubongo na mapafu.
Katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunayo dawa iitwayo LMTM/PA19/NA ambayo ni ya kupaka yenye uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo fangasi sugu sehemu za siri.Baadhi ya magonjwa mengine yanayotibiwa na dawa hii ni pamoja na;saratani ya ngozi,vidonda vibichi,vidonda visivyopona kwa namna yeyote ile,bawasiri,majipu,vimbe mbalimbali,maumivu ya magoti kwa kuchua,nywele kukatika,mabaka na michirizi mwilini,kucha kung'ooka kwaajili ya fangasi kuota tena(ni nzuri sana kwa watu wenye ulemavu wa ngozi),mba....n.k
![]() |
| LMTM/PA19/NA |
JINSI YA KUJIKINGA;
Ili kusaidia kuepuka kupatwa na fangasi sehemu za siri ni vyema kuosha vizuri.Kwa wale wanaume ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani a govi.kwa kifupi ni vizuri sehemu za siri kubaki wakati wote katika hali ya usafi na ukavu,kwa maana ya kutokuwa na unyevunyevu unaweza kusababisha maambukizi.
Matumizi ya poda maalum yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali ili kuzuia unyevunyevu.Vaa nguo isiyobana ,iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba.Badili nguo ya ndani angalau kila siku na tumia kinga pale unapokutana kimwili na mtu ambaye hujui hali yake kiafya.
MAWASILIANO;
EMAIL;lmtmherbal@rocketmail.com
mobl;0798353434
TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA JINSI YA KUKABILIANA NALO
Wengi hujikuta wakitapeliwa na waganga feki ambao wamejaa mjini na vijijini.Katika mitaa utaona mabango mengi ya waganga wa kienyeji wasio na sifa wala usajili wakijitangaza kuwa na dawa za kuongeza nguvu za kiume.
Mara nyingi dawa hizo siyo za kutatua tatizo bali ni kutafuta nguvu za muda.Kukurupuka na kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume kiholela ni hatari kwani nyingi ndio chanzo cha kuumiza mwili na kuathiri viungo kama figo.
Tendo la uume kuwa na nguvu na kuweza kusimama kina mtiririko wa matukio mengi ya kimwili na huwa ni hatua moja kwenda nyingine.Kitendo cha kusimama kinahusisha mfumo wa fahamu kama ubongo,uti wa mgongo na mishipa ya fahamu,mfumo wa damu ambao ni moyo,damu na mishipa na mfumo wa tezi zinazomwaga vichocheo kama homoni.
Zipo kemikali nyingi za kibaiolojia za mwilini zikiwamo protini,virutubisho na vitamini mbalimbali tunavyopata katika lishe ,husaidia pia katika tendo hili.
Kwa kawaida sehemu za uzazi wa kiume huwa na misuli laini kama sponji ambayo huwa na mishipa midogo mingi ambayo imejikunja kunja kama mizizi ya mmea.
Wakati wa kusimama damu iliyosafi humiminika kupitia mishipa ya ateri ambayo hutanuka kuruhusu damu ya kutosha kupita kwenda katika misuli laini kama sponji ambayo huwa imetulia kuruhusu damu kuingia katika mishipa hiyo.Wakati huohuo ile mishipa inayotoa damu chafu kurudi kusafishwa yaani vein ,huwa zimebanwa ili damu hiyo isitoke katika misuli laini ya uume.
Mchepuko wa kupata hisia za kujamiiana ni kituo kilichopo ndani ya uti wa mgongo ,ni matokeo ya eneo la uzazi sehemu ya kiume kusisimuliwa.
Baadhi ya mambo yanayosababisha mtu kukosa nguvu za kiume ni magonjwa kama vile;
-Kisukari
-Maradhi ya mishipa ya damu
-Shinikizo la damu
-Uwapo wa maradhi ya kisukari kisichodhibitiwa kwa muda mrefu huweza kusababisha mishipa inayopeleka damu katika uume kuharibika.Sukari iliyo juu huiharibu mishipa hii ya damu na kuifanya iwe migumu.
-Shinikizo la damu likiwa kali mara kwa mara huweza kuleta uharibifu katika mishipa ya damu ambayo ni midogo iliyotanda kwa wingi katika uume.
Mambo mengine ni;
-Utumiaji wa tumbaku,
-Uvutaji sigara,
-Ulevi uliopindukia,
-Utumiaji wa madawa ya kulevya.
Vitu hivyo pia huweza kuharibu mishipa ya damu katika uume.
Mambo mengine ni magonjwa ya tezi ya koo inayotoa homoni za ukuaji mwili na kutengeneza kidogo kwa homoni muhimu ya kiume ambayo ni Testosterone.
Maradhi mengine ni ugonjwa wa kutetemeka ,unene na uzito kupita kiasi,ugonjwa wa akili na matibabu ya muda mrefu ya saratani ya tezi dume.
Tatizo la nguvu za kiume linaweza kutibiwa kwa matibabu mbalimbali baada ya kufanyiwa uchunguzi yakinifu.
Baada ya uchunguzi daktari anaweza kukupatia dawa au kukupa maagizo kama vile kufanya mazoezi ,kula vyakula fulanina kubadili mitindo kadhaa ya kimaisha.Kama tatizo litakuwa linasababishwa na magonjwa mengine dqaktari anaweza akaanza kutibu magonjwa hayo na afya yako kurejea upya vizuri.
Hatahivyo kwa wale ambao hawana matatizo mengine yoyote ila nguvu zao zimepungua LMTM HERBAL CENTRE tunazo dawa aina mbalimbali za mimea zenye uwezo wa kutatua nguvu za kiume kwa kiwango cha juu.
Moja ya madawa hayo ni LMTM/fg/olv.
KWA MAWASILIANO ZAIDI;
lmtmherbal@rocketmail.com
mobl:0798353434
Ijumaa, 29 Mei 2015
URINARY TRACT INFECTION(UTI) KWA WANAUME NA WANAWAKE
Leo tuangalie tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo(UTI)kwa wanawake na wanaume.Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalam huitwa SIMPLE CYSTITIS au BLADDER INFECTION na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa PYLONEPHRITIS au KIDNEY INFECTION.
Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa ESCHERICHIA COLI.Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa.Lakini watu wengi wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi japokuwa kuna visababishi vingine vichache.Bakteria wa Escherichia Coli hawapo peke yao huambatana na waitwao STAPHYLOCOCCUS,SAPROPHYTI CUS,PSEUDOM ONAS,ENTEROBACTER n.k
Maambukizi katika njia ya mkojo lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo na si pengine popote.Wapo wanawake wamekuwa wakiniulizia kuhusu tatizo la kutokwa na uchafu ukeni na kudhani ni ugonjwa huu,huo ni ugonjwa tofauti kabisa na tunaouchambua leo.
Tunapozungumzia maambukizi katika njia ya mkojo,tuna maana ni kutoka eneo la nje ya utupu hadi kwenye kibofu na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo kitaalam huitwa LOWER URINARY TRACT INFECTION na ikihusisha eneo la juu ya kibofu jina hubadilika na kuitwa UPPER URINARY TRACT INFECTION.Mara nyingi maambukizi haya kwa wanawake hutokea wakati wa kujisafisha,kutonawa vizuri sehemu za siri na kuvaa nguo za ndani chafu.Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambazo huua bacteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bacteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi. Upungufu wa homoni ya kike iitwayo OESTROGEN husababisha bakteria wasababishao maambukizi katika njia ya mkojo kuzaliana kirahisi.Matatizo haya ya maambukizi licha ya kuwapata zaidi wanawake huwakumba pia watoto wadogo kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vyao vya uzazi,njia ya mkojo na haja kubwa vipo jirani.
Watoto wa kiume ambao hawajatahiriwa nao hupata maambukizi rahisi kutokana na viungo vyao vya uzazi kuwa vifupi na wanaponawa maji yasiyo salama kwa watoto wa kiume huwa rahisi bakteria kubaki katika ngozi inayoning'inia(govi),hivyo kusababisha tatizo hili.Lakini pia wanaume watu wazima ambao hawajatahiriwa wanaweza kupata maambukizi kutokana na sababu ambazo tumezitaja hapo juu ambapo pia ni rahisi kwao kuambukizwa ukimwi kama watafanya ngono zembe na ndiyo maana tunasisitiza tohara kwa wanaume.
Maambukizi yanayoshambulia mfumo wa mkojo zaidi ni bakteria wanaoishi katika mfumo wa haja kubwa kusafiri kwa bahati mbaya na kujikita katika mfumo wa mkojo.Bakteria wengine waambukizao njia ya mkojo ni wale watokanao na magonjwa ya zinaa kama kisonono,klamidia na fangasi wanapojamiiana bila kinga.
-Ili kuepuka kupata maambukizi katika njia ya mkojo mara kwa mara ni vema kutumia kinga yaani kondom na kwa mwanamke kila anapomaliza kufanya ngono akojoe ili kuondoa bakteria walioingia au kukaa katika tundu ya mkojo wakisubiri kuingia.Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu,unywaji wa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na kutokunywa maji ya kutosha huchangia tatizo hili.Uwepo wa mawe katika figo na mirija ya figo hata ndani ya kibofu pia ni mojawapo ya chanzo cha maambukizi haya katika njia ya mkojo.
DALILI;
Baadhi ya dalili za mtu kuambukizwa bakteria katika njia ya mkojo kubwa ni maumivu wakati wa kukojoa,mkojo kuwa na rangi ya njano kupindukia na kuwa na harufu kali japokuwa siyo kila mwenye dalili hizo ana maambukizi katika njia ya mkojo au wengine huita URINARY TRACT INFECTION(UTI) wana ugonjwa huu.
-Dalili nyingine za maambukizi ni maumivu,kutokwa na usaha au majimaji wakati wa kukojoa kabla au baada ya kukojoa kukiambatana na maumivu na kuhisi moto wakati wa kukojoa mkojo.Baadhi ya wanaume wakati mwingine hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo wakati wa kujisaidia haja kubwa.Wengine wenye maambukizi hujikuta wakipata vichomi katika njia ya mkojo au kuhisi kuwashwa sehemu hiyo,kuumwa kiuno au tumbo na kadhalika.Mgonjwa anaweza pia kukumbwa na homa kali mara kwa mara na mwili kuwa mchovu,kwa watoto hupoteza hamu ya kula na mwili kuonyesha kuchoka.
-Wagonjwa wengine hupata maumivu kwenye kibofu cha mkojo ambapo husikia maumivu ya chini ya tumbo usawa wa kitovu na huwa hayaishi,matatizo haya ya mfumo wa mkojo kama tulivyoona huko juu huwapata watu wote wanawake na wanaume.Watu wenye matatizo haya kila wakipima huambiwa wana UTI,kwa wanaume huhisi hata nguvu za kiume hupungua na wanawake hupoteza hamu ya tendo la ndoa.
WAJAWAZITO;
-Kwa wajawazito ugonjwa huu unaweza kuhatarisha maisha yao na mtoto aliye tumboni,bakteria wanaweza kuingilia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhara mengine kama vile shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi wa kazi mbovu wa figo.
TIBA;
-Maambukizi katika njia ya mkojo hutibika kwa dawa mbalimbali za kisasa na mbadala baada ya kufanyiwa vipimo na kuwa mgonjwa ana maambukizi hayo.Dawa ambazo anaweza kupewa ni kama vile Ciprofloxacin,Fosfomycin,Monurol,Furadantin,Sulfam ethoxazole,Co-trimax,Ampicillin,Gentamicin n.k lakini usitumie dawa yoyote bila kwanza kupata ushauri wa daktari.
-Katika kituo chetu tunayo dawa iitwayo LMTM-N7/SUZ,LMTM-S32/J na LMTM-RUN/4.5.1 ambazo zinauwezo mkubwa wa kutibu kwa wakati mmoja magonjwa yote ya zinaa(STD)
USHAURI;
-Tunashauri kwa wanawake waepuke kujisafisha sehemu za siri kwa maji yarukayo kwa kasi,pia waepuke kupaka marashi sehemu hizo,au kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu kwani hizo huua bakteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bakteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi.
-Ujisafishapo baada ya kujisaidia unatakiwa uanzie mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bakteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo.Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi wanaweza kushauriana na daktari jinsi ya kutumia oestrogen ya ukeni ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi.Kwa wanaume maambukizi haya huathiri nguvu za kiume na kuenea hadi katika korodani na kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na kukufanya uwe mgumba.
-Maambukizi ya njia ya mkojo huweza kusababisha matatizo ya tezi ya kiume(prostate) kwani husababisha mrija wa mkojo kuziba ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bakteria kujenga makazi.Hali hiyo ikitokea mgonjwa lazma akamuone daktari ili aweze kuwekewa mrija wa kutolea mkojo.
KWA MASWALI,USHAURI NA TIBA;
MOBL;+255776 217417
fax2email+255 736 601119
email:lmtmherbal@rocketmail.com
Jumatano, 15 Aprili 2015
ZIJUE TIBA ZA MIMEA INAYOTUZUNGUKA
ALOVERA(LITEMBWE)
Alovera ni mmea wenye uwezo wa kutibu magonjwa mengi kama vile;
1.Malaria
2.Kisukari
3.Saratani
4.Mkanda wa jeshi
5.Vidonda tumbo
6.Baridi yabisi
7.Maumivu ya viungo
8.Homa ya matumbo
9.Mwili kuvimba
10.L/B/P
11.Madhara ya ukiumwa na wadudu
12.Bawasiri
13.Kuinua CD 4
14.Nguvu za kiume
15.Kuchelewa hedhi
16.Kurefusha maisha kwa wale wenye VVU
17.Hamu ya kula
18.Husaidia kuyeyusha chakula
19.Mkojo utokao kwa shida
20.Pumu
21.Ini
22.Figo
23.Ngozi na masikio kutoa usaha
Matayarisho ;Hutegemea aina ya ugonjwa unaotaka kuutibu
TANGAWIZI;
Tangawizi ijapokuwa ni kiungo katika vyakula pia ni dawa yenye uwezo wa kutibu maradhi mbalimbali yanayomsibu binadamu.Baadhi ya maradhi hayo ni;
1.Tumbo-hutuliza maumivu ya tumbo yanayotokana na matatizo ya usagaji wa chakula
-kuharisha,kuvimbiwa.(Inapotumiwa katika chakula husaidia usagaji wa chakula na inaleta hamu ya kula)
2.Kichefuchefu na kutapika-Huondoa kichefuchefu
3.Matatizo ya moyo-Huimarisha moyo na kumuepusha mtu maradhi ya moyo
4.Matatizo ya kupumua-Inapunguza kiwango cha mafuta mwilini
-Huondoa homa ya mafua
-Hutibu pumu
5.Maumivu-Maumivu ya misuli
-Maumivu ya kichwa,shinikizo la damu,mawazo,kizunguzungu na kukosa umakini
6.Maumivu wakati wa hedhi
7.Husaidia kutibu malaria na homa ya manjano
8.Nguvu za kiume na kuboresha manii
9.Vijiwe katika figo
10.Hufaa kutunzia nywele kwani huondoa uyabisi
11.Husaidia katika tiba ya saratani na kuzuia saratani
12.Husaidia kwa wenye kufunga hedhi na kusaidia kutoka
NAZI;
Nazi ina Vitamin A,B na E
Baadhi ya faida za nazi ni;
a.Huimarisha utumbo
b.Upungufu wa damu
c.Husaidia mapafu
d.Huondoa uchovu wa mishipa pamoja na magonjwa ya mishipa
e.Kuondoa uchovu mwilini
f.Huondoa usahaulifu
g.Huimarisha viungo
h.Homa
MATUMIZI;Jinsi ya kutumia wasiliana na LMTM HERBAL CENTER
MOBL;+255776 217417
fax2email+255736601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com
JE WAJUA KABICHI NI DAWA?

Kabichi ni zao linalolimwa mahala pengi sana hapa duniani.Mara nyingi mboga hii imekuwa ikichukuliwa kama ni aina fulani inayotakiwa kuliwa na watu wa chini au kutumika katika kachumbari tu.Huwa inatumika zaidi sehemu za jumuiya kama vile shule,magerezani na vyuoni kwani gharama yake ni ndogo hivyo mnunuzi anaweza kuhimili kuinunua kwa matumizi ya watu wengi.Mboga hii ina manufaa mengi sana mwilini lakini iwe ya rangi ya kijani,nyekundu au hata zambarau na sio ile iliyokaa sana sokoni hadi kusinyaa,hiyo haina manufaa kabisa kwa mwili wa binadamu.
FAIDA ZA KABICHI;
1.Huzuia saratani-Ulaji wa kabichi huzuia saratani ya matiti,utumbo mpana na saratani ya korodani(testes)kwa wanaume.Kwani ina madini yanayosaidia kupigana na visababishi vya saratani.Pia huzuia uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.
Mboga hii huondoa lehemu (cholesterol)katika damu,kwani huleta shinikizo kubwa la damu pale yanapojaa,pia huweza kusababisha kiharusi na moyo kupasuka.Hivyo kabichi husaidia kuondoa.
2.Kuondoa sumu mwilini-Kabichi ina Vitamin C kwa wingi kuliko hata machungwa,pia ina kampaundi za sifa,vitu hivi huisaidia sana kusafisha damu na kuondoa sumu mwilini.Pia huimarisha ini hivyo kulifanya lifanye kazi vizuri.
3.Ina Vitamin kwa wingi-Kabichi ina Vitamin A,B,C,E na K kwa wingi ambazo zina faida kubwa sana mwilini kama;
a.Vitamin A huisaidia kuimarisha ngozi na uwezo wa kuona.
b.Vitamin B huimarisha uwezo wa kutafakari na kuboresha utendaji wa kazi wa ubongo na kuzuia msongo wa mawazo.
c.Vitamin C huimarisha kinga ya mwili na kuzuia visababishi vya saratani
d.Vitamin E hufanya ngozi ya mwili kuwa nyororo
e.Vitamin K huimarisha mifupa na uhusika na ugandaji wa damu pale unapoumia.
Manufaa mengine ni kama vile kulinda mwili na maambukizi ya magonjwa mbalimbali,pia hutibu vidonda vya tumbo,kwani utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha tiba cha Stanford,iligundulika kuwa wagonjwa 13 walipona vidonda vya tumbo kwa kunywa juisi ya kabichi.Pia hupunguza tatizo la kufunga choo kwani ina kambakamba zinazosaidia kulainisha choo na vilevile ina madini ya salfa na chuma yanayosaidia kusafisha utumbo.
JINSI YA KUANDAA KABICHI;
Kabichi inapendekezwa sana kuliwa ikiwa mbichi kwa kuongezwa ndimu na chumvi ili kuleta ladha nzuri kama vile kachumbari,vilevile unaweza tu ukaichemsha supu yake lakini isiive sana kiasi cha kuua virutubisho vyake,inapendekezwakuchemka kwa dakika 4-5 tu.
ANGALIZO;Ulaji wa kabichi uliopitiliza huweza kusababisha ugonjwa wa Rovu(goiter)kwa hiyo watu wenye tatizo la rovu wasile kabichi kwa wingi.
KWA MAWASILIANO NA MAELEKEZO ZAIDI YA JINSI YA KUTUMIA KULINGANA NA TATIZO UTAKALOKUWA NALO WASILIANA NA OFISI ZETU KUPITIA;
MOBL;+255776217417,
fax2email+255736601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com
Jumatatu, 12 Januari 2015
PROSTATITIS(TATIZO LA KIBOFU CHA MKOJO)
Jinsi umri wa mwanaume unavyosonga mbele PROSTATE huongezeka ukubwa(kuvimba).Hali hii husababishwa aidha na upungufu wa LYCOPENE(ambayo hupatikana kwa wingi kwenye nyanya)au maambukizi (infection)au sababu nyinginezo kama maambukizi ya vijidudu (FUNGI).Kuvimba kwa prostate husababisha kugandamiza kwa kibofu cha mkojo kiasi kwamba mkojo kidogo ukiwa ndani ya kibofu mtu hudhani kibofu kimejaa kumbe sio.
DALILI ZA MTU MWENYE PROSTATE NI;
1.Kubanwa na mkojo mara kwa mara
2.Kwenda haja ndogo mara kwa mara usiku
3.Damu kwenye mkojo au kwenye mbegu za kiume
4.Maumivu wakati wa kukojoa
5.Maumivu baada ya kukojoa au wakati mtu anamaliza kukojoa
6.Kushindwa kukojoa
7Maumivu wakati mbegu za kiume zinatoka
8.Maumivu kwenye hipsi,mgongo,nyonga au mapajani
9.Matone ya mkojo kutoka yenyewe au kushindwa kujizuia na kukuta mkojo umetoka
-Mtu mwenye tatizo hili anaweza kujihisi kama amepungukiwa nguvu za kiume(sprerm count)kitu ambacho kwa kiasi kikubwa sio kweli.Hali hii husababishwa na ile hali ya yale majimaji yanayosafirisha mbegu za kiume kutokuwepo kwa kuishia njiani.Hali ikizidi kuwa mbaya huweza kusababisha muathirika kufanyiwa upasuaji kwaajili ya kuondoa prostate hiyo au kusababisha mtu kupata saratani(PROSTATE CANCER)
USHAURI;Wanaume wanashauriwa kuwa na mazoea ya kula nyanya kwa wingi(iliwe bila kupikwa au kuongezewa kitu chochote kama chumvi),papai,zabibu na mapera kama kinga.ukiweza kula nyanya kwa wingi kila siku itakuwa ni vizuri zaidi.
Hata hivyo habari nzuri ni kuwa katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunazo dawa ya LMTM-RUN/4.5.1 na LMTM/S32/J zenye uwezo mkubwa wa kutibu tatizo hili likiwa bado katika hatua za awali.
KWA MASWALI,USHAURI NA TIBA;
MOBL;+255798353434
fax2email+255736601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com
Jumapili, 7 Desemba 2014
UFAHAMU UGONJWA WA ZINAA WA CHLAMIDIA,DALILI ZAKE ,MADHARA,TIBA NA KINGA
Inawezekana jina la ugonjwa huo halijazoeleka katika masikio ya wengi na hii huenda ni kutokana na kutokuwepo kwa takwimu za kutosha kuhusiana na suala hilo katika nchi nyingi barani Afrika na hasa katika nchi zetu za Afrika Mashariki,hivyo ni vigumu kujua idadi kamili ya maambukizi.Lakini bila shaka chlamidia ndio ugonjwa wa zinaa unaotokana na bakteria unaoongoza kwa maambukizi mengi zaidi duniani ukifuatiwa na ugonjwa wa gono.Gonjwa hili ambalo huwaathiri wanawake na wanaume pia linaweza kuleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Nchini Marekani pekee mwaka 2011 kesi milioni 1 na nusu ziliripotiwa katika hospitali katika majimbo 50 ya nchi hiyo,katika hali ambayo kesi nyingi hazikuripotiwa kwa kuwa watu wengi wenye kuambukiza ugonjwa huo huwa hawaonyeshi dalili na hivyo hawakwenda hospitali.Kama yalivyo magonjwa mengi ya zinaa,chlamidia pia huwapata zaidi vijana na takwimu zinaonyesha kuwa kati ya wasichana walio na umri wa miaka 14-15 wenye kufanya ngono zembe mara kwa mara,mmoja wao huambukizwa chlamidia.
Ugonjwa wa chlamidia huweza kuambukizwa kupitia njia za kujamiiana .Mtu yoyote mwenye kufanya ngono zembe na mtu aliye na ugonjwa huo anaweza kuambukizwa.Pia mama mjamzito huweza kuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.Vilevile ugonjwa huo wa zinaa unaweza kuambukizwa kupitia mbwa,vinyesi vya wanyama kama vile ndege walioambukizwa aina ya chlamidia inayopatikana kwa wanyama kwa mfano kuku,bata,kasuku na kadhalika na kusababisha aina ya homa ya mapafu inayojulikana kama PSITTACOSIS ambayo huambatana na homa kali yenye nyuzi joto kati ya celsius 39.4 hadi 41.1.Chlamidia huathiri sehemu tofauti za mwili wa binadamu kama macho,mfumo mzima wa kupumua,sehemu za siri,viungo vya uzazi na tezi(lymph nodes)
DALILI NA VIASHIRIA VYA UGONJWA WA CHLAMIDIA
-Asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume wanaopata maambukizi ya ugonjwa huu huwa hawaonywshi dalili zozote za ugonjwa huo ila dalili hutokea baada ya wiki 1-3 baada ya mtu kupata maambukizi.
DALILI KWA WANAWAKE;
1)Kutokwa na majimaji ya rangi ya njano yanayotoka kwenye utupu,ambayo huwa na harufu kali
2)Kuhisi maumivu wakati wa haja ndogo
3)Kuhisi kama kuwaka moto wakati wa kukojoa
4)Kutokwa na damu katikati ya kipindi cha hedhi yaani baada ya kumaliza mzunguko wa hedhi na kabla ya kuanza mzunguko mwengine
5)Kuhisi maumivu sehemu ya chini ya tumbo
6)Kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana
7)Kutokwa na damu wakati wa kujamiiana na pia kuvimba na kuhisi maumivu kwenye tezi zilizopo sehemu za siri
DALILI KWA WANAUME;
1.Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
2.Kuhisi kama kuwaka moto wakati wa kukojoa,
3.Kutokwa na njimajikwenye uume ambayo yanaweza kuwa ya ragi nyeupe kama maziwa,kijivu au rangi ya njano.
4.Sehemu ya tundu kwenye uume kuwa nyekundu,kuvimba na kuwasha.
5.Kuhisi maumivu kwenye korodan na tezi zilizopo sehemu za siri ambazo huvimba na huambatana na maumivu.Mara nyingi dalili hizi kwa wanaume huja na kupotea au zinaweza kuonekana tu wakati anapoenda kukojoa asubuhi baada ya kuamka kutoka usingizini.
-Dalili za ugonjwa huu kama umeathiri puru(rectum) kwa wanawake na wanaume ni kama ifuatavyo;
a)Kuwashwa na kutokwa na damu kwenye puru
b)Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
c)Kutokwa na uchafu kama kamasi kwenye puru(rectum)
Iwapo vimelea vya chlamidia vitaathiri macho,wanawake na wanaume huwa na dalili zifuatazo;
-Uvimbe kwenye macho
-Macho kuwa mekundu
-macho kuwasha na hata kutokwa na majimaji machoni.
Baada ya mtu kuhisi dalili hizo tulizozitaja ,hupaswa kwenda hospitalini au katika kituo cha afya ili kupimwa na kuthibitishwa kwamba ana ugonjwa huo ili apatiwe matibabu.
Vipimo vya uchunguzi vya ugonjwa wa chlamidia ni Urethral swab for culture.Katika kipimo hiki majimaji kutoka kwenye uume au uke huchukuliwa kwa kutumia kijiti chenye pamba au swab maalum ambayo hupelekwa maabara ili kuoteshwa na kuangalia aina ya uoto wa bakteria.Pia huchukuliwa vipimo vya mkojo na pia kipimo cha PCR au Polymerase Chain Reaction,ambacho ni cha kuangalia vinasaba vya bakteria au DNA na hufanywa katika maabara.Baada ya majibu kuonyesha kuwa mgonjwa ameambukizwa vimelea vya ugonjwa huo matibabu hufuata.Chlamidia ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayotibika na ugonjwa huu hutibiwa kwa dawa aina ya antibiotiki zilizopo kwenye makundi ya macrolides,Quinolones na Polyketides ambazo hutolewa chini ya maelekezo ya daktari.
MADHARA YA UGONJWA WA CHLAMIDIA;
Kwa wanaume;
-Huathiri korodani na kusababisha mwanaume kukosa uwezo wa kuwa na watoto au kuwa tasa na pia husababisha maambukizi kwenye tezi dume(prostates).
Kwa wanawake;
-Husababisha maambukizi kwenye mirija ya uzazi,mfuko wa uzazi na mayai ya uzazi,kwahivyo kusababisha ugonjwa wa uvimbe katika fupanyonga au Pelvic inflammatory disease(PID).Pia huongeza uwezekano wa wanawake kupata mimba zilizotunga nje ya mfuko wa uzazi ambazo kitaalam huitwa Ectopic pregnancy.Mbali na hilo,mwanamke hupata maumivu sugu kwenye nyonga na ugonjwa wa mifupa arthritis aina ya Reiters syndrome.
-Vilevile chlamidia huweza kusababisha ugumba kwa mwanamke kama hatapata tiba.Si hayo tu,kwa wanawake wajawazito chlamidia husababisha wajifungue kabla ya wakati wake.Pia mtoto anaweza kuzaliwa na maambukizi kwenye masikio,sehemu za siri,macho,mapafu (homa ya mapafu),na kama mtoto hatopatiwa tiba ya haraka ya macho baada ya kuzaliwa basi anaweza kuwa kipofu.
-Dalili za chlamidia kwa watoto wachanga hutokea katika kipindi cha wiki 2 kwenye macho,na iwapo ni homa ya mapafu dalili zake hujitokeza katika kipindi cha wiki 2-miezi 3 baada ya kuzaliwa.
NJIA ZA KUJIKINGA NA UGONJWA WA CHLAMIDIA;
-Kwa wanawake wajawazito,ni vizuri kuhudhuria klinik mapema wakati wa ujauzito na kupima vipimo mbalimbali ambapo kimojawapo ni cha kuangalia iwapo mama mjamzito ameathirika na ugonjwa huu ili aweze kupatiwa matibabu mapema
-Kwa wenye maambukizi wanashauriwa kuchukua tahadhari ya kutowaambukiza wapenzi wao kwa kufanya ngono salama,pia kuepuka kushika macho kwa kutumia mikono na hata ikiwezekana kuwaepuka wapenzi wao ili kuwalinda na maambukizi.
-kwa wale ambao wapenzi wao wameambukizwa au wameonyesha dalili za ugonjwa huu,wanashauriwa na wao pia kupata tiba hata kama hawana dalili zozote pia kondom zihusike kwa kila tendo la ndoa.
NB;Njia kuu na sahihi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa ni kuacha au kuepuka kujamiiana au kufanya ngono zembe na zisizo salama.
MOBL;+255776 217 417
fax2email+255 736 601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com
Ijumaa, 3 Oktoba 2014
JE WAJUA KUWA VYOMBO VYA PLASTIKI NI MOJAWAPO YA VYANZO VYA SARATANI ?SOMA HAPA
- Ili kupunguza uwezekano huo unashauriwa
(1)Usinywe chai kwa kutumia vikombe vya plastiki
(2)Usile chochote chenye moto kilichofungwa ndani ya mfuko wa plastiki kama chips nk.
(3)Usipashe chakula ndani ya microwave kwa kutumia chombo cha plastiki
(4)Epuka kuchoma mabaki ya plastiki sehemu wanakoishi watu kwani ukivuta moshi huo ni hatari na pia inaweza kusababisha saratani ya mapafu nk
NB; TAFADHALI CHUKUA TAHADHARI
SHARE KWA KUWAJULISHA WENGINE
USISAHAU KULIKE PAGE YETU
Jumamosi, 20 Septemba 2014
UFAHAMU UGONJWA WA ZINAA WA TRICHOMONIASIS AMBAO HUWAATHIRI SANA WANAWAKE

Ugonjwa wa Trichomoniasis ni mojawapo ya ugonjwa ulio katika kundi la magonjwa ya zinaa zaidi ya 25 yanayofahamika kwa watu wengi.Ugonjwa huu huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume.Ugonjwa huu wa Trichomoniasis unasababishwa na vimelea vya jamii ya protozoa vinavyojulikana kama Trichomonas Vaginalis ambao huathiri mrija wa kupitishia mkojo(urethra)na tupu ya mwanamke.Trichomoniasis pia hujulikana kwa majina mengine kama Trichomonas Vaginitis au Trich.
Ugonjwa huu huathiri watu milioni 170 kwa mwaka duniani kote .Nchini Marekani pekee ambayo imeendelea katika fani ya tiba watu milioni 8 huambukizwa ugonjwa huu.Ugonjwa huu huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume kutokana na wanaume kutoonyesha dalili zozote wakati wa maambukizi au kutokana na majimaji ya kwenye tezi dume kuwa na madini ya Zinc ambayo huathiri vimelea hivi vya Trichomonas Vaginalis vinavyosababisha ugonjwa huo.
MAAMBUKIZI;
Trichomoniasis huambukizwa kwa njia ya kujamiiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathiriwa na ugonjwa huo.Wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huu ,ili kuufahamu ugonjwa huu vyema kwanza tufafamu nini kinachotokea wakati wa maambukizi(PATHOFIZIOLOJIA)ya ugonjwa huu.
-Umbile la vimelea vya Trichomonas Vaginalis ni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe kwa upana ingawa wakati mwingine ukubwa unaweza kutofautiana kulingana na mazingira.
-Kuwepo kwa umbile kama mikono kwa nje ya kwenye kimelea hicho inayojulikana kama FLAGELLUM ,husaidia vimelea hivi kuingia kwenye tishu za mrija wa kupitishia mkojo na tupu ya mwanamke na hivyo kuharibu seli aina ya EPITHELIUM na kusababisha vidonda katika tishu hizo hali ambayo husababisha watu walioathirika na ugonjwa huu kuwa kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa VVU na magonjwa mengine ya zinaa.
Trichomoniasis huanza kuonekana kuanzia siku ya 4-28 baada ya mtu kupata maambukizi.Kwa wanawake Trichomoniasis huathiri shingo ya kizazi (cervix),mrija wa mkojo,tupu ya mwanamke,kibofu cha mkojo na tezi zinazojulikana kama BARTHOLIN Glands na Skene Glands.
-Kwa wanaume vimelea hivi hupatikana katika sehemu za siri,sehemu ya nje ya mrija wa kupitishia mkojo(Anterior Urethra),kwenye tezi dume,kwenye mirija ya kuhifadhi na kutoa mbegu za kiume(EPIDIDYMIS) na hata kwenye mbegu zenyewe.
DALILI KWA WANAWAKE;
1.Uchafu unaotoka kwenye tupu ya mwanamke ambao huwa na rangi mchanganyiko ya njano na kijani au rangi kama kijivu na huwa mzito sana.
2.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
3.Kutoka harufu kwenye tupu ya mwanamke
4.Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
5.Shingo ya kizazi kuwa nyekundu hali ambayo hugundulika wakati daktari anamfanyia mgonjwa uchunguzi
6.Kuwashwa sehemu za siri(sio wanawake wote)
7.Maumivu chini ya kitovu kwa baadhi ya wanawake
Ingawa wanawake ndio huonyesha dalili na viashiria vya ugonjwa huu mara nyingine wanaweza kuwa na vimelea hivi hata kwa muda wa miaka kadhaa hata kama vipimo vya uchunguzi havitaonyesha kama wameathirika na vimelea vya ugonjwa huu.
DALILI KWA WANAUME;
Baadhi ya wanaume huwa hawaonyeshi dalili zozote .Baadhi ya dalili zinazoonekana ni;
1.Kuwashwa ndani ya uume
2.Kutokwa na uchafu au majimaji kwenye uume
3.Kuwashwa au kuhisi kichomi baada ya kujisaidia haja ndogo au baada ya kutoa mbegu za kiume
Baada ya mtu kuhisi dalili hizo anashauriwa kwenda hospitali au katika vituo vya afya ili kufanyiwa uchunguzi na vipimo.
VIPIMO;
Trichomoniasis hugundulika kwa kutumia vipimo
1.Kipimo cha darubini ambapo daktari humfanyia mgonjwa uchunguzi kwa kuingiza kifaa maalum katika tupu ya mwanamke na kuchukua kipimo kwa kutumia pamba maalum.Hatua hii hufanywa kitaalam bila kusababisha maumivu kwa mgonjwa na kisha kupelekwa maabara ili kuangalia kama kuna vimelea vya Trichomonas Vaginalis.Kwa kufanya uchunguzi huu daktari anaweza pia kuangalia kama kuta za ndani za tupu ya mwanamke au shingo ya kizazi (cervix) zimeathirika kwa kuwa na vidonda ambavyo ni vyekundu.
2.Kwa mwanaume daktari huchukua kipimo cha uchafu unaotoka sehemu za siri au hupangusa sehemu hizo za siri za mwanaume kwa wale ambao hawatoi uchafu au majimaji yoyote kwa kutumia pamba na kupeleka maabara kufanyia uchunguzi.Pia kipimo kilichochukuliwa na daktari kinaweza kuoteshwa kwenye maabara(culture) na kuangalia kama kuna uoto wa vimelea vya Trichomonas Vaginalis baada ya siku tatu.
3.Kuangalia kiwango cha tindikali(PH)-daktari anaweza kuangalia kiwango cha tindikali kwenye tupu ya mwanamke kwa kutumia karatasi maalum ya kkipimo hiki ijulikanayo kama PH paper,ambapo kiwango kama ameathirika itakuwa PH zaidi ya 5.Kwa kawaida PH ya tupu ya mwanamke inakuwa ni ya tindikali(acidic) kuanzia PH 3.8-4.5 .Magonjwa yanayobadilisha PH ni pamoja na;Trichomoniasis na Bacteria Vaginosis.Mabadiliko hayo humfanya mwanamke kuwa kwenye hatari ya maambukizi tofauti.
4.Kipimo cha damu -hufanywa ili kuchunguza Prostate Specific Antigen(PSA).PSA ni aina ya protin inayozalishwa na seli za tezi dume.Uzalishaji wake huongezeka wakati seli za tezi dume zinapoongezeka kuelekea kuwa kansa inayojulikana kitaalam kama BPH au wakati tezi dume inapopata maambukizi(PROSTITIS),na katika saratani ya tezi dume.Kipimo hiki hufanywa kwa wanaume wanaopata ugonjwa wa Trichomoniasis mara kwa mara au wale wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea na ambao wamepata ugonjwa huu wanapaswa kufanyiwa kipimo hiki angalau mara 1 kwa mwaka.
5.Pap smear -hiki ni kipimo kingine ambapo chembechembe au seli za shingo ya kizazi huchukuliwa na kuchunguzwa kwa kutumia darubini.Kipimo hiki pia hutumiwa katika uchunguzi wa wanawake kujua kama wamepata saratani ya shingo ya kizazi au la.Wanawake wenye zaidi ya miaka 18 au wale wenye upungufu wa kinga ya mwili wanashauriwa kufanya kipimo hiki angalau mara 1 kwa mwaka ili kujua afya zao.
6.Kipimo cha kuangalia maambukizi ya VVU-walioathirika na Trichomoniasis wanapaswa kufanyiwa kipimo cha kuangalia kama wameambukizwa ugonjwa wa HIV.
7.Kipimo cha mkojo na damu-hufanywa kuangalia wingi wa damu,chembechembe tofauti za damu na chembechembe bapa(Platelets)
MATIBABU;
Tiba ya trichomoniasis ni kutumia dawa aina ya Metronidazole au Flagyl.Dawa hii haitumiki kwa wanawake wenye ujauzito chini ya miezi 3 au wanaonyonyesha hivyo basi kabla ya kutumia dawa hii ni vyema ukamuona daktari.Kwa wale walioathirika na ugonjwa huu wa zinaa wanashauriwa kupata tiba pamoja na wenzi wao .Madhara mengine ya dawa ya Metronidazole mbali na madhara kwa wamama wajawazito na wanaonyonyesha ni pamoja na;
1.Mzio(mcharuko wa mwili)yaani allergic reaction
2.Kichefuchefu
3.Kukauka midomo
4.Kuharisha
5.Kuhisi ladha kama ya chuma mdomoni
6.Kushuka kiwango cha chembechembe nyeupe za damu(leukopenia)ambazo hutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na hivyo upungufu wake hufanya mtu awe katika hatari ya kupata maambukizi tofauti tofauti.Mcharuko wa dawa hii mara nyingi hutokea iwapo masharti ya dawa hayakufatwa vyema au mtu anapokunywa dozi ya dawa zaidi ya alivyoelekezwa na daktari.Ni muhimu kufahamu kuwa unapohisi hali kama hizo katika matibabu yoyote inakupasa kuacha kutumia dawa zinazokudhuru na kumuona daktari haraka.
Katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunazo dawa za mimea zisizi na kemikali zozote na isiyo na madhara kwa wajawazito na wanyonyeshao yenye uwezo wa kutibu siyo Trichomoniasis pekee bali magonjwa yote sugu ya zinaa kama kaswende,kisonono,klamidia,UTI n.k.Dawa hiyo inajulikana kwa jina la LMTM-N7/SUZ.Kwa wale waliofika katika kituo chetu ni mashahidi wa uwezo wa dawa hii kutibu magonjwa yote ya zinaa.
NB;LMTM HERBAL CENTRE ndicho kituo pekee ndani ya Tanzania,Afrika mashariki kati na kusini mwa Afrika chenye uwezo wa kutibu magonjwa ya zinaa sugu na uzazi.
MADHARA YA TRICHOMONIASIS;
1.Ugonjwa huu ni miongoni ya magonjwa ya zinaa ambayo huongeza hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa mengine kama HIV kama tulivyokwisha sema huko nyuma.
2.ugonjwa huu husababisha mwanamke kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo
3.Huwaongezea wanawake hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi
4.Kuongeza hatari kwa wanaume kupata saratani ya tezi dume.
KITUO CHETU CHA LMTM HERBAL CENTRE KINAPATIKANA ILALA MCHIKICHINI MTAA WA USANGU,
MOBL;+255776 217 417,
fax2email+255 736 601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com
Jumatano, 3 Septemba 2014
UNATAKA KUPUNGUZA UNENE ?SOMA HII HAPA
Hapa nakuletea ratiba ya kupunguza unene/uzito kwa muda wa siku saba kwa kutumia lishe maalum;(1)Siku ya kwanza asubuhi kula matunda(lakini katika matunda hayo usile ndizi).Mchana chemsha kabichi,weka chumvi kidogo na nyanya na upate supu kisha kula mchanganyiko huo.Jioni kula tikiti maji na mboga mboga au kabichi uliyotengeneza mchana.
(2) Siku ya pili kula mboga za majani asubuhi (usile mboga za majani zenye wanga kama karoti).Mchana kula kabichi iliyochemshwa ,tengeneza na kachumbari.katika kabichi weka chumvi,pilipili na mafuta ya olive.Jioni unaweza kula mlo kama wa mchana lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani.
(3)Siku ya tatu kula mboga za majani na matunda ,unaweza kuongeza kiazi kitamu kimoja .
(4)Siku ya nne kula ndizi moja na unywe na maziwa ya mtindi wakati wa asubuhi ,Mchana kula kabichi kama ulivyoitengeneza kwenye siku ya kwanza,usiku rudia mlo wa mchana.
(5)Siku ya tano kula nyanya nn pamoja na samaki au kipande cha kuku asubuhi.Mchana unaweza kula samaki wa kuchemsha kiasi ambaye amechanganywa na nyanya.Wakati wa jioni unaweza kula chakula kama cha mchana.
(6)Siku ya sita unaweza kula chakula cha protin na mboga za majani.Anza siku kwa kula kachumbari asubuhi.Mchana kula tambi kiasi na kipande kidogo cha samaki.Usiku tengeneza supu ya kabichi.
(7)Siku ya saba anza kwa matunda na juisi,Mchana kula mboga za majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.
NB:Unatakiwa kunywa maji angalau glasi nne kila siku.Dayati hii ni kwa siku saba tu.
Jumapili, 6 Julai 2014
ZIJUE DALILI,TIBA NA UCHUNGUZI WA TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO

TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO(KIDNEY STONES)
-Figo ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu,hufanya kazi ya kuchuja damu huku ikiondoa sumu zote za mwili,figo hufanya kazi ya kurekebisha kiasi cha maji mwilini(electrolyte level).
kabla damu haijapita katika figo,huwa imebeba maji na takataka nyingi sana(urea),lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu lakini,masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwa ni pamoja na kiwango cha maji kilichozidi hupitishwa kwenye mirija miwili(ureters)kuelekea kwenye kibofu(urinary bladder) na kishas kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo(urethra)
Mkusanyiko wa kemikali hizi(chemical crystals),wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga,kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadi wengine hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo katika figo yenyewe(neprone) au kwenye mirija ya kupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu(ureteter),hapo ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kusikia maumivu makali.
DALILI ZA UWEPO WA MAWE KWENYE FIGO;
Mtu mwenye mawe kwenye figo huonyesha dalili zifuatazo;
a.Maumivu ya mgongo na kiuno
b.Mkojo kutoka ukiwa na rangi ya damu
c.Kutokwa na jasho wakati wa usiku
d.Kupatwa na homa kali kwa wakati flani ikiambatana na kutetemeka mwili
e.Kuhisi kichefuchefu na kutapika
f.Mkojo kuwa na harufu kali
g.Maumivu makali sehemu za mbavu
h.Miguu kujaa maji/kuvimba.
i.Maumivu ya tumbo chini ya kitovu upande wa kushoto au kulia kutegemea ni figo ya upande gani iliyoathirika.
j.Maumivu makali unapogusa upande wa figo iliyoathirika.
KISABABISHI CHA MAWE KATIKA FIGO(KIDNEY STONES);
1.Matumizi ya baadhi ya dawa husababisha mtu kupata mawe katika figo pindi anapozitumia kila mara.Dawa hizo ni kama vile za kutibu kansa na HIV,antibiotic kama ciprofloxacin,cefrtriaxone na madawa yenye sulphur kama metacalphin nk.
2.Utumiaji wa vyakula vyenye kuongeza vitamin A na D,ambavyo huongeza kwa kiasi kikubwa madini joto mwilini
3.Kuishi kwenye mazingira ya joto sana bila kupata maji ya kutosha husababisha kiasi cha chemical kuongezeka katika figo na kusababisha zigandamane na kutengeneza mawe ndani ya figo.
4.Maambukizi ya magonjwa ya figo kama renal tubula acidocis ctc,huongeza hatari ya kupata tatizo hilo.
5.Kurithi kutoka kwa wazazi (wanakuwa na homoni ziitwazo antiduretic hormone)zisizoweza kufanya kazi ya kuchuja damu kikamilifu na mwishowe hutengeneza mawe katika figo.
6.Utumiaji wa vyakula vyenye protin zinazotokana na wanyama na chumvi nyingi(huongeza hatari ya kupata tatizo hili)
7.Unene kupita kiasi
JINSI YA KUGUNDUA TATIZO;
1.Mgonjwa kufanyiwa X-Ray au scan ili kujua kama ana mawe katika figo.
2.Vipimo vya damu(blood test)
3.Vipimo vya mkojo(urenarlulisis)
TIBA YA TATIZO;
-Ikiwa mgonjwa baada ya uchunguzi atagundulika kuwa na tatizo hili hupewa mojawapo ya tiba zifuatazo:
1.Extracorporeal shock wave lithotripys(eswl)-Hii ni mionzi inayoelekezwa katika figo ili kuyeyusha mawe (chemical au sumu zilizogandamana)ambazo huvunjwavunjwa na hii mionzi kisha mgonjwa hukojoa vipandevipande.
2.Percutaneous nephrolithotomy(PCNL)-Hiki ni kifaa chenye mwanga na kamera ambacho huingizwa kwenye kokwa za figo (nephrone)ambayo huvunjavunja mawe katika figo.
3.Ureteroscopy-Kifaa hiki huingizwa kwenye mirija ya kupitishia mkojo(urether)kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu ili kuondoa mawe yaliyokwama kwenye mirija na kuzuia mkojo kutoka.
4.Stone removal-Hapa mgonjwa hufanyiwa operesheni ya kuondoa mawe moja kwa moja.
- Kama tulivyoona tiba hizi zina madhara na ni ghali.Hivyo basi kabla hujaenda katika tiba hizi zenye madhara makubwa ni muhimu kutumia tiba mbadala na tiba asili ili kuepuka madhara mengine.
Katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunayo dawa asili zenye uwezo mkubwa wa kutibu tatizo hili la mawe kwenye figo bila madhara yoyote.Aina hizi za dawa hufanya kazi za kuyeyusha kemikali na mafuta yaliyogandamana katika figo na kuzibua mirija iliyojiziba ili kuruhusu mtiririko wa mkojo kuwa kama unavyotakiwa.
Baadhi ya madawa tuliyonayo ni;
a.LMTM-F5/AFH2
b.LMTM/S32/J
Dawa hizi mbali na kutibu matatizo ya mawe katika figo zinauwezo wa;
1. kutibu saratani ya kizazi,kusafisha mirija ya uzazi na kutoa maji katika mirija hiyo
2.Uvimbe wowote ndani ya mwili
3.Kurekebisha hedhi iliyovurugika kwa akina mama(hasa waliowahi kutumia dawa za uzazi wa mpango)
4.Saratani ya ini na kibofu cha mkojo
5.Kusafisha mfumo mzima wa njia ya mkojo
6.Huwasaidia akina mama wenye kasoro mbalimbali katika via vya uzazi,waotafuta uzazi kupata watoto
Ijumaa, 30 Mei 2014
IMARISHA UWEZO WA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA KULA MATUNDA NA MBOGAMBOGA

Ili mtu awe na afya bora na hatimaye aweze kumudu tendo la ndoa ni lazima mwili wake upate virutubisho kama vile;
a.wanga
b.mafuta
c.protini
d.vitamin na madini kwa kiwango sahihi kutoka katika chakula
Moja ya sababu ya mtu kupoteza hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa ni msongo mzito wa mawazo.Msongo wa mawazo unaufanya mwili kushindwa kuzalisha kiwango tosha la vichocheo ya kufanya tendo la ndoa.Kwahiyo hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa inapungua.Sababu nyingine inayosababisha mtu kukosa hamu na nguvu ya tendo la ndoa ni vyakula.
Ili mwanaume aweze kuwa na hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa lazma tezi dume lake liwe na afya bora.Madini ya zinki ambayo hupatikana kwa urahisi katika maharage,vitunguu,matango,karoti,spinachi,kabichi na matunda mbalimbali husaidia kufanya tezi dume kuwa imara.
Baadhi ya vitamini kama;
1.vitamini A inayopatikana kwa wingi katika spinachi,karoti,matikiti na maembe.Inaweza kubadili lehemu kuwa kichocheo madhubuti katika kufanya tendo la ndoa.
2.vitamini B inayopatikana kwa wingi katika viazi,ndizi na maboga husaidia kutengeneza vichocheo katika tendo la ndoa
3.vitamini E inayopatikana kwa wingi katika vyakula vya asili kama vile pumba za ngano,majani machanga ya mtama,ufuta na matunda ya aina mbalimbali kwa kiasi kikubwa inaimarisha maisha ya mu katika kufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu.Upungufu wa vitamini E mwilini unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume mwilini.
Ulaji wa ndizi unasaidia kupunguza msongo wa mawazo kwa sababu ya kuwa na madini ya potassium kwa wingi ambayo husababisha mwili kuongezeka kwa wingi vichocheo vya tendo la ndoa.Kwa mwanaume kazi moja ya tezi za dume ni kutoa majimaji yaliyochanganyika na mbegu za kiume wakati wa kufanyika tendo la ndoa.
Baadhi ya watu hutumia dawa au hormonies ili kuongeza nguvu ya kufanya tendo la ndoa.Matumizi ya aina zozote za dawa yana changamoto zake,ikiwemo madhara ya kiafya na kiuchumi hivyo watu wanashauriwa kujenga tabia ya ulaji bora na kufanya mazoezi ili kuweza kukabili tatizo hilo.Ulaji wa kudumu wa matunda na mbogamboga au juisi za asili unaimarisha afya na kumpa mtu nguvu na hamu ya kufanya tendo la ndoa. Hata hivyo ieleweke kuwa kuna baadhi ya watu kama vile wasiozalisha vichocheo,tiba yao sio chakula pekee bali ni lazma waende hospitalini kufanyiwa vipimo na kup[atiwa tiba sahihi kulingana na tatizo walilonalo.
Tahadhari:matumizi holela ya madawa yanaweza kuleta madhara katika figo au kudhoofisha kabisa nguvu ya kufanya tendo la ndoa.
KWA MAONI,USHAURI TUWASILIANE KUPITIA;
MOBL:0776 217417,
fax2email +255736661119.
email;lmtmherbal@rocketmail.com
Jumapili, 16 Februari 2014
MISKI NI DAWA MUJARABU KWA WANAOWAHI WAKATI WA TENDO LA NDOA NA MENGINEYO

-Miski ni mfalme wa aina zote za mafuta mazuri na ni matukufu zaidi.Ni mafuta ambayo hupigiwa mfano mzuri kwa kufadhilishwa kuliko mafuta mengine.
SIFA ZA MISKI;
-Miski hali yake ina joto na inauyabisi katika daraja la pili.
-Ina harufu na ladha yake ni tofauti na mafuta mazuri mengine.Ukitaka kutofautisha miski feki na halisi,ni kwamba katika tiba za kimwili miski feki haiwezi kutibu maradhi maduka mengi yanauza miski feki ambazo sio zile zilizokusudiwa kutuka katika tiba.Ikiwa unahaja ya tiba hakikisha umeata miski asilia.
TIBA ZA MISKI;
1.Huchangamsha na kusafisha mishipa ya fahamu na ubongo.
2.Huongeza hisia,ashiki na ladha za tendo la ndoa kwasababu huzidisha matamanio na joto mwilini
3.Huwasaidia wanawake wasiokuwa na ashki(hisia) na ladha wakati wa tendo la ndoa.Tunayo pia dawa ya ziada ya kuongeza nguvu,hisia na hamu yatendo la ndoa kwa wanawake dawa hii ulizia katika kituo chetu cha lmtm herbal centre.
4.Huwasaidia wanaume wanaowahi kumaliza tendo la ndoa kabla ya mke.Namna ya kutumia wasiliana na wataalam wetu waliopo katika kituo chetu kilichopo ilaa cha lmtm herbal centre.Kwa ziada ya haya tunazo dawa zingine za kuongeza nguvu za kiume ambazo ni za kunywa na za kuchua kwa kuimarisha na kuipa nguvu mishipa ya dhakal.Dawa hii pia ni mujarab kwa kuchelewesha kuwahi kutoa manii haraka
5.Husaidia wanawake waliomaliza siku zao za hedhi kuondoa harufu mbaya.Pia hupunguza umajimaji na harufu mbaya itokayo ukeni
6.Hukazanisha utupu wa mwanamke na kufanya sehemu hiyo kuwa ndogo
NB:Kufahamu namna ya kutumia miski kama dawa kutibu magonjwa yaliyotajwa hapo juu pamoja na wapi pa kupata miski halisi wasiliana na kituo chetu cha lmtm herbal centre kilichopo ilala mchikichini mtaa wa usangu jijini dar es salaam;
Simu no;+255776217417,
fax2email+255736601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com
USIACHE KULIKE PAGE YETU YA LMTM HERBAL CENTRE
Ijumaa, 14 Februari 2014
Jumanne, 11 Februari 2014
FAIDA ZA PILIPILI KICHAA KIAFYA NA KITIBA
- Jamii nyingi hususa Marekani na bara la Asia wana historia ya kutumia pilipili kichaa kama tiba.Ni dawa yenye nguvu sana na matumizi mengi,hutumika sana kwa kusafisha damu na kutoa sumu mwilini,pia hutumika kusisimua mzunguko wa damu na kuweka sawa uwiano wa tindikali(acid)mwilini.Pilipili kichaa imetumika kwa maradhi tofautitofauti ikiwemo moyo,gauts,kupooza,homa,kikohozi,tonsilatis,kichefuchefu na hemorhoids kwa miaka mingi huko Asia na mashariki ya mbali.
MAAJABU YA PILIPILI KICHAA;
13.Husaidia kuongezeka kwa kiwango cha METABOLIC kwa 23% ndani ya masaa matatu.14.Husaidia kupunguza cholestro na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu. KWA USHAURI,MASWALI;TEMBELEA PAGE YETU YA LMTM HERBAL CENTRE AU KUPITIA EMAIL; lmtmherbal@rocketmail.com,fax2email+255736601119NB:USISAHAU KULIKE PAGE YA LMTM HERBAL CENTRE.
1.Kutibu kidonda-Hii inaweza kuwa ni ajabu kwa walio wengi lakini ni tiba liyothibitishwa na imekuwa ikitumika miaka kadhaa iliyopita katika nchi mbalimbali.Sio tu kuzuia kutokwa na damu katika kidonda cha kujikata kama ilivyozoea kutumiwa na wengi huko majumbani kwa miaka mingi bali pia huzuia fangasi na bakteria kuingia katika uwazi wa kidonda hicho hutumika pia kuondoa sumu mwilini 2.Hufanya mwili kuweza kutumia vyema virutubisho vipatikanavyo kutokana na chakula3.Husaidia uyeyushaji wa mafuta mwilini/Kuchoma mafuta4.Pilipili ina antioxidants muhimu kama beta carotene,ina wingi wa vitamini A,C na K hebu tuziangalie vitamini hizo: a.Vitamini A husaidia kuweka sawa kinga ya mwili pia hutukinga na kansa na magonjwa ya moyob.Kazi ya vitamini C-ni kuzuia strock,magonjwa ya moyo,macho na kansa mbalimbali.Miili ya binadamu haiwezi kujitengenezea vitamini C,hivyo basi tunaweza kupata vitamini C kupitia chakula.c.Vitamini K-Husaidia katika ukuwaji wa mifupa,pia ni muhimu katika mzunguko wa damu.Pilipili zote huwa na Capsaicin ambayo kazi yake ni kupunguza maumivu,kuzuia kansa na magonjwa ya moyo.5.Inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu6.Huwasaidia watu wanene(over weight) au wanaougua ugonjwa wa kisukari.Hii ni kwa mujibu wa watafiti katika chuo kikuu cha Tasmania uliochapishwa katika American Joarnal of Clinical Neutition mwezi julai 2006.7.Inasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa INSULIN kwa 60% baada ya kula chakula8.Husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa RHEMATOID na ARTHRITIS kupata nafuu9.Husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja mwilini10.Husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua na kukufanya upumue kwa urahisi.11.Husaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya utumbo.
12.Husaidia kuongezeka kiwango cha METABOLIC ambayo husaidia kuchoma mafuta13.Husaidia kuongezeka kwa kiwango cha METABOLIC kwa 23% ndani ya masaa matatu.14.Husaidia kupunguza cholestro na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu. KWA USHAURI,MASWALI;TEMBELEA PAGE YETU YA LMTM HERBAL CENTRE AU KUPITIA EMAIL; lmtmherbal@rocketmail.com,fax2email+255736601119NB:USISAHAU KULIKE PAGE YA LMTM HERBAL CENTRE.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)





















.jpg)





