Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 10 Mei 2013

MAASAI TRADITIONAL MEDICINE(TIBA ASILI ZA KIMASAI): UKIMWI UNATIBIKA (LMTM-LE/37/VIH NDIO SULUHISHO)


MAASAI TRADITIONAL MEDICINE(TIBA ASILI ZA KIMASAI): UKIMWI UNATIBIKA (LMTM-LE/37/VIH NDIO SULUHISHO): Kwa kuanza tuangalie na kutafakari kabla ya kuamua na kujiridhisha kama ukimwi unatibika kwa kuangalia mambo mawili muhimu yafuatayo; 1.VVU...

UKIMWI UNATIBIKA (LMTM-LE/37/VIH NDIO SULUHISHO)


Kwa kuanza tuangalie na kutafakari kabla ya kuamua na kujiridhisha kama ukimwi unatibika kwa kuangalia mambo mawili muhimu yafuatayo;
1.VVU NI NINI
2.UKIMWI NI NINI

Kwa kuanzia tuangalie
1.VVU -Ni kifupi cha neno ''VIRUSI VYA UKIMWI'' ni virusi au vijidudu vinavyosababisha kudhoofika kwa mfumo wa kinga ya mwili wa binadamu.Aina hii ya virusi husababisha ugonjwa kwa binadamu tu.Hudhoofisha mfumo wa kinga ambao kwa kawaida humlinda mtu dhidi ya maradhi,virusi kama vilivyo virusi vingine.VVU ni viini au vijidudu vidogo ambavyo vinaingia kwenye vituo vilivyo hai na kutumia viumbe hai kujinakili.VVU husababisha UKIMWI (yaani ukosefu wa kinga mwilini)
2.UKIMWI-Ni mkusanyiko wa magonjwa mbalimbali ambayo hutokea wakati mfumo wa kinga ya mtu unapodhoofishwa na VIRUSI VYA UKIMWI.Kwa maelezo haya UKIMWI ambao ni mkusanyiko wa maradhi mbalimbali(magonjwa nyemelezi)yanatibika.Watu wengi wanashindwa kutofautisha UKIMWI na VIRUSI VYA UKIMWI.Watu wengi wenye VVU hujisikia wenye afya nzuri kwa muda wa miaka michache baada ya maambukizo,baadea huwa wagonjwa wa ukimwi.Virusi ni viumbe vidogo sana, vidogo mno zaidi bakteria wanaosababisha kifua kikuu au kipindupindu.Viini au vijidudu hivi ambavyo ni vya kawaida na ambavyo kila mmoja wetu hukabiliana au huambukizwa mara kwa mara katika maisha yetu ya kila siku.Virusi husababisha mafua,ugonjwa wa kupooza(polio),surua,machumbwichumbwi na flu.Virusi hivi huweza kuenea kwa kukohoa,chafya au kugusana.VVU ni tofauti.Pamoja na kwamba ni virusi lakini havienezwi kwa njia hizo tulizozitaja.VVU vyaweza kuenea tu kwa ngono,kuongezewa damu yenye VVU,sindano na vifaa vingine vyenye ncha kali na toka kwa mama kwenda kwa mtoto akiwa tumboni,wakati wa kujifungua na wakati wa kunyonyesha.
Ni vigumu kutibu VVU kwa madawa lakini ukimwi ambao ni mkusanyiko wa maradhi mbalimbali yatokanayo na kudhoofika kwa kinga ya mwili kulikosababishwa na vvu unatibika.Ukimwi kwa tafsiri nyingine ni magonjwa nyemelezi.Dawa zinazowaua bakteria kama vile penislini au tetracycline haziuwi virusi vya ukimwi.VVU ni virusi maalum vinavyojulikana kwa jina la RITROVIRUS ambavyo hujinakili vyenyewe kwa njia mbalimbali kuliko wale wa aina nyingine,kutokana na sababu hiyo ni vigumu sana kutibu virusi tofauti na ukimwi.Njia bora ya kuzuia kuenea kwa virusi na maradhi wanayosababisha kwa watu ni kuepuka maambukizo.Unaweza kuzuia kuenea kwa surua kwa kutumia chanjo,lakini vvu ni tofauti,kwa kubadili mwenendo tunaweza kuzuia kuenea kwa VVU.Mfano ni kunawa mikono baada ya kutoka chooni kunaweza kupunguza uwezekano wako wa kupata maradhi ya kuhara.Kubadili mwenendo pia kunaweza kuzuia kuenea kwa VVU.
Kuna aina mbili ya VVU:VVU-1 na VVU-2.Kama ilivyo kwa dada na kaka wanayo mambo wanayofanana na wanayotofautiana.VVU-1 hupatikana duniani kote wakati VVU-2 hupatikana afrika ya magharibi.Kwavile kuenea kwa virusi vyote hivi kunaweza kuzuiwa kwa njia moja ,tujadili kama VVU -2.
Kinga maana yake ni ulinzi na usalama.Mfumo wa kinga ya mwili hufanya kazi ya kuondoa viini au vidudu vinavyoshambulia mwili;mfano,virusi kama vile vinavyosababisha polio(ugonjwa wa kupooza),bakteria kama wale wanaosababisha TB viini au vimelea kama vile vinavyosababisha malaria na fangasi vinavyosababisha ukungu.Viini au vijiduu au vimelea hivi huwaingia watu na kusababisha maradhi na kifo.Mfumo wa kinga umeundwa na seli mbalimbali.Seli ni sehemu ndogo sana ya mwili wa binadamu ambayo huwezi kuziona bila msaada wa darubini.Mwili umeundwa na mabilioni ya seli.Kila seli aina fulani inajukumu maalum,baadhi ya seli huunda mifupa,nyingine huunda misuli,na nyingine mfumo wa kinga.
Seli za mfumo wa kinga kama ilivyo kwa seli nyingine zina kiini au kituo cha katikati kiitwacho NUKLIASI.Nukliasi au kituo cha kati au makao makuu ya seli ina aina fulani ya jini iitwayo DNA.Nukliasi hufanya kazi ya kuongoza au kuratibu shughuli zozote ndani ya seli.Hutoa taarifa kwa seli wakati muafaka wa kutengeneza mmiminiko unaohitajika wakati  wa kutengeneza seli mpya.DNA ndani ya seli hutumia sehemu tofauti mbalimbali zilizopo kwenye DNA kuratibu shughuli mbalimbali.Kama mfumo wako wa kinga ukikabiliana na kitu kilichopo nje ya mwili inatengeneza vitu vidogovidogo fulani vilivyotengenezwa na protini vinavyoitwa ANTIBODI(askari).Hivi hujishikiza kwenye kitu kilichoingia mwilini na kuusaidia mfumo wa kinga kwa ujumla kuvitafuta na kuviharibu.Hii inatoa nafasi kwa mwili kuepuka maradhi au kupona  kama alikuwa ameugua.
Protini maalum iitwayo CD4 huweka alama nje ya baadhi ya seli ya mfumo wa kinga na kutofautisha na aina nyingine ya seli za kinga.Alama ya CD4 ni kama michirizi au mistari ya aina fulani inayotofautisha kama ile inayotofautisha pundamilia na punda punda kihongwe.Seli za CD4 pia huitwa msaidizi(seli za Tsaidizi)kwa sababu mwili huzitumia kutambua na kulinda dhidi ya wavamizi kama vile virusi na bakteria.Hata hivyo pamoja na juhudi zote hizo hatimae virusi hufanikiwa kuingia kwenye seli nyeupe zenye tabaka la CD4 juu yake.Kwa maana nyingine seli za CD4 hushambuliwa na vurusi hivyo vya VVU,ambazo zinajaribu kuzizuia zisilete madhara.Hili ni tatizo kubwa kwasababu mwili huhitaji seli aina ya CD4 ili kujilinda zenyewe dhidi ya maradhi.Hii ndio sababu inayofanya wenye VVU waugue maradhi ambayo kwa kawaida mtu asiye na VVU hupambana nayo na kuyatokomeza.Viini vya bakteria,fangasi,virusi vingine na vimelea vinavyotegemea viumbe vingine hutumia mwanya huo kuingia kwenye mwili wa mtu ambaye mfumo wake wa kinga umedhoofika na kusababisha maradhi yanayojulikana kwa jina la;MAGONJWA NYEMELEZI(UKIMWI)na ndio yanayowauwa wenye VVU.
VVU vinapoingia ndani ya mwili hutafuta seli za CD4.Vikishafanikiwa kuvipata seli za CD4 vinajishikiza kwenye seli na kuingia ndani.Mara vinapokuwa ndani VVU hukutana na DNA ndani ya nukliasi ya seli.Hapo huanza kujinakili vyenyewe kwa kutumia nyenzo za kujinakili zilizopo katika DNA ya seli,halafu nakala hizo hujificha katika DNA ya seli ya CD4.Ukiangalia kwa darubini utaona DNA ya seli kuwa ya kawaida ingawaje imechanganyika na DNA ya VVU.Mara VVU vinapofaulu kujificha kwenye DNA ya seli,VVU vinaweza kufanya mojawapo ya mambo mawili -kirusi kinaweza kukaa kimya ndani ya seli hai au kinaweza kubadili DNA ya seli na kutumia uwezo wa seli kutengeneza nakala yake yenyewe.Hujinakili nakala kwa kutumia aina fulani ya ute (protini).Kama vikianza kuongezeka huweza kutengeneza maelfu ya virusi vipya.Virusi vipya huacha seli na kuingia ndani ya seli nyingine ya CD4 na mambo tuliyoyaeleza hapo juu hujirudia tena.Kama DNA ya VVU ikikaa ndani ya DNA ya seli hakuna njia nyingine ambayo mwili unaweza kutumia kutenganisha na kutokomeza.Virusi huwa vinajificha vizuri kiasi ambacho hata mwili unashindwa kutambua kwamba kuna virusi hapa. Uwezo huu wa kujificha ndio unaowawezesha kuenea mwilini. Pamoja na uwezo wa kujinakili vyenyewe ndani ya seli iliyoathirika virusi vina njia nyingine ya kuzaliana.Seli inapoamua kutengeneza seli nyingineinatengeneza DNA ya VVU yake yenyewe.Hivyo kila mara seli mpya inapotengenezwa,VVU navyo hutengenezwa.Kwa sababu hiyo siyo rahisi kuelezea tofauti iliyopo kati ya DNA ya VVU na DNA ya seli ya mwili wa binadamu na hakuna dawa iliyopo ya kuweza kuteketeza virusi vyote vilivyopo mwilini.
Watu hutengeneza dawa za maradhi au magonjwa yanayowatokea watu waliokwisha ambukizwa  VVU baada ya mifumo yao ya kinga kudhoofika.Pia wanajishughulisha na njia zitakazosaidia VVU visiongezeke kwa hali hiyo tutaeleza tu dawa zinazotumika kutibu magonjwa nyemelezi(ukimwi)na sio VVU.kuna njia nne zinazotumika kupambana na VVU inapoingia mwilini ,wakatiVVU vinapoingia ndani ya seli,wakati VVU vinapokuwa sehemu ya DNA ya seli,wakati VVU inapotengeneza nakala nyingine kwa ajili ya kuingia seli nyingine.Kuna aina mbili tu za dawa zinazokabiliana na VVU ''Reverse transcriptase inhibitors''mfano AZT,DDI DDC,Nevirapine na D4T ambazo huzuia kirusi cha UKIMWI kuwa sehemu ya DNA ya seli.Aina nyingine ya dawa ni protease inhibitor kama vile saquinavir,indinavir na ritonavir ambazo huzuia VVU kujikusanya pamoja na kujinakili kwa kuchelewesha uwezo wa kirusi kutengeneza nakala yake yenyewe.Dawa hizi mara nyingi huwawezesha waathirika wa VVU kuishi kwa muda mrefu pamoja na kwamba dawa hizi haziwezi kuondoa kabisa VVU au kumponya muathirika wa VVU.VVU vinakuwa sehemu ya mwili wa mtu na hakuna njia ya kutokomeza virusi vyote mwilini.Hii inamaana kwamba mtumiaji lazima atumie dawa hizi maisha yake yote ambalo ni tatizo jingine.Mtu anayetumia dawa hizi kwa mtiririko mzuri inafikia hatua ambayo dawa haziwezi kumsaidia tena kwa sababu VVU vimeshakuwa sugu.Lingine ni kwamba mtu anayezitumia dawa hizi anaweza kupata madhara yanayotokana na dawa hizi.Kwa kuzingatia maelezo hayo ndiyo maana LMTM CENTRE inakuletea dawa ya LMTM-LE/37/VIH inayotibu pamoja na ukimwi(magonjwa nyemelezi)dawa hii pia husaidia kuongeza CD4,kuondoa sumu zozote mwilini inayosababishwa na dawa mbalimbali na vyakula mbalimbali na haina madhara kwa mtumiaji anayetumia ARV'S.Badala yake humsaidia muathirika kuondoa sumu zinazoachwa na dawa za ARV'S mwilini.Dawa hii haina madhara kwa namna yoyote ile ukizingatia inatokana na mchanganyiko wa mimea ya asili iliyoandaliwa kwa njia za asili.Natumai makala haya yamefafanua vizuri VVU ni nini na UKIMWI ni nini na kwamba ukimwi unatibika wakati VVU haitibiki kama tulivyoeleza kwa undani.Soma makala zilizopita na zinazoendelea za LMTM.
Kwa maoni,ushauri,tiba,na maswali
fax2email+255736601119
www.facebook.com/losila maasai
lmtmherbal.blogspot.com
lmtmherbal@rocketmail.com

Jumamosi, 4 Mei 2013

JE WAJUA ASALI INA UWEZO WA KUTIBU MAGONJWA MBALIMBALI ?


MAAJABU YA ASALI;
Huko Misri kuligunduliwa mwili wa mtoto ambao haukuoza katika mojawapo ya wafalme wa zamani ,mwili huo ulikuwa umetiwa ndani ya chombo kilichojazwa asali.Tukio hili laonyesha kuwa asali ina siri kubwa iliofanya mwili wa mtoto huyu kutooza tangu miaka 4500 iliyopita.

JINSI YA KUJITIBU BAADHI YA MARADHI KWA ASALI.
1.Kujikuna(allergy)
Tia asali ndani ya kikombe na kisha ongeza vaselini na mafuta waridi jipake mahala panapowasha asubuhi na jioni,na jiepushe na vinavyochochea kujikuna.
2.Uzuri wa uso
Upake asali uso wote wakati mwili upo katika mapumziko baada ya robo saa osha uso kwa maji ya vuguvugu na kausha,halafu jipake kidogo mafuta ya zaituni.Endelea kufanya hivi kwa muda wa wiki moja mfululizo.
3.Jeraha(kidonda)
Paka asali penye kidonda na funga bandeji na uepushe umajimaji,usifungue mpaka baada ya siku tatu.
4.Kuungua
Chukua asali na uchanganye na vaselini kiasi kama kama hicho cha asali halafu jipake mahala palipoungua asubuhi na jioni mpaka ile ngozi iliyoungua ibanduke.Au changanya yai katika asali kiasi cha kijiko kimoja na jipake mahala palipoungua kila siku.
5.Kuua chawa na mayai yake
Paka kichwa chote asali pamoja na kukisugua vizuri mpaka uhakikishe kuwa  imeingia vema hadi mashinani halafu jifunge kitambaa iwe kabla ya kulala.Asubuhi osha kwa maji ya uvuguvugu pamoja na kuchana nywele .Endelea namna hii kwa muda wa wiki moja mfululizo.
6.Kukosa usingizi
Chukua glasi ya maziwa na changanya na asali kijiko kikubwa na unywe kabla ya kulala.
7.Maradhi ya kinafsi na wazimu
Mgonjwa ale asali na mgongo wake uumwe na nyuki,na pale alipoumwa apake asali.Aendelee hivyo japo kila mwezi mara moja na aendelee kula asali,kutafuna nta yake na nyuma ya kichwa chake apake sega la nyuki kidogo.
8.Kifafa
Asubuhi kabla ya kunywa chai,anywe asali kikombe kimoja na jioni kikombe kimoja.Aendelee hivyo kwa wiki moja.
9.Magonjwa yote ya macho
Jipake asali asubuhi kama vile unapaka wanja,vilevile kabla ya kulala pamoja na kunywa asali kijiko kimoja.
10.Kiungulia/Asidi
Meza punje ya kitunguu saumu kabla ya kula meza na kikombe cha maziwa yaliyochanganywa asali kijiko kimoja kwa muda wa siku tano.
11.Kuhara/Tumbo la kuendesha
12.Kufunga choo
Kufunga choo ni kinyume cha kuharisha.Chukua maziwa baridi kikombe kimoja korogea asali ndani yake kijiko kimoja halafu unywe,fanya hivyo asubuhi na jioni.
13.Kutapika
Chemsha karafuu na korogea asali halafu kunywa kiasi cha kikombe kimoja kabla ya kula chakula;kutapika na kichefuchefu kutaisha.
14.Kidonda
Chukua asali nusu kikombe na kikombe cha maziwa na changanya unga wa ganda la ndizi lililokaushwa kijiko kimoja,Tumia asubuhi na jioni kwa muda wa mwezi
15.Maradhi ya kifua
Chukua juisi ya figili kikombe kimoja na korogea asali kijiko kimoja.Kunywa asubuhi na jioni.Vilevile unaweza kuchukua ubani dume ukautia ndani ya maji na kuchanganya na asali kijiko kimoja ili kuyapa mapafu nguvu.
16.Harufu mbaya mdomoni
Chukua asali vijiko viwili ikoroge ndani ya maji na kisha chemsha katika moto mdogo mpaka itoe moshi. Vuta puani na mdomoni moshi huo kupitia kwenye paipu au bomba lililofungwa vizuri katika chombo.Endelea na tiba hii pamoja na kutafuna nta ya asali.
17.Kukaukiwa na sauti
Fany kama dawa hiyo iliyotangulia (harufu mbaya)pamoja na kugogomoa asali na chumvi kidogo kwa muda wa siku tatu.
18.Homa ya mafua(Influenza)
Vuta puani moshi wa kiziduo cha asali na kitunguu maji kabla ya kulala pamoja na kunwa asali kijiko kimoja baada ya chakula.Tiba hii hufanywa kwa kuchukua asali na kitunguu maji kidogo kilicho chambuliwa maganda;vikatiwa katika chombo chenye maji na kuchemsha juu ya moto mdogo hadi moshi utoke.
19.Malengelenge ngozini
Chukua binzari nyembamba kiasi cha kikombe na changanya na asali nusu kikombe kisha chemsha pamoja na kuhifadhi ndani ya chupa safi halafu uwe ukijipaka.
20.Maumivu ya fizi na kuyapa meno nguvu
Changanya asali na siki na usukutue asubuhi na jioni.Vilevile waweza kusugua fizi kwa asali;sugulia kwa mswaki(asali iwe ndio dawa ya mswaki)dawa hii hukinga meno yasioze na huyapa meno na fizi nguvu.
21.Mishipa iliyovimba
Kwa maradhi yote ya ugonjwa huo pamoja na vidonda tumia asali kama mafuta ya kujipaka mara tatu kwa siku.Jipake taratibu na kunywa asali kijiko kimoja kila umalizapo kula.Endelea hivyo mpaka utakapopona.
22.Kidonda kilichooza
Chukua asali kikombe kimoja na mafuta ya ini la samaki kikombe kimoja yachanganye pamoja na ujipake baada ya kusafisha kidonda kwa asali iliyochanganywa na maji ya moto.Fanya hivyo kila siku hadi upone.
23.Kidonda kisichopona
Tumia gundi ya asali kwa maradhi haya.Jifunge bandeji kwa gundi hiyo pamoja na kukisafisha kila siku na kubadilisha bandeji,pamoja na kunywa asali kijiko kimoja asubuhi na jioni kabla ya kula chakula.
24.Kifua kikuu na mapafu
Changanya maji ya waridi na asali vipimo sawa  alafu kunywa kikombe kimoja asubuhi na jioni na ujipake kifuani na shingoni .Mafuta ya zaituni yaliyopigwa kwenye asali jipake kabla ya kulala.Endelea hivyo mpaka upone.
25.Uvimbe wa tishu za msuli kwenye moyo na kutetemeka
Changanya asali vijiko viwili ndani ya maji ya baridi glasi moja kisha unywe kabla ya kula chakula .
26.Moyo kubana
Kila baada ya kula kunywa asali kijiko kimoja ikifatiwa na juisi ya karoti.Fanya hivyo kwa muda wa mwezi mmoja
27.Uvimbe mdomoni na ulimi kufura
Tia kijiko cha asali ndani ya nusu kikombe cha maji ya moto na sukutua mara tatu kwa siku kila siku.
28.Maradhi ya masikio na maumivu
Changanya asali katika maji na chumvi kidogo na utie sikioni matone kidogo kabla ya kulala kila siku.
29.Baridi yabisi(Rheumatism)
Kunywa asali iliyochanganywa na maji na mafuta ya habatsouda(maji yawe ya uvuguvugu).Pia jipake mafuta ya habatsouda yaliyochanganywa na mafuta ya kafur na mafuta ya zaituni na asali kwa vipimo sawa;Jipake kabla ya kulala na jifunge kitambaa cha sufi mahali panapouma.Pia kuumwa na nyuki penye maumivu hutibu baridi yabisi,baada ya hapo paka asali mahali palipoumwa.
30.Jongo(Edema)
Kunywa mchanganyiko wa asali na ubani dume asubuhi na jioni.
31.Sugu/Chunju
Chukua gundi ya nyuki upashe moto na kuweka juu ya sugu na ufunge vizuri kisha acha kwa siku tatu mpaka sugu iondoke.
32.Magonjwa ya ini
Chukua ganda la muoka (mualoni)lisage vizuri,chukua kiasi cha kijiko kimoja ukoroge katika asali na uwe ukila kabla ya kula chakula kwa muda wa mwezi mmoja.
33.Kutia nguvu na nishati
Chemsha majani ya chai halafu uyachuje na kuchanganya na asali.Kunywa kama chai kila siku.
34.Maradhi ya wanawake na uzazi
Kunywa kikombe kimoja cha asali kwa mama anayesikia uchungu wa kuzaa humsaidia kuzaa kwa urahisi.Baada ya kuzaa mzazi ale kwa wingi mkate wa ngano asili na asali.Kwa anayetaka hedhi imtoke na pia kumaliza maumivu yake Chemsha uwatu kiasi cha kikombe kimoja,ongeza asali na anywe kila siku asubuhi na jioni.Pia inashauriwa mwanamke kusafisha uke kwa asali na maji ya moto ili kumpatia nafuu,badala ya kwenda kusafishwa na vifaa vinavyo muumiza na kumdhuru.
35.Nguvu za kiume
Chukua vitunguu maji vitatu viponde na kuvikamua vizuri maji yake kisha changanya na asali kiasi hichohicho cha maji ya vitunguu na ubandike juu ya moto mdogo huku ukikoroga mpaka povu la asali limalizike halafu tia ndani ya chupa.Kunywa kijiko kimoja kila baada ya kula kila siku.Waweza pia kuiboresha kwa kuongeza habatsouda na figili iwe kama jam (marhamu).
36.Utasa/ugumba
Kula mkate wa nyuki ulio mpya yaani baada ya kutolewa kwenye mzinga na baadae kunywa maziwa ya ng'ombe glasi moja yaliyochanganywa na unga wa pembe ya kifaru miligram tatu.Fanya hivyo kwa mda wa mwezi mmoja.
37.Saratani
Chukua mkate wa nyuki kutoka mzingani moja kwa moja kiasi cha miligram miamoja kula kila wiki mara moja ikifatiwa na kula asali pomoja na nta yake kila siku kiasi cha kikombe kimoja na sugua mwili wako kwa asali na mafuta ya habatsouda kisha oga baada ya lisaa limoja kwa maji ya vuguvugu na baadae kula asali iliyochanganywa na unga wa habatsouda katika juisi ya karoti kila siku.
38.Ukoma
Changanya asali na amonia na jipake kila siku hadi upone.
39.Kinga ya sumu
Chukua mafuta ya ufuta (simsim)kiasi cha kijiko kimoja changanya kwenye kikombe cha asali na uwe unakunywa kila asubuhi na jioni kunywa asali iliyochanganywa kwenye kikombe cha maziwa ya moto na ambari kidogo endekea hivyo kila siku kwa muda wa siku tatu pamoja na kutokula nyama.
40.Tezikibofu
Kula mkate wa nyuki kutoka mzingani moja kwa moja kiasi cha miligram hamsini kisha oga na maji ya vuguvugu yaliyochanganywa na asali wakati wa jioni.

KWA MAONI,USHAURI,TIBA NA MASWALI TUANDIKIE ;
FAX2EMAIL+255736601119,
WWW.FACEBOOK.COM/LOSILA MAASAI
lmtmherbal.blogspot.com,
EMAIL;lmtmherbal@rocketmail.com