Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 13 Januari 2014

IJUE HABATSOUDA NA UMUHIMU WAKE KATIKA TIBA YA MARADHI MBALIMBALI

Habatsouda ni punje nyeusi yenye umbo mthili ya ufuta ndani yake imebeba dwa yenye faida kubwa.Huko misri huitwa habbatul-barakh(punje ya baraka),vilevile huitwa kamun aswad.Huko Iran huitwa shaniuz ama huku Afrika Mashariki hujulikana kwa majina ya habalsoda,yai jeusi na zenyeu.
      Habalsoda ina viini vyenye adhari nzuri,ladha nzuri na faida kubwa.Ndani yake kuna fosfeti,chuma,fosforasi,kabohaidreti na mafuta 28%.Vilevile ina viua sumu(antibaotik)vyenye kuangamiza virusi,viini vya maradhi na vijidudu.Pia ina karotini inayozuia saratani,homoni inayoongeza nguvu za kiume na nishati mwilini.Pia inasafisha mkojo na kutoa safura.Ina vimeng'enyo (enzymes) na kizima-asidi(ant asid),pia ina viini vyenye kuburudisha na kuchangamsha kwa wakati mmoja.
     Ndani yake kuna faida na manufaa yanayomfanya mtu kutotumia madawa ya famasi.

                       MAGONJWA YANAYOTIBIWA KWA KUTUMIA HABALSODA KWA USHAURI WA WATAALAM WA TIBA MBADALA NI HAYA YAFUATAYO;
1.KUNYONYOKA NYWELE
   Kanda uga wa habalsoda katika juisi ya kachiri(komoni/rocket)pamoja na kijiko cha siki nyepesi na kikombe cha mafuta ya zaituni kisha sugua kichwa kwa mafuta hayo.(kwa maelezo zaidi wasiliana na daktari)
2.MAUMIVU YA KICHWA
   Chukua unga wa habalsoda,karafuu iliyosagwa nusu ya kiwango cha habalsoda na anisuni,changanya pamoja,chukua kiasi cha kijiko cha chai na ule na maziwa ya mgando.Waweza pia kusugua mahali panapouma kwa mafuta ya habalsoda.
3.UKOSEFU WA USINGIZI
   Chukua kijiko cha habalsoda changanya na glasi ya maziwa ya moto yaliyochanganywa na asali kunywa yakiwa ya vuguvugu.
4.CHAWA NA MAYAI YAKE
   Chukua unga wa habalsoda ukande kwenye siki mpaka uwe kama marhamu alafu jipake kichwani baada ya kunyoa nywele au sugua marhamu kwenye mashine ya nywele alafu kaa katika jua kwa muda wa robo saa.Usioshe kichwa mpaka baada ya masaa matano.
5.KISUNZI NA MAUMIVU YA SIKIO
   Tia tone la mafuta ya habalsoda katika sikio na kunywa na sugua sehemu za panda uso na nyuma ya kichwa kumaliza kisunzi.
6.UPAA NA MABAKA
   Kijiko cha unga wa habalsoda,siki kiasi cha kikombe kimoja mafuta ya kitunguu thaumu kikombe kidogo changanya na ujipake baada ya kunyoa nywele.
7.MALENGELENGE YA NEVA KATIKA NGOZI
   Jipake sehemu ya malengelenge mafuta ya habalsoda mara tatu kwa siku
8.MARADHI YA WANAWAKE NA UZAZI
   Dawa kubwa ya kurahisisha kuzaa ni habalsoda iliyochemshwa na kuchanganywa na asali.Tumia pia mafuta ya habalsoda katika kinywaji cha moto kwa maradhi yote ya wanawake.
9.MENO NA MAUMIVU YA FINDO NA KOO
   Chemsha habalsoda na utumie kwa kusukutua,kugogomoa husaidia sana maradhi yote ya mdomo na koo.Vivyo hivyo bugia kijiko cha habalsoda kwa kumeza na maji yenye vuguvugu kila siku na kupaka mafuta yake sehemu ya ndani ya koo.
10.MARADHI YA TEZI
   Chukua unga wa habalsoda na kanda kwa asali na sega la nyuki kila siku
11.CHUNUSI
   Chukua unga wa habalsoda ukande katika mafuta ya simsim pamoja na kijiko cha unga wa ngano.Jipake usoni jioni na asubuhi halafu osha kwa maji ya vuguvugu na sabuni na uwe unakunywa mafuta ya habalsida kwenye vinywaji vya moto.
12.MARADHI YA NGOZI
   Mafuta ya habalsoda,mafuta ya waridi/marashi jabali na unga wa ngano asili.Changanya kwa viwango sawa alafu ukande vizuri.Osha sehemu iliyoathirika kwa siki nyepesi alafu kaa kwenye jua na baadae ujipake dawa hiyo kila siku.Tahadhari epuka kula vyakula vinavyochochea hisia(aleji) mfano;samaki,maembe,mayai na mfano wake.
13.SUGU/CHUNJUA/WART
   Chukua unga wa habalsoda ukande katika siki nzito na sugua kwa kitambaa cha sufi au katani mahali penye sugu.
14.KUNG'ARISHA USO NA KUREMBESHA
   Kanda unga wa habalsoda katika mafuta ya zaituni kisha jipake usoni.
15.KUUNGANISHA MVUNJIKO HARAKA
   Supu ya adesi/dengu,kitunguu maji pamoja na yai la kuchemsha na kijiko kikubwa cha unga wa habalsoda changanya na supu hiyo kula siku baada ya siku.Sugua pia sehemu karibu na mvunjiko kwa mafuta ya habalsoda yenye vuguvugu.
16.MVILIO WA DAMU
   Chemsha kiganja kimoja cha habalsoda kisha chua sehemu iliyovilia damu na maji hayo kwa muda wa robo saa au zaidi.Baada ya hapo jipake mafuta ya habalsoda na usifunge
17.BARIDI YABISI(RHEUMATISM)
   Chua kwa mafuta ya habalsoda ya moto halafu kunywa mafuta ya habalsoda yaliyochemshwa na kuchanganywa na asali.
18.KISUKARI
   Unga wa habalsoda kikombe kimoja,manemane iliyosagwa kiasi cha kijiko kikubwa,habbarrshad nusu kikombe,koma manga iliyosagwa kiasi cha kikombe kimoja mzizi wa kabichi iliyosagwa baada ya kukaushwa kiasi cha kikombe kimoja na kijiko kidogo cha mvuje kula kiasi cha kijiko kimoja na mziwa ya mgando ili iwe rahisi kumeza.
19.SHINIKIZO LA DAMU(HIGH BLOOD PRESHA)
   Kila unywapo kinywaji cha moto tia matone machache ya habalsoda
20.UVIMBE WA FIGO
   Tengeneza kibandiko cha unga wa habalsoda iliyochanganywa katika mafuta ya zaituni na ubandike sehemu yenye maumivu ya figo pamoja na kubugia fundo la mafuta ya habalsoda kila siku.
21.KUVUNJA VIJIWE TUMBONI
   Chukua kikombe cha habalsoda kisha ukande katika asali na kitunguu thaumu na ule kabla ya chakula kila siku.
22.KUKOJOA KWA MAUMIVU
   Paka mafuta ya vuguvugu ya habalsoda kwenye kinena  kabla ya kulala pamoja na kunywa kikombe cha mafuta hayo kilichochanganywa na asali
23.KUKOJOA BILA KUKUSUDIA
   Habalsoda,maganda ya mayai yaliyosafishwa na kuokwa na kusagwa yatie kwenye maziwa na kunywa kiasi cha kikombe kimoja kila siku
24.JONGO(EDEMA)
   Weka kibandiko cha unga wa habalsoda kilicho kandwa katika siki juu ya kitovu na kula kijiko cha habalsoda asubuhi na jioni.
25.KIFUKO CHA NYONGO NA VIJIWE VYAKE
   Habalsoda kiasi cha kijiko kimoja,manemane robo kijiko na asali kikombe kimoja kula kila asubuhi na jioni.
26.WENGU
   Weka kibandiko cha habalsoda iliyokandwa na mafuta ya zaituni weka kibandiko katika ubavu wa kushoto kila jioni.Na wakati huo kula uwatu uliochanganywa na asali na mafuta ya habalsoda kidogo.
27.MARADHI YOTE YA KIFUA NA BARIDI.
   Mafuta ya habalsoda kijiko kikubwa itie kwenye maji yaliyochemka na kufuka moshi kisha uanze kuuvuta ule moshi huku umefunika kichwa ili ule moshi usiende upande mwingine fanya hivyo kila siku kabla ya kulala pamoja na kunya zaahatari iliyochanganywa na uga wa habalsoda
28.MOYO NA MZUNGUKO WA DAMU
   Kula asali iliyochanganywa na habalsoda kila siku.
29.MCHANGO(MSOKOTO WA TUMBO)
   Chemsha anisuni,binzari nyembamba(kamuni)na naanaa kwa kipimo sawa na tia asali kidogo tia matone ya habalsoda na kunywa kikiwa na uvuguvugu pamoja na kupaka mafuta ya habalsoda mahali panaposokota
30.KUHARA
   Juisi ya chirichiri iliyochanganya na unga wa habalsoda kijiko komoja kikubwa kunywa kutwa mara tatu.
32.UZIWI
   Chemsha habalsoda pamoja na karafuu kunywa bila kuongeza kitu
33.GESI NA MAUMIVU
   Kula unga wa habalsoda kijiko kimoja kabla ya kula kisha fuatisha glasi ya maji ya moto iliyotiwa asali ya muwa kiasi cha vijiko vitatu
34.ASIDI
   Habalsoda,asali na maziwa ya moto kumaliza asidi
35.UVIMBE WA TUMBO
   Unga wa habalsoda kijiko kimoja na kijiko cha urkusus changanya na juisi ya peas iliyochanganywa na kokwa zake
36.MARADHI YA MACHO
   Paka habalsoda sehemu za kandokando na macho na kope kabla ya kulala na kunywa matone kadhaa ya mafuta ya habalsoda katika kinywaji chochote cha moto au katika juisi ya karoti..
37.AMOEBA(AMIBA)
   Unga wa habalsoda kijiko kimoja,kitunguu thaumu kilichosagwa changanya katika kikombe cha juisi ya tomato iliyotiwa chumvi kidogo,kunywa kila siku kabla ya kula chakula.
38.KICHOCHO
   Kula habalsoda kijiko kimoja kila asubuhi na jioni na kujipaka mafuta yake
39.KUTOA WADUDU TUMBONI
   Kijiko kimoja cha unga wa habalsoda,punje tatu za kitunguu thaumu,kijiko kimoja cha mafuta ya zeti,pilipili manga kidogo na punje kumi za boga kisha fuatisha mafuta ya nyonyo/mbarika/mbono
40.UTASA
   Unga wa habalsoda,unga wa uwatu na mbegu ya figili kwa kipimo sawa kula kijiko kimoja asubuhi na jioni ikiwa imekorogwa katika nusu kikombe cha asali na baadae fuatisha na kikombe kikubwa cha maziwa.
41.TEZI KIBOFU(PROSTATE GLAND)
   Jipake habalsoda chini ya mgongo na chini ya korodani na kusugua kwa mzunguko na kula unga wa habalsoda kijiko kimoja iliyochanganywa na kijiko kidogo cha manemane katika nusu glasi ya asali iliyotiwa katika maji yenye vuguvugu
42.PUMU
   Nusa moshi wa mafuta ya habaloda na kula unga wake kabla ya kula chakula kila siku na jipake mafuta yake kifuani na kooni kabla ya kulala
43.KIDONDA(VIDONDA TUMBO)
   Mafuta ya habalsoda,kikombe cha asali na kijiko cha maganda ya koma manga yaliyokaushwa na kusagwa kula kabla ya chakula na baadae kunywa glasi ya maziwa yasiyotiwa chochote
44.SARATANI(CANCER)
   Paka mafuta ya habalsoda pamoja na kula unga wake kila umalizapo kula katika juisi ya karoti
45.NGUVU ZA KIUME
   Habalsoda kijiko kimoja changanya ndani ya mayai saba ya kienyeji.Hatakama una miaka120 utapata nguvu.

   NB;MADAWA HAYA HUPATIKANA LMTM HERBAL  CENTRE PEKEE
         ;USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA LMTM HERBAL CENTRE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni