Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 26 Aprili 2013

AINA MPYA YA KISONONO YASAMBAA DUNIANI


Aina mpya ya vimelea vya ugonjwa wa kisonono au "gono"ambavyo vinahimili dawa(resistant to drugs)zinazotumika kutibu ugonjwa huu imegundulika duniani.Taarifa iliyotolewa na shirika la afya duniani(WHO)hivi karibuni imesema,ugonjwa wa kisonono unaoathiri mamilioni ya watu ulimwenguni  umeanza kuwa sugu dhidi ya dawa zinazotumiwa kuutibu na hivyo kuna hatari ya kutoweza kutibika kabisa.Shirika la afya duniani limetoa wito kwa serikali na madaktari kuongeza ufuatiliaji wa aina hii ya kisonono kutokana na ugonjwa wa kisonono kuwa na athari nyingi kama mcharuko(inflammatoin),ugumba,matatizo wakati wa ujauzito na vifo vya akina mama wajawazito.                                                                                                                     Aina hii mpya ya vimelea vya kisonono vinaonyesha usugu wa dawa zote za antibiotiki tunazotumia dhidi yake ikiwemo dawa za jamii ya cephalosporins ambazo ni dawa za mwisho katika kutibu ugonjwa wa kisonono.Miaka michache  ijayo, aina hii mpya ya kisonono itakuwa sugu dhidi ya dawa zote ambazo zipo.Inakisiwa watu milioni 106 ulimwenguni kote huathiriwa na ugonjwa wa kisonono kila mwaka.Ugonjwa wa kisonono pia huongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya ukimwi(vvu).Ugonjwa sugu wa kisonono sio tatizo la bara la ulaya au afrika pekee bali ni tatizo la dunia nzima kwa sasa,kwa mara ya kwanza vimelea sugu vya ugonjwa wa kisonono dhidi ya dawa aina ya cephalosporins viliripotiwa katika nchi ya japan ikifuatiwa na uingereza,hongkong na norway.                                                                           Wanasayansi wanaamini matumizi mabaya ya dawa aina ya antibiotiki pamoja na uwezo wa vimelea vya ugonjwa wa kisonono kubadilika na kuzoea mazingira mapya ndio chanzo kikuu cha kutokea kwa ugonjwa sugu wa kisonono na hivyo muda si mrefu ugonjwa huu utakuwa janga kubwa dunia nzima kama hatua za haraka hazitachukuliwa.Kuna uwezekano wa vimelea hivi sugu vya kisonono vinasambaa kwa sasa duniani bila kuweza kugundulika kutokana na nchi nyingi kutokuwa na utunzaji wa kumbukumbu nzuri wa ugonjwa wake.                                                                                                                                                                       Katika kituo chetu cha LMTM CENTRE tunazo dawa za LMTM/N7/SUZ ambazo zina uwezo mkubwa sana wa kutibu magonjwa yote ya zinaa (STD)sexual transmitted diseases).Kama muathirika atazitumia kwa kufuata maelekezo ya daktari na kwa dozi kamili dawa hii hutibu 100%.                                                       TOFAUTI YA KISONONO NA KASWENDE                                                                                                           Ni muhimu kueleza tofauti ya ugonjwa wa kaswende na kisonono kwa sababu kumekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ambao wanapotoa maelezo au malalamiko yao wamekuwa wakichanganya ugonjwa wa kaswende na kisonono.Kwa kawaida daktari anatakiwa amsikilize mgonjwa anavyojieleza kuhusu anavyojiskia kwa wakati huo,alianza kuumwa vipi na magonjwa mengine aliyowahi kuumwa hapo nyuma.Maelezo hayo kutoka kwa mgonjwa na majibu mengine atakayojibu baada ya kuhojiwa na daktari humsaidia daktari kujua vipimo vya aina gani akufanyie ili aweze kuelewa una ugonjwa gani na uko katika hatua gani ili kukupa matibabu yanayostahili.Inapotokea mgonjwa akatoa maelezo ambayo si sahihi inaweza kumfanya daktari atoe matibabu ya ugonjwa tofauti na ule unaoumwa na matokeo yake ni kuendelea kuumwa na kusababisha usugu wa ugonjwa kwa baadhi ya dawa.                                                                                               Kisonono ni ugonjwa tofauti na kaswende kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo;kwanza kabisa tofauti kubwa ni dalili za magonjwa haya,kisonono kina dalili ya kutokwa usaha sehemu za siri ambao huambatana na maumivu makali sana wakati wa kukojoa kwa wanaume na wanawake husikia mkojo kuchoma sana wakati wa kukojoa.Kwa watoto wanaozaliwa na mama mwenye ugonjwa wa kisonono mtoto atazaliwa na ugonjwa wa macho kwa kutokwa na matongotongo mengi na macho kuwa mekundu kwa sababu ya kushambuliwa na bakteria wa kisonono.Ukweli kisonono hutambulika mapema kuliko kaswende kwa sababu dalili zake ni bayana na zinamlazimisha mgonjwa kwenda hospitali au kununua dawa za kutuliza maumivu.Kaswende ni tofauti na kisonono dalili zake ni za kuota vipele mwilini na hata uambukizaji wake ni zaidi ya kisonono,japo magonjwa yote yanaweza kuanbukuzwa kwa njia ya kujamiiana.Kaswende inaweza kuambukuzwa kwa kugusa majimaji yanayotoka kwenye vipele vya mgonjwa wa kaswende,hata kuchangia taulo au shuka na mgonjwa huyo unaweza kupata maradhi hayo iwapo majimaji yanayotoka kwenye vipele hivyo,vimegusa ngozi yako.Wadudu wa kaswende wanaweza kupenya katika ngozi ya kawaida tofauti na ugonjwa wa ukimwi ambayo yanahitaji kuwepo michubuko ili yaingie mwilini. Dalili za kaswende ni hatari sana kwani ugonjwa zaidi ya vipele huendelea kukua ndani kwa ndani bila kujua na dalili kubwa zinajitokeza wakati ugonjwa umefikia hatua ya juu zaidi.                                                                                                             Dalili hizi ni pamoja na kuongezeka kwa vipele sehemu za siri na mwili mzima,kwa kina mama mimba hutoka mara kwa mara na kwa wale watakaojifungua salama basi utakuta mtoto ana kasoro za maumbile.Kaswende imeishawafanya wengi kuishia kuwa vichaa na kuokota makopo barabarani.Hata hivyo njia za kuyaepuka magonjwa haya zinafanana sana;kuacha kufanya ngono ni bora kuliko kupata magonjwa haya mawili,hii itakusaidia kuwa na nafasi ya kujipanga na kutafuta mpenzi au mchumba na wakati utakapofika mnakubaliana maisha ya pamoja na kuwa na mahusiano  ya ngono yaliyo salama.Kuwa na mpenzi mwaminifu ni muhimu sana kama wote mtatunziana heshima na asiingizwe mtu wa tatu katika mahusiano yenu ya kingono basi ujue kuwa magonjwa hayo mtayasikia kwa wengine kwani nyie mkiwa salama itaendelea hivyo maisha yenu yote.Mwisho nawasisitiza matumizi sahihi na ya mara kwa mara ya mpira wa baba au mama maarufu kama kondomu,hii imewasaidia wengi sana.Kondomu zinazuia magonjwa ya zinaa na hata mimba zisizotarajiwa,hivyo basi tujitahidi kuuliza na kuzijua dalili za magonjwa mbalimbali ili tusiwachanganye madaktari wanapotuhudumia.                                                                                            Kwa maelekezo zaidi au ufafanuzi tuwasi                                                                                                    FAX2EMAIL +255736601119,                                                                                                                 lmtmherbal.blogspot.com                                                                                                                             EMAIL:lmtmherbal@rocketmail.com na www.facebook.com/losila maasai

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni