Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 28 Aprili 2013

JITIBU MAGONJWA MBALIMBALI KWA KUTUMIA VITU MBALIMBALI VINAVYOKUZUNGUKA


MAGONJWA NA JINSI YA KUYATIBU
(1)PUMU-
Matumizi;(a)hutibiwa kwa kutumia;simbi zaidi ya 20,ndimu nyingi na asali.Kunywa mchanganyiko huu kijiko 1 mara3 kwa siku hadi upone.AU kula vitunguu maji kwa wingi
(b)Pembe ya mbuzi-kausha kisha usage na unga wake changanya na asali na ulambe mara 3 kwa siku
(2)NGUVU ZA KIUME-
Hutibiwa kwa kutumia;
(a)kitunguu swaumu-
Matumizi;ponda na changanya na asali ya njano na ulambe asali hiyo kijiko1 mara3 kwa siku tumia mchanganyiko huu kwa wiki 2.
(b)tende na rose-
matumizi;changanya na maziwa na kisha kunywa wiki1-wiki3.
(c)mchele mkavu-
(d)Tikiti maji,tangawizi,pilipilinafaka halisi,mbogamboga za majani
Matumizi;tafuna mchele kidogo lisaa limoja kabla ya kujamiiana utarudiwa na nguvu zako.
KIFUA/KUKOHOA-
Hutibiwa kwa kutumia mchanganyiko wa;asali,kitunguu maji,kitunguu swaumu na tangawizi;
Matumizi;twanga mchanganyiko huu pamoja kisha ndio utumie.
(3)MAGONJWA YA MOYO-
Matumizi;kunywa juisi ya vitunguu maji kwa wingi.
(4)MAPAFU-
Matumizi;kula zabibu au kunywa juisi yake kwa wingi kila siku.
(5)GESI-
Matumizi;kunywa maji glasi8 au zaidi kwa siku.
(6)MAWE KATIKA KIBOFU CHA MKOJO-
Matumizi;kula chakula kilichopikwa na manjano.
(7)UVIMBE KATIKA SEHEMU ZA SIRI NYUMA-
Matumizi;paka alovera mahali penye uvimbe mara 3 kwa siku.
(8)KUPATA CHOO KIKUBWA-
Matumizi;kunyia chai ya tangawizi
(9)KICHOMI-
Matumizi;kula ndizi mbivu kila siku.
MAJIPU NA VIDONDA VISIVYOPONA-
Matumizi;binzari ya manjano koroga katika maji upate uji mzito kisha paka sehemu iliyoathirika mara2 kwa siku.AUchanganya zafarani kiasi na unga wa risasi na weka maziwa ya mbuzi kidogo kisha paka kwenye kidonda.
(10)MAUMIVU MAKALI TUMBONI-
Matumizi;changanya vijiko2 vya tangawizi na castro oil kisha kunywa mara 2 kwa siku.
(11)MIFUPA ILIYOVUNJIKA-
Matumizi;kula nusu nanasi kila siku hadi upone.AU kaanga vitunguu maji na uboho(rojorojo)
(12)MAUMIVU YA VIUNGO/MGONGO-
Vifaa;mafuta ya simsim,haba souda,na pilipili manga
Matumizi;chemsha,chuja na paka kwenye maeneo yanayouma yakiwa na uvuguvugu.
(13)KUTAPIKA DAMU-
Matumizi;weka kuzubara katika siki kali masaa24,ongeza sukari na chuja kisha unywe kutwa mara3
(14)KUSAGA CHAKULA NA KUIMARISHA TUMBO DHAIFU-
Vifaa;habasouda vijiko2, pilipili manga2,karafuu2
Matumizi;changanya kisha kunywa kijiko1 cha chai ndani ya kinywaji chochote cha uvuguvugu
(15)KIFUA/MARADHI-
Vifaa;juisi ya figili kikombe cha kahawa,kijiko kikubwa cha asali
Matumizi;changanya na maji ya moto kikombe cha chai yaache yapoe ndio unywe kutwa mara2 asubuhi na jioni.
(16)KIKOHOZI CHA MUDA MREFU-
Vifaa;khardal,asali safi ya nyuki.
(17)KUONDOA COLESTEROL-
Vifaa;tembe 3,kitunguu swaumu,kijiko1 cha zaatari,maji lita1
Matumizi;chemsha kidogo kunywa kikombe1 mara3 kwa siku.
(18)HIGH BLOOD PRESSURE/LOW BLOOD PRESSURE-
Vifaa;papai na tangawizi
Matumizi;sagapapai na tangawizi kamua juisi yake kunywa kutwa mara2 AU chemsha na kunywa juisi ya mmung'unya mara3 kwa siku
(19)KIKOJOZI-
Vifaa;ufuta mweusi na maziwa
Matumizi;saga ufuta mweusi na unga wake koroga kijiko1 ndani ya maziwa kunya mara2 kwa siku asubuhi na jioni mpaka upone
(20)HEDHI ILIYOKITHIRI/HEDHI KWA WINGI-
Matumizi;koroga unga wa ufuta mweusi ndani ya maji ya moto kisha kunywa AU chukua unga wa giligilani glasi1 chemsha katika nusu lita ya maji kisha kunywa nusu glasi mara3 kwa siku.
(21)KISUKARI-
Matumizi;chukua kijiko1 cha mdalasini weka katika kikombe cha kahawa kunywa kutwa mara3 kwa siku40 AU tengeneza juisi ya bitter gourd kunywa kila siku
(22)MAUMIVU YA MIGUU NA MAGOTI-
Matumizi;chukua kijiko1 kidogo cha zafarani changanya katika chai ya moto kunywa kutwa mara3
(23)KUZUIA MIMBA KUTOKA-
Matumizi;chukua kijiko 1 cha unga wa amla changanya na asali,kunywa kwa muda wa wiki1
(24)KUACHA SIGARA-
Matumizi;chukua hamira changanya vijiko 2 katika glasi1 ya maji na unywe pamoja na unga wake,kunywa glasi1 kutwa mara3
(25)KICHWA-
Matumizi;kula samaki na tangawizi
(26)KUVIMBIWA-
Matumizi;kula ndizi mbivu
(27)BARIDI YABISI-
Matumizi;kula tangawizi
(28)KIBOFU-
Matumizi;kula kunazi nyekundu
(29)BP-
Matumizi;zabibu nyeusi1kg,giligilani nusu,twanga kisha uchemshe na kunywa nusu glasi mara 3
(30)KWIKWI-
Matumizi;twanga hiliki changanya na maziwa kisha kunywa glasi moja
(31)DEGEDEGE-
Matumizi;ponda vitunguu swaumu kisha mpake  mwenye tatizo hilo na uichome na mfukizie
(32)UGONJWA WA KUSAHAU-
Matumizi;chukua zabibu kavu changanya na kungumanga na utafune mara2 kwa siku21
(33)MAWE KATIKA FIGO-
Matumizi;kitunguu maji chekundu,cheupe na njano,kata vipande4 kila kimoja weka vipande hivyo katika sufuria baada ya kuvisaga acha ichemke kisha kunywa jusi yake
(34)DAMU PUANI-
Vifaa;siki,limao,chumvi
matumizi;chukua chumvi kijiko kidogo weka katika glasi changanya na siki mpaka  chumvi iyeyuke ,kamulia limao nusu tumia siku3 mpaka 4 mfululizo 

TIBA MBADALA KWA KUTUMIA MBOGAMBOGA NA MATUNDA
(1)BOGA-Lina vitamini B kwa wingi
HUTIBU;
a.Huupa mwili nguvu
b.Huondoa tatizo la kufunga choo
c.Hurekebisha utolewaji wa nyongo mwilini
d.Huongeza nguvu za kiume
e.Husaidia kuvunja nguvu za sumu mwilini
f.Husaidia kupata mkojo hivyo kusafisha figo
g.Husaidia kuondoa mawe kwenye figo(Kidney stone)
h.Linafaa kwa wagonjwa wa kisukari
i.Husaidia kuimarisha glandi za kiume zitoazo mbegu za uzazi(PROSTATE GLAND
MAANDALIZI
-Chukua boga lililokomaa na katakata lisage kwenye blender(kama huna blender waweza kuliponda kwenye kinu safi na likishalainika ongeza maji kidogo kusudi upate juice yake.Wakati unakamua juice usiondoe mbegu na kiini.
NB.MAANDALIZI HAYA HUTEGEMEA UGONJWA UNAOTAKA KUUTIBU
(2)KAROTI-Ina vitamini nyingi mbalimbali
HUTIBU;
a.kulainisha tumbo
b.Inapigana na kutibu upungufu wa damu
c.Inasafisha damu
d.Inasaidia kutibu uvimbe wa saratani
e.Inatibu baridi yabisi
f.Inatibu chunusi,vidonda tumbo,koo,macho na kibofu
MAANDALIZI;
-Chukua karoti kilo1 ponda iwe laini na kisha uchemshe kwa dakika 15 ndani ya maji lita 1 na nusu au mbili chuja,kunywa juisi yake kwa kutibu vidonda tumbo au saratani ya tumbo,saratani ya kizazi tumia nusu kikombe cha chai miezi 3 mpaka 6,kwa kurembesha uso nawia juisi yake kila asubuhi mfululizo kwa siku 5.
(3)UNGA WA MKAA-
Unaweza kupata kupata kutoka kwenye mti wa mkuyu,kifuu cha nazi,msonobari au mkaratusi
INATIBU;
a.Kuumwa na nyoka
b.Kunywa sumu
c.Uvimbe
d.Kutapika,kiungulia,macho,kuharisha na kuhara damu ,kusaga chakula,vidonda tumbo,tindikali na kuungua
MAANDALIZI
a.Choma kifuu cha nazi hadi kiwe mkaa
b.Saga uwe unga(kwa miti tumia magome)
-Chukua kijiko 1 kikubwa cha unga na koroga katika maji safi ya kunywa ya vuguvugu kikombe 1 kunywa kabla ya kula kwa kutibu vidonda tumbo,kutoa asidi
KUUMWA NYOKA-
-Shona kifuko cha kitambaaa.
-Chota unga wa mkaa kijiko kikubwa na uweke ndani ya kifuko na tia maji kidogo na ufunge na nyingine ndani ya maji vuguvugu kikombe 1 uwe kama uji na umpe anywe kwa mtu aliyekunywa sumu tumia njia hiyo ya kunywa
MACHO-
-Weka katika kifuko kama hapo juu na ufunge kwenye jicho ,fanya hivyo kwa siku 3 mfululizo wakati wa usiku.
(4)GILIGILANI-
Inatibu tumbo,moyo na hedhi nk
MAANDALIZI
-Vijiko 2 vikubwa vya giligilani iliyosagwa ndani ya maji lita 1 kisha chemsha kwa dakika 10 na kunywa nusu kikombe kutwa mara 3 kwa siku 5 
(5)NYONYO-
-Majani yanatibu kifua kikuu na uvimbe wa miguu
-Mizizi ni dawa ya mafindofindo,macho ya njano,uvimbe,kisonono na kaswende
-Kikonyo chake ni dawa ya kwikwi-jaza maji ya baridi katika kikombe cha chai na kikonyo mpe mgonjwa anywe kila baada ya dakika 3 mpaka kwikwi iishe
-Kunywa punje yake na maji glasi kwa siku kwa muda wa siku 5 inatibu MOTODASI AU MOTO WA MUNGU
-Tumia majani kwa kupasha moto na kufungia miguu inayouma au kukandia miguu inayouma
-Kwa magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende mizizi kiasi na chemsha ndani ya maji nusu lita kisha kunywa kikombe cha chai kutwa mara 3 kwa muda wa siku 5
(6)SWAUMU-
HUTIBU
a.Kuumwa kichwa
b.Kibofu cha mkojo
c.Matatizo katika damu,chunusi nk
d.Macho kutoona vizuri,pumu,figo,ukurutu(fungus),baridi yabisi,majipu nk
NAMNA YA KUITUMIA KUTIBU BAADHI YA MAGONJWA;
A.Shinikizo la damu:Tumia juisi ambayo waweza kuichanganya kwenye saladi kama chakula cha pembeni
MAANDALIZI
-Menya chengachenga za kitunguu swaumu zipatazo 10-30 na kuziponda na zikishalainika na kutoa maji kaua juisi yake na uweke kwenye chombo kisafi
-Chukua malimao 2 au 3 uyakamue upate juisi yake na ulichanganye na ile ya kitunguu swaumu na uiache usiku kucha na asubuhi koroga vizuri na anza kuitumia kwa kunywa kijiko 1 cha chai kila baada ya saa moja na hakikisha hukiachi kijiko hicho ndani ya juisi kwani hutengeneza sumu.Magonjwa ya kichwa pia hutibiwa kwa njia hii kama unataka kuitumia kutibu magonjwa kwa muda mrefu waweza kuichemsha na kuiweka katika chupa safi pindi inapopoa na utumie kikombe cha chai kila asubuhi na jioni na pia waweza kutumia saladi yake wakati wa chakula.
B.Ukurutu(fungus)-
-Twanga kitunguu swaumu na weka kwenye eneo lililoathirika na uifungie kwa bandeji na kuacha kwa nusu saa na endelea kufanya hivyo kwa muda wa wiki mbili hii ni pamoja na magonjwa ya ngozi
C.Vidonda mdomoni,mafindofindo,kuharisha,maumivu ya tumbo na kunyonga-
-Kwa matatizo mengine ya kifua kula kikonyo kimoja cha kitunguu swaumu kutwa mara tatu kulingana na ukubwa wa kitunguu.
(7)NANASI-
-Nanasi lina vitamini A,B,C pia lina madini ya chuma ,calcium, na copper ambayo ni muhimu kwenye mifupa,meno,neva na misuli(MUSCELS)
HUTIBU;
a.Matatizo mbalimbali ya tumbo,magonjwa ya bandama(SPILEN),ini,utumbo mwembamba,homa,magonjwa ya midomo(VIDONDA),magonjwa ya koo,ugonjwa wa kusahau,maradhi ya akili,hali ya kukosa mori(LOW SPIRIT)
b.Aidha nanasi huondoa matatizo ya wanawake ambayo husababishwa na upungufu wa shughuli za homoni au makosa fulani katika sehemu ya yai ,huondoa shida ya kufunga choo,baridi yabisi,upungufu wa damu(ANEMIA) na maambukizo kwenye maungio ya mifupa(ARTHRITIS).Aidha kwa kula au kunywa juisi ya nanasi husaidia akina mama wanaonyonyesha walio na maziwa kidogo na hata wale wajawazito wanashauriwa kutumia mananasi
-Pia ni kichocheo kizuri katika kupona haraka kwa mifupa iliyovunjika.
BIRINGANYA(EGGS PLANTS)-
-Tunda la biringanya ukilipika kama mboga linatibu vidonda tumbo na linasaidia kupata usingizi.Kwa wale wenye tatizo la kukosa usingizi (INSOMNIA)wanashauriwa kula biringanya kwa wingi.
-Biringanya huharakisha kupona magonjwa na kuleta afya nzuri mwilini.Ikumbukwe kuwa usingizi ni kitu muhimu sana kwa afya ya mwili wa binadamu na ustawi wake.
-Kwa kutumia tunda hili kama mboga katika mlo ulao husaidia kunenepesha kwa wale wanaotaka kunenepa.hakikisha katika mlo ulapo na ufurahie chakula unachokila kila siku ,tumia kwa muda wa mwezi mmoja utaona matokeo yake.

KWA USHAURI, MAONI,MASWALI NA TIBA TUANDIKIE KUPITIA;
lmtmherbal.blogspot.com au lmtmherbal@rocketmail.com au www.facebook.com/losila maasai au dr.elhachym.ly@gmail.com na kwa kupitia
fax2email+255736601119 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni