Wamasai hasa wanaoishi milimani hutumia vitu mbalimbali katika kupambana na maradhi mbalimbali.Mara nyingi tiba hutolewa kulingana na aina ya ugonjwa,umri wa mgonjwa na mgonjwa yuko katika hali gani.Katika jamii ya kimasai tiba hufanywa na wataalam waliobobea katika tiba wanaojulikana kwa majina ya ILOIBONOK.Wataalam hawa wana heshimika sana katika jamii lakini heshima yao hupotea pale ambapo hutoa huduma kwa hisani au kwa sadaka ndogo hutoza pesa ili waweze kutimiza majukumu mengine kulingana na mahitaji yao.Katika jamii ya sasa,jamii imechangia kwa kiasi fulani kuharibu hadhi ya ILOIBONOK kwa kutowapa huduma za kutosha kulingana na umuhimu wao katika jamii husika.Kwa msingi huo wa OLOIBINI ale nini,avae nini,na afurahi vipi iwapo anao wahudumia hawasaidii kukidhi haja zake?Maswali haya humpa haki ya kutoza gharama kiasi kwaajili ya utowaji wake huduma.Muhimu ni azingatie kuwa tiba ni haki ya kila mtu hivyo aweke gharama ambayo haimfanyi tajiri kupata na masikini kukosa. Pamoja na kuwa kwa kipindi hiki kuna LOIBONOK wa uongo ni jukumu la jamii kuwakataa waongo ili hadhi na heshima ya LOIBONOK isidhalilishwe.Kwa hali hiyo utaalam,maarifa na ujuzi uhifadhiwe ili jamii ya maasai ihifadhike kiafya.Afya njema huwezesha jamii kuhifadhi mimea na wanyama sio kwa chakula tu bali pia kwa matibabu ya vizazi vya leo na vya baadae.Utamaduni wa kulinda kutunza na kustawisha utaimarisha na kudumisha urithi walioturithisha mababu zetu nasi tuirithishe jamii.Ikumbukwe kuwa kutunza madawa haya na kuyaenzi utaimarisha nia ya kutunza mazingira,wanyama na mimea ya asili. Kama ilivyo kichwa cha habari hapo juu,sasa tuangalie baadhi ya tiba za maasai zinavyotolewa kwa njia mbalimbali na vitu mbalimbali. (1)KUTAFUNA-Njia hii hutumika katika utoaji wa huduma za dharura na haraka kwa kutumia miti shamba katika jamii ya maa.Majani hutafunwa na mtu asiyekuwa na vidonda kinywani na ni lazima awe mtaalam au vilevile asiwe mtaalam lakini kwa kufuata maelekezo ya mtaalam na hupakwa au kubandikwa kwenye jeraha au kukamuliwa maji yake ambayo ni mchanganyiko wa dawa na mate na kupewa mgonjwa mahututi au mtoto mdogo mgonjwa ambaye hawezi kutafuna dawa kwa uoga au udogo wake.Njia hii pia hutumika kuandaa dawa kwa ajili ya kusafisha chuchu za mama aliyetoka kujifungua muda mfupi kabla ya mtoto kunyonyeshwa.Njia hii ya kuandaa dawa za haraka kwa ajili ya kuumwa na nyoka,masikio kuuma,macho kuwasha na kuzuia kuvuja damu baada ya tohara au ng'ombe kutolewa damu kwa matumizi bila kuua ng'ombe,mbuzi au ngamia (2)KUKAANGA AU KUPASHA MOTO-Baadhi ya madawa huandaliwa kwa njia ya kukaanga au kupasha moto kabla haijatumika kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali,baadhi ya magonjwa hayo ni kama;vidonda vya nje,uvimbe wa matezi ,kuteguka,maumivu ya mgongo,kifua na maradhi sugu ambayo mara nyingi tiba zake hutolewa kwa kuchanganya zaidi ya aina tano za dawa ili kupata dawa iliyo bora kuliko mchanganyiko wa vitu viwili au vitatu hasa kwa magonjwa sugu nk. BAADHI YA JAMII YA MIMEA MUHIMU KATIKA TIBA ZA MAA (1)ILOODWA/OSEKETETI(MYSINE AFRICANA)- Mti huu ni mti muhimu sana na ni dawa mama katika tiba yajamii ya maa.Kila sehemu ya mti huu ni dawa inayotibu maradhi mbalimbali ya asili na ya kisasa.Dawa hutolewa kulingana na ugonjwa unaoutibu,pia dawa hii huchanganywa na miti mingine kutegemeana na ugonjwa unaotaka kuutibu.Mchanganyiko huo hufanywa kulingana na maelekezo ya mtaalamu wa miti dawa.Baadhi ya magonjwa yanayo tibiwa kwa kutumia mti huu(oloodwai)ni;minyoo ya tumboni,tegu,minyoo uzi,maumivu ya kifua,baridi yabisi,viungo kukakamaa,kufunga choo,amoeba,typhoid,malaria,udhaifu wa mwili,kaswende,kisonono,matatizo ya ini,moyo kujaa maji,unene usio hitajika,kisukari,uchafu katika damu,vidonda vibichi,vidonda kooni,pepo punda,upungufu wa madini joto mwilini,upele,presha,fangasi nk. (2)ORKUJUK(PRUNUS AFRICANA)- Huu ni mti muhimu sana kwa maasai waishio sehemu za miinuko ambao hutumika kutibu magonjwa yafuatayo;homa,homa za vipindi,maumivu ya tumbo,maumivu ya mifupa,kuvimbiwa,mwili kujaa maji,miguu kuvimba,baridi yabisi,kukosa hamu ya kula,kuimarisha mifupa iliyo zeeka,malaria,bandama,kutoa sumu ya chakula,kuhara na kuhara damu nk. (3)ORKINYEI(EUCLEA DIVINORUM)- Mti huu kama ilivyo mingine ni muhimu katika tiba ya kupambana na maradhi mbalimbali katika jamii ya maa.baadhi ya magonjwa yanayotibiwa na mti huo ni;chango la mwezi,pneumonium,maumivu ya kifua,pumu,kifaduro,tambazi,uvimbe tumboni,kuharisha,minyoo,mwili kulegea,kukosa hamu ya kula na kuongeza cd4 kwa wenye vvu ikichanganywa na miti mingine kwa maelekezo ya mtaalam. (4)OLNG'ERIANTUS LOO NDOYE(GALIUM APARINOIDES)- Mti huu hutumika kutibu magonjwa yafuatayo katika jamii ya maa.Magonjwa hayo ni;mwili kuvimba,maumivu ya viungo,maumivu ya tumbo,upungufu wa madini joto,saratani,upele,kuwashwa na mwili,mapunye,unene usiohitajika,mafuta kwenye mishipa,uzito wa viungo na misuli.Kwa matokeo bora huchanganywa na miti mingine kwa ushauri wa daktari. MVULE/MILICIA EXCEISA- Mti huu hutumika kusafisha damu na pia waweza kutumia kutibu magonjwa mengine kwa kuchanganya na miti mingine kulingana na ugonjwa unaoutibu. (5)ORBUKOI/MKUNDEKUNDE/MLUNDALUNDA/MZOKA(CASSIA ABREVIATA)- Hutumika kwa kusafisha damu,hedhi kuvurugika,magonjwa ya zinaa,malaria na ugumba. (6)OSENGWAI/MKUNDEKUNDE(CASSIA ALATA) - Hutibu minyoo,magonjwa ya ngozi,malaria,maumivu ya viungo nk. (7)OLOISUKI/MLUNGULUNGU/MJAFARI(ZANTHOXYLUM CHALYBEUM)- Hutibu malaria,homa,kichwa,kisukari,ngozi,hedhi kuvurugika,maumivu ya kifua,meno,fizi kutoa damu na tambazi. (8)OLDULE(RICINUS COMMUNIS) Huu ni kati ya miti muhimu katika tiba za asili za jamii ya maa.Baadhi ya magonjwa yanayotibiwa kwa kutumia mti huu ni;kuhamisha majipu ikichanganywa na oloisuki,kukosa hamu ya kula,kusafisha tumbo,vidonda tumbo,kuhara,kuchelewa kuzaa au kuchelewa kutoa kondo la nyuma baada ya kujifungua,pumu kwa kuchanganywa na magadi,masikio kuvuja usaha,kifaduro,kufungua tumbo lililofunga choo na kulainisha ngozi. (9)ENDISIA(CONYTZA PYRRHOPPA)- Pia ni moja ya miti muhimu katika tiba asili na tiba mbadala katika jamii ya maa inayoishi katika sehemu za miinuko.Nayo hutumika kutibu baadhi ya magonjwa yafuatayo;mafindofindo,kansa ya koo,mafua yasiyopona,mafua ya vipindi,kuvimbiwa,malaria,tumbo lililofunga choo,kusafisha figo,sumu ya chakula,mapele ya tumboni,kusafisha maziwa ya mama nk. (10)OLMERAA(CATHA EDULIS)- Hutumika kama kiburudisho kwa baadhi ya watu hasa vijana kwa kutafuna,hutibu kikohozi,malaria,maumivu ya mwili,kisonono,kuwashwa sehemu za siri na mafua yasiyopona. (11)OLASESIAI(OSYRIS ABYSSINICA)- Mmea huu hupatikana katika sehemu za miinuko na hutumiwa sana kutibu baadhi ya magonjwa yafuatayo;kisonono,kaswende,matatizo ya figo,kufunga choo,kichocho,perpes,ugumba,maumivu ya hedhi,homa,matatizo ya ini,bawasiri,kuhara damu na amoeba nk. (12)OSITETI(GREWUA BUCIKIR)- Hutibu maumivu ya kifua,kuumwa na nyoka,mafua yasiyopona,maumivu ya tumbo,sumu ya chakula nk. NB(1).Hii ni sehemu ndogo ya miti muhimu na vitu mbalimbali inayo tumika katika tiba ya jamii ya maasai.Tumeona pia jinsi baadhi ya magonjwa ya haraka yanavyotibiwa kwa kupitia wataalam wa tiba katika jami ya maa.Tutaendelea kukuletea mimea mingine na vitu vingine inayotumiwa na wamasai katika kupambana na maradhi mbalimbali katika machapisho yatakayofuata. (2)Madawa haya huandaliwa na kutumiwa kulingana na ugonjwa unaotaka kuutibu na kwa wakati gani. Kwa maoni,ushauri na tiba tuwasiliane kupitia; LMTM CENTRE; BOX.79289,DAR ES SALAAM FAX2EMAIL0736601119, EMAIL:lmtmherbal@rocketmail.com na www.facebook.com/losila maasai
Asanteni kwa kutupa ufahamu wadawa natiba Ila ningependa kujua kama nikiitaji dawa nitapataje asante
JibuFutaMimi ni mzalendo wa Afrika Kusini.Nafurahi kusoma kwa namna na tiba tofauti zaki Afrika.Naomba tu endelee nakinga natiba zetu
JibuFutanamba yenu ya simu
JibuFutaHuwa dawa Kama hizo ukinywa Kuna reaction yeyote hutokea baada ya matumizi? Mfano kuhara au kizunguzungu
JibuFutaJamani dawa ya kimasai ya uzazi ambayo ulitumia unakojoa rangi ya kizambarau inaitwaje
JibuFutaNikitaka kuagiza hizi dawa orijino za kimasai nafanyaje?
JibuFuta