Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 28 Julai 2013

MAASAI TRADITIONAL MEDICINE(TIBA ASILI ZA KIMASAI): MAAJABU YA ASALI KATIKA TIBA YA MARADHI MBALIMBALI...


MAASAI TRADITIONAL MEDICINE(TIBA ASILI ZA KIMASAI): MAAJABU YA ASALI KATIKA TIBA YA MARADHI MBALIMBALI...: Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote.Vitabu vingi vya...

MAAJABU YA ASALI KATIKA TIBA YA MARADHI MBALIMBALI




Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote.Vitabu vingi vya zamani vinazungumzia namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali.Moja ya vitabu hivyo ni KURUANI TUKUFU ambayo Mwenyezi Mungu anaitaja asali kama tiba(AN-NAHL 16:68-69).Sasa hivi kuna makala nyingi zilizo andikwa zikielezea kuhusu uwezo wa asali katika tiba ya magonjwa mbalimbali.Warusi na Wafaransa wanafahamika sana katika kufanya utafiti katika maabara kuhusu uwezo wa asali katika tiba mbali na Kuruani Tukufu kuna baadhi ya vitabu vingine vinavyofahamika kuandikwa na watafiti kuhusu uwezo wa asali katika tiba.Moja kile cha BEES DON'T GET ARTHRITIS CHA FRED MALONE NA BEE IN BALANCE CHA AMBER ROSE.
Leo tuangalie tiba ya asali na mdalasini na namna ya kuitumia kutibu maradhi mbalimbali(asali tunayoizungumzia hapa ni asali safi mbichi.)
BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA KWA ASALI NA MDALASINI NI KAMA IFUATAVYO:
1.UGONJWA WA VIUNGO/MAUMIVU NA UVIMBE(ARTHRITIS)
-Chukua maji kiasi vuguvugu na ongeza mdalasini (unga kijiko cha chai na asali vijiko 2 vya chakula na kuchua sehemu zenye maumivu)
-Vilevile waweza kutengeneza kikombe kimoja cha chai kwa kuweka kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na kuongeza asali vijiko viwili vya chakula na kisha kunywa ikiwa ya moto kutwa mara mbili(asubuhi na jioni)
2.KUKATIKA KWA NYWELE(HAIR LOSS)
-Asali ikichanganywa na mdalasini na mafuta vuguvugu ya olive hutia kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele.
-Tumia mchanganyiko huo vuguvugu kwa kupaka na kusugua kichwani na acha kwa dk 15 kisha uoshe.
3.UKUNGU WA MIGUU(FUNGUS)
-Changanya kijiko cha chakula cha asali na vijiko viwili vya chai vya mdalasini na acha kwa muda wa nusu saa kisha safisha .(rudia hivyo mpaka upone)
4.MAAMBUKIZI KWENYE KIBOFU CHA MKOJO(BLADDER INFECTION)
-Changanya maggy ya maji vuguvugu na vijiko2 vya chai vya mdalasini na kijiko1 cha asali huondoa bakteria kwenye kibofu.
5.MAUMIVU YA JINO(TOOTHACHE)
-Changanya sehemu tano za asali na sehemu moja ya mdalasini na dondoshea kwenye jino linalouma hadi maumivu yatakapotoweka.
6.VIDONDA VITOKANAVYO NA MAGONJWA YA KULALA KWA MUDA MREFU(BED SORES)
-Paka saladi iliyochanganywa asali na mdalasini.Vilevile tumia chai ya roseberry nyekundu kwa kuondoa maumivu makali ya canker sores/bed sores.
7.LEHEMU(CHOLESTRAL)
-Changanya asali safi mbichi vijiko2 vya chakula na unga wa mdalasini vijiko2 vya chakula na kikombe cha chai cha maji ya moto na unywe kutwa mara 3
8.MAFUA(COLDS)
-Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali vuguvgugu na robo kijiko cha unga wa mdalasini kuondoa chafya na kuvimba koo.
9.UGUMBA(INFERTILITY)
-Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi.Kwa wapenzi. wa jinsia zote wanashauriwa kunywa walau vijiko 2 vya chakula kila siku kabla ya muda wa kulala..Mdalasini imetumika muda mrefu katika dawa za kichina na kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa
-Changanya mdalasini na kiasi cha asali na kufanya mgando (paste)na upake kwenye fizi na meno na kuacha inyonywe na kuingia mwilini taratibu na hii ni kwa akina mama wasio na sababu za kimsingi za kuwakosesha kuzaa.
10.MCHAFUKO WA TUMBO(STOMACH UPSET)
-Asali kwa muda mrefu imetambulika kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo na kichefuchefu.Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali pia hupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
11.GESI(ACID)
-Kula asali pamoja na mdalasini kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi(acid)huu ni uchunguzi ulio fanywa na Japan na India
12.UGONJWA WA MOYO(HEART DISEASE)
-Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara kwa kupakaa kama jam wakati wa kula mkate wa ngano wenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko 1 cha chakula cha mchanganyiko huo(asali na mdalasini) kila siku
13.SHINIKIZO LA DAMU(H/B/P)
-Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya upata dozi ya mara kwa mara ya asali iliyochanganywa na mdalasini.
14.KINGA YA MWILI(IMMUNE SYSTEM)
-Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja.Utafiti unaonyesha kuwa hazina  kubwa ya vitamini(virutubisho),madini pamoja na mchanganyiko wa mdalasini na asali iondoayo magonjwa na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za damu husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea(virus)na bakteria.
15.UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME(UHANITHI/IMPOTENCE)
-Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu ya uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji.Asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za mashariki za dunia.Watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali inauwezo wa kupelekea mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo mdalasini.
-Katika Afrika na dunia ya kusini mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza nguvu ya kufanya mapenzi.
16.KUTOKUCHAGULIWA KWA CHAKULA(INDIGESTION)
-Kula vijiko 2 vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo huondoa kiungulia na wataalam wanasema asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa chakula tumboni na mdalasini unaongeza kasi ya kuchaguliwa kwa chakula.
17.FLU(INFLUENZA)
-Tafiti  moja ya Kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa iliyopo katika asali ni dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu vimelea(virus)waletao flu.
18.KUONGEZA UMRI WA KUISHI(LONGEVITY)
-Unaweza kuishi hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali.Kutengeneza kinywaji hiki kitamu weka vijiko 4(vikubwa)vya mdalasini na vijiko 4 vya asali,vikombe 3 vya maji na koroga kwa dk 10 kisha kunywa robo kikombe mara 3 au 4 na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.
19.KUONDOA CHUNUSI(PIMPLES)
-Changanya vijiko 3 vikubwa vya asali na kijiko 1 kikubwa cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.Uwezo wa asali wa kuua bakteria unafanya uso kuwa wa kawaida katika muda wa wiki 2.
20.KUUMWA NA WADUDU(WASHA WASHA WENYE SUMU)
-Changanya asali na mdalasini kisha pakaa moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia tena hadi uvimbe uishe.
21.MADHARA YA NGOZI(INFECTIONS)
-Fanya kama ilivyoandikwa namba ishirini hapo juu.
22.KUPUNGUZA UZITO.
-Waweza kufurahia vyakula vyote unavyovipenda kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri kilichojaa vitu muhimu viwili ambavyo ni asali na mdalasini.
-Unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako.Vilevile wataalam wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyama nyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko 2 vikubwa vya asali na kijiko 1 cha mdalasini.Rudia mchanganyiko huo kabla ya kulala.Wataalam wamethibitisha kuwa inapunguza hamu ya kula na kuleta joto mwilini.
23.SARATANI(CANCER)
-Utafiti uliofanyika huko Australia na Japan umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya magonjwa kwa anaetumia madawa ya kutibu saratani.Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua saratani ya mifupa na utumbo ambao walikuwa wanatumia kila siku dozi ya asali na mdalasini walionyesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wanatumia madawa ya kutibu saratani peke yake.Dr.HIROKI OWATA alisema waliwapa mchanganyiko wa asali na mdalasini kijiko kimoja kutwa mara 3 kwa mwezi 1 na wengine waliendelea kama kawaida.
24.KUONDOA UCHOVU(FATIQUE)
-Uko ushahidi kwamba sukari asilia iliyopo katika asali inauwezo wa kuongeza nishati mwilini.Zikitumika ipasavyo sukari hii inaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.Wataalam wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu kikombe cha maji yaliyonyunyiziwa mdalasini kunywewa masaa mawili baada ya kuamka.Rudia kunywa saa 9 alasiri wakati nishati(nguvu)inapoanza kuisha kufuatia ushauri wa dr.MILSTON ABBOZZA ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.
25.KUVIMBA NYAYO(SOREFEET)
-Changanya asali na mdalasini katika maji vuguvugu na uchue miguu(nyayo)zilizoathirika baada ya siku ndefu ya kazi au baada ya mazoezi marefu.Rudia kila asubuhi na unawe nyayo kwa maji baridi na vaa viatu.
26.HARUFU MBAYA MDOMONI
-Chukua maji ya vuguvugu changanya na asali na mdalasini kisha sukutua kila asubuhi.Katia Asia ya kusini mashariki watu hula kijiko cha asali na mdalasini ili kuondoa harufu mbaya(halitosis).Wataalam wanaamini uwezo wa kuua bakteria uliopo kwenye asali ndio unaopigana na harufu mbaya toka mdomoni.
27.KUPUNGUA KWA USIKIVU(LOSS OF HEARING)
-Dozi za kila siku za asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu kuwa makini kama ilivyogunduliwa na Wagiriki zamani.
-Kutumia mdalasini na asali kutakufanya uonekane kuwa na afya nzuri.
KWA MAONI,MASWALI NA USHAURI TUWASILIANE KUPITIA;
fax2email+255736601119
lmtmherbal.blogspot.com
email;lmtmherbal@rocketmail.com,
NA USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA LMTM HERBAL CENTRE

Ijumaa, 26 Julai 2013

YAFAHAMU MADAWA MBALIMBALI YA MAGONJWA MBALIMBALI YANAYOPATIKANA LMTM CENTRE




LMTM-SUP/+3/PCL
-Ni dawa bora mpya mchanganiko wa mimea ya kuongeza maumbile ya kiume
INAPATIKANA LMTM CENTRE PEKEE

LMTM/MISKI
-Ni mafuta halisi yenye faida nyingi katika tiba mbadala
YANAPATIKANA LMTM CENTRE PEKEE



LMTM/PA19/OLV
-Dawa mchanganyiko wa miti na mafuta ya mzaituni inayotibu ,kuongeza nguvu za kiume,kuongeza maumbile ya kiume,bawasir,kansa ya ngozi,nywele pamoja na magonjwa yote ya ngozi.Dawa hii ni ya kupaka kulingana na ugonjwa unaoutibu na kwa maelekezo ya daktari.
Inapatikana katika ujazo wa cc100
INAPATIKANA LMTM CENTRE TU!










LMTM/ATH/PE8
-Dawa mchanganyiko wa asali na mimea mujarab kwa kutibu Pumu,maumivu ya kifua,kikohozi kisichosikia dawa na inayo ambatana na harufu ya damu kifuani,kifaduro,vidonda mdomoni,vichomi na mzio.
Hutumika kwa kulamba kulingana na ugonjwa unaoutibu kwa maelekezo ya daktari.
Inapatikana katika ujazo wa cc100
INAPATIKANA LMTM CENTRE TU!
     





LMTM/PA19/NAZ
-Ni kati ya madawa bora kabisa na iliyofanyiwa utafiti wa muda mrefu na kituo cha tiba asili chuo kikuu cha muhimbili.Dawa hii ni mchanganyiko wa miti na mafuta inayotibu kwa uhakika magonjwa zaidi ya 60 ya ngozi.Baadhi ya magonjwa hayo ni 1.saratani ya ngozi(inawafaa sana watu wenye ulemavu wa ngozi)
2.fangasi za vidole vya miguu,mikono,mapaja,mba,mapunye na mashilingi.
3.Mkanda wa jeshi
4.Vidonda vibichi na visivyopona kwa namna yoyote ile.
5.Majipu(hutumbuka na kukauka kwa haraka)
6.Chunusi,kucha kung'ooka kutokana na fangasi(huota tena)
7.Muwasho na harara
8.Mgolo/bawasir
9.Kurutubisha nywele na kuzuia kukatika,kunyonyoka na husaidia uzalishaji wa sehemu ya juu ya ngozi(collagen)na kufanya ngozi kunawiri.
10.Kuondoa sumu katika ngozi kwa walioacha mkorogo
11.Kuondoa fangasi sehemu za siri
12.Kuondoa upele wa ndevu baada ya kunyoa
13.Kuondoa mabaka,michirizi,makovu na kufanya ngozi kuwa laini na kung'aa(inafaa sana kwa watu wanaosumbuliwa na magonjwa nyemelezi baada ya maambukizi ya vvu n.k.
Inapatikana katika ujazo wa cc50.
Dawa hii ni ya kupaka kulingana na ugonjwa unaoutibu na kwa maelekezo ya daktari.
INAPATIKANA LMTM CENTRE TU!

LMTM/V11/CH
-Ni dawa ya kuchua mchanganyiko wa mafuta na mimea mujarab kwa kutibu maumivu ya viungo kama;gauts,magoti kuvimba,miguu kuwaka moto,maumivu makali ya mgongo na kiuno,kuteguka n.k.
Hutumika kulingana na ugonjwa kwa maelekezo ya daktari na iko katika ujazo wa cc50.
INAPATIKANA LMTM CENTRE TU!











NB:TAHADHARI DHIDI YA MATAPELI DAWA HIZI ZINAPATIKANA LMTM CENTRE TU NA ZINA ALAMA MAALUM YA SIRI.
KWA USHAURI,MAONI NA MASWALI TUWASILIANE KUPITIA:
fax2email+255736601119,
PIA UNAWEZA KULIKE PAGE YETU NA KUTUANDIKIA KUPITIA:
www.facebook.com/lmtmherbalcentre
lmtmherbal.blogspot.com

Jumamosi, 6 Julai 2013

TUMIA KALENDA KUJUA SIKU NZURI KWA MIMBA KUWEZA KUTUNGWA


Wakina mama wengi wamekuwa hawajui mizunguko yao ya hedhi hivyo kuwawia vigumu kujua siku zao za kukutana na wapenzi wao ili kuweza kushika mimba au kukwepa kupata mimba.Ili kujua siku nzuri ya mimba kutungwa nilazima kwanza ujue siku ya kilele(fruitful/productive/fetal day)kwa maana ya siku ile ambayo huitwa siku ya kumi na nne.Leo napenda kuzungumzia jambo hilo ambalo ni juu ya namna wanawake wanavyoweza kujua (kui-pin point)siku ile ya kilele(i.e fruitful/productive/fertile day),hapa nina maana siku ile wao wanayoiita siku ya 14
Ikumbukwe kuwa wanawake wanatofautiana katika swala zima la urefu wa mzunguko wao wa hedhi (menstral cycle)yaani idadi ya siku kati ya period ya kwanza hadi ile ya pili inayofuatia.Kundi kubwa la wanawake wanaangukia (fall)kwenye kati ya siku 22 hadi 35 .Japo walio kawaida(normal)wana siku 28.Vilevile kuna wengine huwa na mzunguko (menstral cycle)mbili,yaani fupi na ndefu.Hivyo walio na mzunguko (menstral cycle)fupi mathalani wale wenye siku 22,huwa vilevile wana kipindi kifupi sana cha kutokwa na damu.(period),yaani damu inaweza kukatika ndani ya siku mbili tu!Na wale wenye siku 35 au zaidi huwa wana kipindi kirefu sana cha kutokwa na damu (period) ambapo wengine huwachukua hadi siku 8.Hivyo basi kama wewe ni mwanaume inakubidi umuelewe vizuri mwenzi wako juu ya hayo hapo juu ili ikusaidie kujua(kui-pin-point)siku ya mimba(fertile day).
Swali:Je siku ya mimba ni ipi?
Watu wengi na hata baadhi ya wanasayansi wanafikiri siku ya mimba ni ile siku ya 14 baada ya dalili za kwanza za damu ya hedhi(period).Wao huhesabu kuanzia siku ile damu ilipoanza kutoka hadi siku ya 14!Utaratibu huu umethibitisha kushindwa (prove failure).Hii ni kwa sababu wanawake wana mizunguko (menstral cycle)zinazotofautiana kwa urefu hivyo basi jibu sahihi ni kama ifuatavyo hapa chini;
1.Kwanza inabidi ujue kama mwenzi wako ukiwa ni mwanaume ana mzunguko (menstral cycle)ipi fupi au ndefu,au zote mbili?
2.Baada ya kujua urefu wa mzunguko (menstral cycle)ya mwenzi wako chagua/teua(pin point)siku ile ya mwisho halafu uhesabu kurudi nyuma(backwards)siku 15 kuanzia siku ile ya mwisho.Siku hii ya 15 kuanzia mwisho ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote.Ukishafahamu siku ya 15 kutoka siku ya mwisho kutakuwezesha kujua siku ya kupata ujauzito au kukwepa kupata mimba(once you know the 15th day'from the last one,then you can manoeuvre whatever you want to get her pregnant or to avoid pregnancy).
Kwa kutumia utaratibu huo wa kuweka alama utagundua kuwa wanawake wote katika mizunguko yao hutumia njia za zamani ambazo huwafaa tu wale wenye mzunguko wa siku 28(with this new aproach of pin pointing the fertile day,you will find that all women menstral cycles are covered,whereas the old way of counting fits only to women whose menstral cycles are 28 days).
Kwa maelezo hayo sasa nitoe mifano hai ya jinsi ya kutumia kalenda kwa faida ya wakina mama na wapenzi wao ili waweze kutambua siku nzuri kwa mimba kutungwa.Njia hizi huwafaa tu wale wasio na matatizo katika mfumo wao wa uzazi.
1.Kwa mwanamke mwenye mzunguko (menstral cycle)ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavyo;kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za mzunguko (menstration cycle) kama ifuatavyo hapa chini:
1st,2nd,3rd,4th,5th,6th,7th,8th,9th,10th,11th,12th,13th,14th,15th,16th,17th,18th,19th,20th,21st,22nd.Baada ya kuandaa kalenda hii hesabu kuanzia ile siku ya 22 kurudi nyuma mpaka ufike siku ya 15.Utaona kuwa siku ya 15 inaangukia kwenye siku ya 8(8th day)ya kalenda yake.Hivyo siku ya 8(8th day)ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana mzunguko (menstration cycle)ya siku 22.Akumbuke kwamba siku ya kwanza (1st day) ndiyo siku anayoanza kuona siku zake (ku-bleed).
2.Kama mwanamke ana mzunguko(menstration cycle)ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavyo:kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za mzunguko(mensration cycle)kama ifuatavyo:
1st,2nd,3rd,4th,5th,6th,7th,8th,9th,10th,11th,12th,13th,14th15th,16th,17th,18th,19th,20th,21st,22nd23rd,24th,25th,26th,27th,28th.
Baaada ya kumaliza kuandaa kalenda hesabu kuanzia ile siku ya 28(28th day)kurudi nyuma mpaka ufikishe siku ya 15 utaona kuwa siku ya 15 inaangukia kwenye (14th day) ambayo ndiyo itakuwa siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana mzunguko(menstration cycle)ya siku 28.Akumbuke kuwa siku ya kwanza(1st day)ndiyo sku anayo anza kuona siku zake(ku-bleed).
3.Kama mwanamke ana mzunguko(menstration cycle) ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavyo:Kwanza inabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za mzunguko(menstration cycle)kama hapa chini:
1st,2nd,3rd,4th,5th,6th,7th,8th,9th,10th,11th,12th,13th,14th,15th,16th,17th,18th,19th,20th,21st,22nd,23rd,24th,25th,26th,27th,28th,29th,30th,31st,32nd,33rd,34th,35th.
Kisha ahesabu kuanzia siku ya 35 (35th day) kurudi nyuma hadi siku ya 15.Hapa ataona kuwa siku ya 15 itaangukia kwenye siku ya 21 (21st day).Hii inamaana kwamba siku ya 21(21st day) ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana mzunguko(mensration cycle) ya siku 35.Ikumbukwe kwamba siku ya kwanza (1st day) ndiyo siku anayoanza kuona siku zake.
4.Kama mwanamke ana mzunguko usio wa kawaida(abnormal menstration cycle)ya siku 15,kuna uwezekano wa kutopata mimba kabisa kama itakavyooneshwa hapa chini:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za mzunguko (menstration cycle)yake mwenyewe kama kawaida
1st,2nd,3rd,4th,5th,6th,7th,8th,9th,10th,11th,12th,13th,14th,15th.
Kisha ahesabu kuanzia ile siku ya 15 (15th day)kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.Ataona kuwa siku ya 15 inaangukia kwenye siku ya kwanza(1st day).Inamaana kwamba ,siku ya kwanza (1st day)ya mzunguko(menstration cycle)ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote mwenye mzunguko (menstration cycle)ya siku 15.Akumbuke kuwa siku ya kwanza(1st day)ndiyo siku anayoanza kuona siku zake(ku-bleed)na ndiyo siku hiyo hiyo ambayo mwanamke wa kundi hili anaweza kupata mimba.
Hii inamaana kwamba,siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa.Mwanamke wa aina hii anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kuona siku zake(ku-bleed).Kwani ni siku ambayo yai moja linaanza kuharibika na ndiyo siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linakuwa tayari kurutubishwa.Wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au kuhisi ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa kurutubishwa,kwani ute wa mwanamke wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu kwa vile unatoka siku ileile wanapoanza siku zao (ku-bleed).
Pia wanawake wa kundi hili huwa wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu na hukatika ndani ya siku 1 au 2 tu.Jambo la kushangaza ni kwamba, wanawake wengi hawana elimu   (knowledge)ya kutosha juu ya swala hili la siku ya mimba;hasa wale ambao wana mzunguko(menstration cycle)inayobadilika badilika!Wao hushtukia tu wameanza ku -bleed na ndiyo maana hawawezi hata kupanga(ku-plan)kutopata mimba.Hawana ujanja kabisa na ndiyo sababu wengi wanatumia sindano na njia zingine za kuzuia mimba ambazo mwisho wa siku huwaletea matatizo ya uzazi kwani nyingi huziba(block)njia ya uzazi.Nimewaona wengi wenye matatizo ya uzazi uliosababishwa na njia hizi za uzazi wa mpango.Wengine hulazimika kwenda hospitalini kuzibuliwa ili wapate mimba jambo ambalo linahatarisha afya zao kama uzibuaji huo hautafanywa kwa uangalifu wa hali ya juu.
Katika kituo chetu cha LMTM CENTRE tunazo dawa bora kabisa kwa tiba ya njia ya uzazi(lmtm-s32/j)ambayo hutibu matatizo yote ya uzazi pamoja na magonjwa ya njia za uzazi na hayana kemikali.Tunayo pia dawa ya asili ya uzazi wa mpango ambayo ukiitumia kwa kufuata maelekezo itakusaidia kupanga lini upate mimba na lini usipate mimba.
Kwa maelezo haya ni matumaini yetu kuwa sasa mmepata elimu ya lini siku nzuri ya kupata mimba na kuwaondolea mkanganyiko unaowasumbua wanawake wengi.
Kwa wale wenye maswali,au wanaohitaji ushauri,tiba wanaweza kufika katika kituo chetu cha LMTM CENTRE kilichopo ILALA MCHIKICHINI mtaa wa USANGU mkabala na ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
fax2email+255736601119,
lmtmherbal.blogspot.com
NB:Kwa wale wanaopenda kuwasiliana kwa njia ya sms, fungua sehemu ya ujumbe mfupi katika simu yako kisha andika neno lmtm acha nafasi,andika swali lako na kisha utume kwenda namba15522 na swali lako litajibiwa.Waweza pia kutuma maswali na kulike  katika page yetu www.facebook.com/lmtmherbalcentre.
Tunapatikana pia kwenye fb,google,youtube na tweeter
                              USISUMBUKE LMTM IPO KWA AJILI YAKO