Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 7 Desemba 2014

UFAHAMU UGONJWA WA ZINAA WA CHLAMIDIA,DALILI ZAKE ,MADHARA,TIBA NA KINGA


Chlamidia ni aina ya ugonjwa ulio katika kundi la magonjwa ya zinaa(STD) unaosababishwa na bacteria aina ya CHLAMIDIA TRACHOMATIS,ambao wanaweza kuathiri viungo vya uzazi na pia kusababisha ugonjwa wa homa ya mapafu unaojulikana kama TYPICAL PNEUMONIA.Kati ya magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na bakteria,chlamidia ndio ugonjwa unaoongoza kwa maambukizi duniani ambapo nchini Marekani pekee inakisiwa watu milioni 4 huambukizwa ugonjwa huu kila mwaka.
  Inawezekana jina la ugonjwa huo halijazoeleka katika masikio ya wengi na hii huenda ni kutokana na kutokuwepo kwa takwimu za kutosha kuhusiana na suala hilo katika nchi nyingi barani Afrika na hasa katika nchi zetu za Afrika Mashariki,hivyo ni vigumu kujua idadi kamili ya maambukizi.Lakini bila shaka chlamidia ndio ugonjwa wa zinaa unaotokana na bakteria unaoongoza kwa maambukizi mengi zaidi duniani ukifuatiwa na ugonjwa wa gono.Gonjwa hili ambalo huwaathiri wanawake na wanaume pia linaweza kuleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu mfumo wa uzazi wa mwanamke.
  Nchini Marekani pekee mwaka 2011 kesi milioni 1 na nusu ziliripotiwa katika hospitali katika majimbo 50 ya nchi hiyo,katika hali ambayo kesi nyingi hazikuripotiwa kwa kuwa watu wengi wenye kuambukiza ugonjwa huo huwa hawaonyeshi dalili na hivyo hawakwenda hospitali.Kama yalivyo magonjwa mengi ya zinaa,chlamidia pia huwapata zaidi vijana na takwimu zinaonyesha kuwa kati ya wasichana walio na umri wa miaka 14-15 wenye kufanya ngono zembe mara kwa mara,mmoja wao huambukizwa chlamidia.
   Ugonjwa wa chlamidia huweza kuambukizwa kupitia njia za kujamiiana .Mtu yoyote mwenye kufanya ngono zembe na mtu aliye na ugonjwa huo anaweza kuambukizwa.Pia mama mjamzito huweza kuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.Vilevile ugonjwa huo wa zinaa unaweza kuambukizwa kupitia mbwa,vinyesi vya wanyama kama vile ndege walioambukizwa aina ya chlamidia inayopatikana kwa wanyama kwa mfano kuku,bata,kasuku na kadhalika na kusababisha aina ya homa ya mapafu inayojulikana kama PSITTACOSIS ambayo huambatana na homa kali yenye nyuzi joto kati ya celsius 39.4 hadi 41.1.Chlamidia huathiri sehemu tofauti za mwili wa binadamu kama macho,mfumo mzima wa kupumua,sehemu za siri,viungo vya uzazi na tezi(lymph nodes)

     DALILI NA VIASHIRIA VYA UGONJWA WA CHLAMIDIA
 -Asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume wanaopata maambukizi ya ugonjwa huu huwa hawaonywshi dalili zozote za ugonjwa huo ila dalili hutokea baada ya wiki 1-3 baada ya mtu kupata maambukizi.

   DALILI KWA WANAWAKE;
1)Kutokwa na majimaji ya rangi ya njano yanayotoka kwenye utupu,ambayo huwa na harufu kali
2)Kuhisi maumivu wakati wa haja ndogo
3)Kuhisi kama kuwaka moto wakati wa kukojoa
4)Kutokwa na damu katikati ya kipindi cha hedhi yaani baada ya kumaliza mzunguko wa hedhi na kabla ya kuanza mzunguko mwengine
5)Kuhisi maumivu sehemu ya chini ya tumbo
6)Kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana
7)Kutokwa na damu wakati wa kujamiiana na pia kuvimba na kuhisi maumivu kwenye tezi zilizopo sehemu za siri

   DALILI KWA WANAUME;
1.Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
2.Kuhisi kama kuwaka moto wakati wa kukojoa,
3.Kutokwa na njimajikwenye uume ambayo yanaweza kuwa ya ragi nyeupe kama maziwa,kijivu au rangi ya njano.
4.Sehemu ya tundu kwenye uume kuwa nyekundu,kuvimba na kuwasha.
5.Kuhisi maumivu kwenye korodan na tezi zilizopo sehemu za siri ambazo huvimba na huambatana na maumivu.Mara nyingi dalili hizi kwa wanaume huja na kupotea au zinaweza kuonekana tu wakati anapoenda kukojoa asubuhi baada ya kuamka kutoka usingizini.
-Dalili za ugonjwa huu kama umeathiri puru(rectum) kwa wanawake na wanaume ni kama ifuatavyo;
     a)Kuwashwa na kutokwa na damu kwenye puru
     b)Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
     c)Kutokwa na uchafu kama kamasi kwenye puru(rectum)
Iwapo vimelea vya chlamidia vitaathiri macho,wanawake na wanaume huwa na dalili zifuatazo;
 -Uvimbe kwenye macho
 -Macho kuwa mekundu
 -macho kuwasha na hata kutokwa na majimaji machoni.
Baada ya mtu kuhisi dalili hizo tulizozitaja ,hupaswa kwenda hospitalini au katika kituo cha afya ili kupimwa na kuthibitishwa kwamba ana ugonjwa huo ili apatiwe matibabu.
  Vipimo vya uchunguzi vya ugonjwa wa chlamidia ni Urethral swab for culture.Katika kipimo hiki majimaji kutoka kwenye uume au uke huchukuliwa kwa kutumia kijiti chenye pamba au swab maalum ambayo hupelekwa maabara ili kuoteshwa na kuangalia aina ya uoto wa bakteria.Pia huchukuliwa vipimo vya mkojo na pia kipimo cha PCR au Polymerase Chain Reaction,ambacho ni cha kuangalia vinasaba vya bakteria au DNA na hufanywa katika maabara.Baada ya majibu kuonyesha kuwa mgonjwa ameambukizwa vimelea vya ugonjwa huo matibabu hufuata.Chlamidia ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayotibika na ugonjwa huu hutibiwa kwa dawa aina ya antibiotiki zilizopo kwenye makundi ya macrolides,Quinolones na Polyketides ambazo hutolewa chini ya maelekezo ya daktari.

 MADHARA YA UGONJWA WA CHLAMIDIA;
  Kwa wanaume;
-Huathiri korodani na kusababisha mwanaume kukosa uwezo wa kuwa na watoto au kuwa tasa na pia husababisha maambukizi kwenye tezi dume(prostates).
Kwa wanawake;
-Husababisha maambukizi kwenye mirija ya uzazi,mfuko wa uzazi na mayai ya uzazi,kwahivyo kusababisha ugonjwa wa uvimbe katika fupanyonga au Pelvic inflammatory disease(PID).Pia huongeza uwezekano wa wanawake kupata mimba zilizotunga nje ya mfuko wa uzazi ambazo kitaalam huitwa Ectopic pregnancy.Mbali na hilo,mwanamke hupata maumivu sugu kwenye nyonga na ugonjwa wa mifupa arthritis aina ya Reiters syndrome.
-Vilevile chlamidia huweza kusababisha ugumba kwa mwanamke kama hatapata tiba.Si hayo tu,kwa wanawake wajawazito chlamidia husababisha wajifungue kabla ya wakati wake.Pia mtoto anaweza kuzaliwa na maambukizi kwenye masikio,sehemu za siri,macho,mapafu (homa ya mapafu),na kama mtoto hatopatiwa tiba ya haraka ya macho baada ya kuzaliwa basi anaweza kuwa kipofu.
-Dalili za chlamidia kwa watoto wachanga hutokea katika kipindi cha wiki 2 kwenye macho,na iwapo ni homa ya mapafu dalili zake hujitokeza katika kipindi cha wiki 2-miezi 3 baada ya kuzaliwa.

  NJIA ZA KUJIKINGA NA UGONJWA WA CHLAMIDIA;
-Kwa wanawake wajawazito,ni vizuri kuhudhuria klinik mapema wakati wa ujauzito na kupima vipimo mbalimbali ambapo kimojawapo ni cha kuangalia iwapo mama mjamzito ameathirika na ugonjwa huu ili aweze kupatiwa matibabu mapema
-Kwa wenye maambukizi wanashauriwa kuchukua tahadhari ya kutowaambukiza wapenzi wao kwa kufanya ngono salama,pia kuepuka kushika macho kwa kutumia mikono na hata ikiwezekana kuwaepuka wapenzi wao ili kuwalinda na maambukizi.
-kwa  wale ambao wapenzi wao wameambukizwa au wameonyesha dalili za ugonjwa huu,wanashauriwa na wao pia kupata tiba hata kama hawana dalili zozote pia kondom zihusike kwa kila tendo la ndoa.

NB;Njia kuu na sahihi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa ni kuacha au kuepuka kujamiiana au kufanya ngono zembe na zisizo salama.

MOBL;+255776 217 417
fax2email+255 736 601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com

Ijumaa, 3 Oktoba 2014

JE WAJUA KUWA VYOMBO VYA PLASTIKI NI MOJAWAPO YA VYANZO VYA SARATANI ?SOMA HAPA






-   Kwa mujibu wajumuia ya madaktari wa marekani baadhi ya vyanzo vya saratani ni vifaa vya plastiki.Plastiki ikipatajoto inatoa kemikali inayoweza kusababisha aina 52 za saratani.
 -  Ili kupunguza uwezekano huo unashauriwa
(1)Usinywe chai kwa kutumia vikombe vya plastiki
(2)Usile chochote chenye moto kilichofungwa ndani ya mfuko wa plastiki kama chips nk.
(3)Usipashe chakula ndani ya microwave kwa kutumia chombo cha plastiki
(4)Epuka kuchoma mabaki ya plastiki sehemu wanakoishi watu kwani ukivuta moshi huo  ni hatari na pia inaweza kusababisha saratani ya mapafu nk




 NB;  TAFADHALI CHUKUA TAHADHARI
   SHARE KWA KUWAJULISHA WENGINE
     USISAHAU KULIKE PAGE YETU

Jumamosi, 20 Septemba 2014

UFAHAMU UGONJWA WA ZINAA WA TRICHOMONIASIS AMBAO HUWAATHIRI SANA WANAWAKE






Ugonjwa wa Trichomoniasis ni mojawapo ya ugonjwa ulio katika kundi la magonjwa ya zinaa zaidi ya 25 yanayofahamika kwa watu wengi.Ugonjwa huu huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume.Ugonjwa huu wa Trichomoniasis unasababishwa na vimelea vya jamii ya protozoa vinavyojulikana kama Trichomonas Vaginalis ambao huathiri mrija wa kupitishia mkojo(urethra)na tupu ya mwanamke.Trichomoniasis pia hujulikana kwa majina mengine kama Trichomonas Vaginitis au Trich.
Ugonjwa huu huathiri watu milioni 170 kwa mwaka duniani kote .Nchini Marekani pekee ambayo imeendelea katika fani ya tiba watu milioni 8 huambukizwa ugonjwa huu.Ugonjwa huu huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume kutokana na wanaume kutoonyesha dalili zozote wakati wa maambukizi au kutokana na majimaji ya kwenye tezi dume kuwa na madini ya Zinc ambayo huathiri vimelea hivi vya Trichomonas Vaginalis vinavyosababisha ugonjwa huo.

MAAMBUKIZI;
Trichomoniasis huambukizwa kwa njia ya kujamiiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathiriwa na ugonjwa huo.Wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huu ,ili kuufahamu ugonjwa huu vyema kwanza tufafamu nini kinachotokea wakati wa maambukizi(PATHOFIZIOLOJIA)ya ugonjwa huu.
-Umbile la vimelea vya Trichomonas Vaginalis ni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe  kwa upana ingawa wakati mwingine ukubwa unaweza kutofautiana kulingana na mazingira.
-Kuwepo kwa umbile kama mikono kwa nje ya kwenye kimelea hicho inayojulikana kama FLAGELLUM ,husaidia vimelea hivi kuingia kwenye tishu za mrija wa kupitishia mkojo na tupu ya mwanamke na hivyo kuharibu seli aina ya EPITHELIUM na kusababisha vidonda katika tishu hizo hali ambayo husababisha watu walioathirika na ugonjwa huu kuwa kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa VVU na magonjwa mengine ya zinaa.
Trichomoniasis huanza kuonekana kuanzia siku ya 4-28 baada ya mtu kupata maambukizi.Kwa wanawake Trichomoniasis huathiri shingo ya kizazi (cervix),mrija wa mkojo,tupu ya mwanamke,kibofu cha mkojo na tezi zinazojulikana kama BARTHOLIN Glands na Skene Glands.
-Kwa wanaume vimelea hivi hupatikana katika sehemu za siri,sehemu ya nje ya mrija wa kupitishia mkojo(Anterior Urethra),kwenye tezi dume,kwenye mirija ya kuhifadhi na kutoa mbegu za kiume(EPIDIDYMIS) na hata kwenye mbegu zenyewe.

DALILI KWA WANAWAKE;
1.Uchafu unaotoka kwenye tupu ya mwanamke ambao huwa na rangi mchanganyiko ya njano na kijani au rangi kama kijivu na huwa mzito sana.
2.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
3.Kutoka harufu kwenye tupu ya mwanamke
4.Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
5.Shingo ya kizazi kuwa nyekundu hali ambayo hugundulika wakati daktari anamfanyia mgonjwa uchunguzi
6.Kuwashwa sehemu za siri(sio wanawake wote)
7.Maumivu chini ya kitovu kwa baadhi ya wanawake
Ingawa wanawake ndio huonyesha dalili na viashiria vya ugonjwa huu mara nyingine wanaweza kuwa na vimelea hivi hata kwa muda wa miaka kadhaa hata kama vipimo vya uchunguzi havitaonyesha kama wameathirika na vimelea vya ugonjwa huu.

DALILI KWA WANAUME;
Baadhi ya wanaume huwa hawaonyeshi dalili zozote .Baadhi ya dalili zinazoonekana ni;
1.Kuwashwa ndani ya uume
2.Kutokwa na uchafu au majimaji kwenye uume
3.Kuwashwa au kuhisi kichomi baada ya kujisaidia haja ndogo au baada ya kutoa mbegu za kiume
Baada ya mtu kuhisi dalili hizo anashauriwa kwenda hospitali au katika vituo vya afya ili kufanyiwa uchunguzi na vipimo.
VIPIMO;
Trichomoniasis hugundulika kwa kutumia vipimo
1.Kipimo cha darubini ambapo daktari humfanyia mgonjwa uchunguzi kwa kuingiza kifaa maalum katika tupu ya mwanamke na kuchukua kipimo kwa kutumia pamba maalum.Hatua hii hufanywa kitaalam bila kusababisha maumivu kwa mgonjwa na kisha kupelekwa maabara ili kuangalia kama kuna vimelea vya Trichomonas Vaginalis.Kwa kufanya uchunguzi huu daktari anaweza pia kuangalia kama kuta za ndani za tupu ya mwanamke au shingo ya kizazi (cervix) zimeathirika kwa kuwa na vidonda ambavyo ni vyekundu.
2.Kwa mwanaume daktari huchukua kipimo cha uchafu unaotoka sehemu za siri au hupangusa sehemu hizo za siri za mwanaume kwa wale ambao hawatoi uchafu au majimaji yoyote kwa kutumia pamba na kupeleka maabara kufanyia uchunguzi.Pia kipimo kilichochukuliwa na daktari kinaweza kuoteshwa kwenye maabara(culture) na kuangalia kama kuna uoto wa vimelea vya Trichomonas Vaginalis baada ya siku tatu.
3.Kuangalia kiwango cha tindikali(PH)-daktari anaweza kuangalia kiwango cha tindikali kwenye tupu ya mwanamke kwa kutumia karatasi maalum ya kkipimo hiki ijulikanayo kama PH paper,ambapo kiwango kama ameathirika itakuwa PH zaidi ya 5.Kwa kawaida PH ya tupu ya mwanamke inakuwa ni ya tindikali(acidic) kuanzia PH 3.8-4.5 .Magonjwa yanayobadilisha PH ni pamoja na;Trichomoniasis na Bacteria Vaginosis.Mabadiliko hayo humfanya mwanamke kuwa kwenye hatari ya maambukizi tofauti.
4.Kipimo cha damu -hufanywa ili kuchunguza Prostate Specific Antigen(PSA).PSA ni aina ya protin inayozalishwa na seli za tezi dume.Uzalishaji wake huongezeka wakati seli za tezi dume zinapoongezeka kuelekea kuwa kansa inayojulikana kitaalam kama BPH au wakati tezi dume inapopata maambukizi(PROSTITIS),na katika saratani ya tezi dume.Kipimo hiki hufanywa kwa wanaume wanaopata ugonjwa wa Trichomoniasis mara kwa mara au wale wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea na ambao wamepata ugonjwa huu wanapaswa kufanyiwa kipimo hiki angalau mara 1 kwa mwaka.
5.Pap smear -hiki ni kipimo kingine ambapo chembechembe au seli za shingo ya kizazi huchukuliwa na kuchunguzwa kwa kutumia darubini.Kipimo hiki pia hutumiwa katika uchunguzi wa wanawake kujua kama wamepata saratani ya shingo ya kizazi au la.Wanawake wenye zaidi ya miaka 18 au wale wenye upungufu wa kinga ya mwili wanashauriwa kufanya kipimo hiki angalau mara 1 kwa mwaka ili kujua afya zao.
6.Kipimo cha kuangalia maambukizi ya VVU-walioathirika na Trichomoniasis wanapaswa kufanyiwa kipimo cha kuangalia kama wameambukizwa ugonjwa wa HIV.
7.Kipimo cha mkojo na damu-hufanywa kuangalia wingi wa damu,chembechembe tofauti za damu na chembechembe bapa(Platelets)

MATIBABU;
Tiba ya trichomoniasis ni kutumia dawa aina ya Metronidazole au Flagyl.Dawa hii haitumiki kwa wanawake wenye ujauzito chini ya miezi 3 au wanaonyonyesha hivyo basi kabla ya kutumia dawa hii ni vyema ukamuona daktari.Kwa wale walioathirika na ugonjwa huu wa zinaa wanashauriwa kupata tiba pamoja na wenzi wao .Madhara mengine ya dawa ya Metronidazole mbali na madhara kwa wamama wajawazito na wanaonyonyesha ni pamoja na;
1.Mzio(mcharuko wa mwili)yaani allergic reaction
2.Kichefuchefu
3.Kukauka midomo
4.Kuharisha
5.Kuhisi ladha kama ya chuma mdomoni
6.Kushuka kiwango cha chembechembe nyeupe za damu(leukopenia)ambazo hutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na hivyo upungufu wake hufanya mtu awe  katika hatari ya kupata maambukizi tofauti tofauti.Mcharuko wa dawa hii mara nyingi hutokea iwapo masharti ya dawa hayakufatwa vyema au mtu anapokunywa dozi ya dawa zaidi ya alivyoelekezwa na daktari.Ni muhimu kufahamu kuwa unapohisi hali kama hizo katika matibabu yoyote inakupasa kuacha kutumia dawa zinazokudhuru na kumuona daktari haraka.
Katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunazo dawa za mimea zisizi na kemikali zozote na isiyo na madhara kwa wajawazito na wanyonyeshao yenye uwezo wa kutibu siyo Trichomoniasis pekee bali magonjwa yote sugu ya zinaa kama kaswende,kisonono,klamidia,UTI n.k.Dawa hiyo inajulikana kwa jina la LMTM-N7/SUZ.Kwa wale waliofika katika kituo chetu ni mashahidi wa uwezo wa dawa hii kutibu magonjwa yote ya zinaa.
NB;LMTM HERBAL CENTRE ndicho kituo pekee ndani ya Tanzania,Afrika mashariki kati na kusini mwa Afrika chenye uwezo wa kutibu magonjwa ya zinaa sugu na uzazi.

MADHARA YA TRICHOMONIASIS;
1.Ugonjwa huu ni miongoni ya magonjwa ya zinaa ambayo huongeza hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa mengine kama HIV kama tulivyokwisha sema huko nyuma.
2.ugonjwa huu husababisha mwanamke kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo
3.Huwaongezea wanawake hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi
4.Kuongeza hatari kwa wanaume kupata saratani ya tezi dume.

 KITUO CHETU CHA LMTM HERBAL CENTRE KINAPATIKANA ILALA MCHIKICHINI MTAA WA USANGU,
MOBL;+255776 217 417,
fax2email+255 736 601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com

Jumatano, 3 Septemba 2014

UNATAKA KUPUNGUZA UNENE ?SOMA HII HAPA

Hapa nakuletea ratiba ya kupunguza unene/uzito kwa muda wa siku saba kwa kutumia lishe maalum;
  (1)Siku ya kwanza asubuhi kula matunda(lakini katika matunda hayo usile ndizi).Mchana chemsha kabichi,weka chumvi kidogo na nyanya na upate supu kisha kula mchanganyiko huo.Jioni kula tikiti maji na mboga mboga au kabichi uliyotengeneza mchana.
 (2) Siku ya pili kula mboga za majani asubuhi (usile mboga za majani zenye wanga kama karoti).Mchana kula kabichi iliyochemshwa ,tengeneza na kachumbari.katika kabichi weka chumvi,pilipili na mafuta ya olive.Jioni unaweza kula mlo kama wa mchana lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani.
 (3)Siku ya tatu kula mboga za majani na matunda ,unaweza kuongeza kiazi kitamu kimoja .
 (4)Siku ya nne kula ndizi moja na unywe na maziwa ya mtindi wakati wa asubuhi ,Mchana kula kabichi kama ulivyoitengeneza  kwenye siku ya kwanza,usiku rudia mlo wa mchana.
(5)Siku ya tano kula nyanya nn pamoja na samaki au kipande cha kuku asubuhi.Mchana unaweza kula samaki wa kuchemsha kiasi ambaye amechanganywa na nyanya.Wakati wa jioni unaweza kula chakula kama cha mchana.
 (6)Siku ya sita unaweza kula chakula cha protin na mboga za majani.Anza siku kwa kula kachumbari asubuhi.Mchana kula tambi kiasi na kipande kidogo cha samaki.Usiku tengeneza supu ya kabichi.
 (7)Siku ya saba anza kwa matunda na juisi,Mchana kula mboga za majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.
  NB:Unatakiwa kunywa maji angalau glasi nne kila siku.Dayati hii ni kwa siku saba tu.

Jumapili, 6 Julai 2014

ZIJUE DALILI,TIBA NA UCHUNGUZI WA TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO







      TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO(KIDNEY STONES)
-Figo ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu,hufanya kazi ya kuchuja damu huku ikiondoa sumu zote za mwili,figo hufanya kazi ya kurekebisha kiasi cha maji mwilini(electrolyte level).
kabla damu haijapita katika figo,huwa imebeba maji na takataka nyingi sana(urea),lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu lakini,masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwa ni pamoja na kiwango cha maji kilichozidi hupitishwa kwenye mirija miwili(ureters)kuelekea kwenye kibofu(urinary bladder) na kishas kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo(urethra)
Mkusanyiko wa kemikali hizi(chemical crystals),wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga,kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadi wengine hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo katika figo yenyewe(neprone) au kwenye mirija ya kupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu(ureteter),hapo ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kusikia maumivu makali.


     DALILI ZA UWEPO WA MAWE KWENYE FIGO;
  Mtu mwenye mawe kwenye figo huonyesha dalili zifuatazo;
a.Maumivu ya mgongo na kiuno
b.Mkojo kutoka ukiwa na rangi ya damu
c.Kutokwa na jasho wakati wa usiku
d.Kupatwa na homa kali kwa wakati flani ikiambatana na kutetemeka mwili
e.Kuhisi kichefuchefu na kutapika
f.Mkojo kuwa na harufu kali
g.Maumivu makali sehemu za mbavu
h.Miguu kujaa maji/kuvimba.
i.Maumivu ya tumbo chini ya kitovu upande wa kushoto au kulia kutegemea ni figo ya upande gani iliyoathirika.
j.Maumivu makali unapogusa upande wa figo iliyoathirika.

   KISABABISHI CHA MAWE KATIKA FIGO(KIDNEY STONES);
1.Matumizi ya baadhi ya dawa husababisha mtu kupata mawe katika figo pindi anapozitumia kila mara.Dawa hizo ni kama vile za kutibu kansa na HIV,antibiotic kama ciprofloxacin,cefrtriaxone na madawa yenye sulphur kama metacalphin nk.
2.Utumiaji wa vyakula vyenye kuongeza vitamin A na D,ambavyo huongeza kwa kiasi kikubwa madini joto mwilini
3.Kuishi kwenye mazingira ya joto sana bila kupata maji ya kutosha husababisha kiasi cha chemical kuongezeka katika figo na kusababisha zigandamane na kutengeneza mawe ndani ya figo.
4.Maambukizi ya magonjwa ya figo kama renal tubula acidocis ctc,huongeza hatari ya kupata tatizo hilo.
5.Kurithi kutoka kwa wazazi (wanakuwa na homoni ziitwazo antiduretic hormone)zisizoweza kufanya kazi ya kuchuja damu kikamilifu na mwishowe hutengeneza mawe katika figo.
6.Utumiaji wa vyakula vyenye protin zinazotokana na wanyama na chumvi nyingi(huongeza hatari ya kupata tatizo hili)
7.Unene kupita kiasi

   JINSI YA KUGUNDUA TATIZO;
1.Mgonjwa kufanyiwa X-Ray au scan ili kujua kama ana mawe katika figo.
2.Vipimo vya damu(blood test)
3.Vipimo vya mkojo(urenarlulisis)

    TIBA YA TATIZO;
-Ikiwa mgonjwa baada ya uchunguzi atagundulika kuwa na tatizo hili hupewa mojawapo ya tiba zifuatazo:
1.Extracorporeal shock wave lithotripys(eswl)-Hii ni mionzi inayoelekezwa katika figo ili kuyeyusha mawe (chemical au sumu zilizogandamana)ambazo huvunjwavunjwa na hii mionzi kisha mgonjwa hukojoa vipandevipande.
2.Percutaneous nephrolithotomy(PCNL)-Hiki ni kifaa chenye mwanga na kamera ambacho huingizwa kwenye kokwa za figo (nephrone)ambayo huvunjavunja mawe katika figo.
3.Ureteroscopy-Kifaa hiki huingizwa kwenye mirija ya kupitishia mkojo(urether)kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu ili kuondoa mawe yaliyokwama kwenye mirija na kuzuia mkojo kutoka.
4.Stone removal-Hapa mgonjwa hufanyiwa operesheni ya kuondoa mawe moja kwa moja.

- Kama tulivyoona tiba hizi zina madhara na ni ghali.Hivyo basi kabla hujaenda katika tiba hizi zenye madhara makubwa ni muhimu kutumia tiba mbadala na tiba asili ili kuepuka madhara mengine.
Katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunayo dawa asili zenye uwezo mkubwa wa kutibu tatizo hili la mawe kwenye figo bila madhara yoyote.Aina hizi za dawa hufanya kazi za kuyeyusha kemikali na mafuta yaliyogandamana katika figo na kuzibua mirija iliyojiziba ili kuruhusu mtiririko wa mkojo kuwa kama unavyotakiwa.
Baadhi ya madawa tuliyonayo ni;
a.LMTM-F5/AFH2
b.LMTM/S32/J
Dawa hizi mbali na kutibu matatizo ya mawe katika figo zinauwezo wa;
1. kutibu saratani ya kizazi,kusafisha mirija ya uzazi na kutoa maji katika mirija hiyo
2.Uvimbe wowote ndani ya mwili
3.Kurekebisha hedhi iliyovurugika kwa akina mama(hasa waliowahi kutumia dawa za uzazi wa mpango)
4.Saratani ya ini na kibofu cha mkojo
5.Kusafisha mfumo mzima wa njia ya mkojo
6.Huwasaidia akina mama wenye kasoro mbalimbali katika via vya uzazi,waotafuta uzazi kupata watoto

Ijumaa, 30 Mei 2014

IMARISHA UWEZO WA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA KULA MATUNDA NA MBOGAMBOGA


Ili mtu awe na afya bora na hatimaye aweze kumudu tendo la ndoa ni lazima mwili wake upate virutubisho kama vile;
a.wanga
b.mafuta
c.protini
d.vitamin na madini kwa kiwango sahihi kutoka katika chakula
   Moja ya sababu ya mtu kupoteza hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa ni msongo mzito wa mawazo.Msongo wa mawazo unaufanya mwili kushindwa kuzalisha kiwango tosha la vichocheo ya kufanya tendo la ndoa.Kwahiyo hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa inapungua.Sababu nyingine inayosababisha mtu kukosa hamu na nguvu ya tendo la ndoa ni vyakula.
   Ili mwanaume aweze kuwa na hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa lazma tezi dume lake liwe na afya bora.Madini ya zinki ambayo hupatikana kwa urahisi katika maharage,vitunguu,matango,karoti,spinachi,kabichi na matunda mbalimbali husaidia kufanya tezi dume kuwa imara.
    Baadhi ya vitamini kama;
   1.vitamini A inayopatikana kwa wingi katika spinachi,karoti,matikiti na maembe.Inaweza kubadili lehemu kuwa kichocheo madhubuti katika kufanya tendo la ndoa.
   2.vitamini B inayopatikana kwa wingi katika viazi,ndizi na maboga husaidia kutengeneza vichocheo katika tendo la ndoa
   3.vitamini E inayopatikana kwa wingi katika vyakula vya asili kama vile pumba za ngano,majani machanga ya mtama,ufuta na matunda ya aina mbalimbali kwa kiasi kikubwa inaimarisha maisha ya mu katika kufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu.Upungufu wa vitamini E mwilini unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume mwilini.
   Ulaji wa ndizi unasaidia kupunguza msongo wa mawazo kwa sababu ya kuwa na madini ya potassium kwa wingi ambayo husababisha mwili kuongezeka kwa wingi vichocheo vya tendo la ndoa.Kwa mwanaume kazi moja ya tezi za dume ni kutoa majimaji yaliyochanganyika na mbegu za kiume wakati wa kufanyika tendo la ndoa.
   Baadhi ya watu hutumia dawa au hormonies ili kuongeza nguvu ya kufanya tendo la ndoa.Matumizi ya aina zozote za dawa yana changamoto zake,ikiwemo madhara ya kiafya na kiuchumi hivyo watu wanashauriwa kujenga tabia ya ulaji bora na kufanya mazoezi ili kuweza kukabili tatizo hilo.Ulaji wa kudumu wa matunda na mbogamboga au juisi za asili unaimarisha afya na kumpa mtu nguvu na hamu ya kufanya tendo la ndoa. Hata hivyo ieleweke kuwa kuna baadhi ya watu kama vile wasiozalisha vichocheo,tiba yao sio chakula pekee bali ni lazma waende hospitalini kufanyiwa vipimo na kup[atiwa tiba sahihi kulingana na tatizo walilonalo.
  Tahadhari:matumizi holela ya madawa yanaweza kuleta madhara katika figo au kudhoofisha kabisa nguvu ya kufanya tendo la ndoa.

KWA MAONI,USHAURI TUWASILIANE KUPITIA;
MOBL:0776 217417,
fax2email +255736661119.
email;lmtmherbal@rocketmail.com

Jumapili, 16 Februari 2014

MISKI NI DAWA MUJARABU KWA WANAOWAHI WAKATI WA TENDO LA NDOA NA MENGINEYO








-Miski ni mfalme wa aina zote za mafuta mazuri na ni matukufu zaidi.Ni mafuta ambayo hupigiwa mfano mzuri kwa kufadhilishwa kuliko mafuta mengine.
SIFA ZA MISKI;
-Miski hali yake ina joto na inauyabisi katika daraja la pili.
-Ina harufu na ladha yake ni tofauti na mafuta mazuri mengine.Ukitaka kutofautisha miski feki na halisi,ni kwamba katika tiba za kimwili miski feki haiwezi kutibu maradhi maduka mengi yanauza miski feki ambazo sio zile zilizokusudiwa kutuka katika tiba.Ikiwa unahaja ya tiba hakikisha umeata miski asilia.

TIBA ZA MISKI;
1.Huchangamsha na kusafisha mishipa ya fahamu na ubongo.
2.Huongeza hisia,ashiki na ladha za tendo la ndoa kwasababu huzidisha matamanio na joto mwilini
3.Huwasaidia wanawake wasiokuwa na ashki(hisia) na ladha wakati wa tendo la ndoa.Tunayo pia dawa ya ziada ya kuongeza nguvu,hisia na hamu yatendo la ndoa kwa wanawake dawa hii ulizia katika kituo chetu cha lmtm herbal centre.
4.Huwasaidia wanaume wanaowahi kumaliza tendo la ndoa kabla ya mke.Namna ya kutumia wasiliana na wataalam wetu  waliopo katika kituo chetu kilichopo ilaa cha lmtm herbal centre.Kwa ziada ya haya tunazo dawa zingine za kuongeza nguvu za kiume ambazo ni za kunywa na za kuchua kwa kuimarisha na kuipa nguvu mishipa ya dhakal.Dawa hii pia ni mujarab kwa kuchelewesha kuwahi kutoa manii haraka
5.Husaidia wanawake waliomaliza siku zao za hedhi kuondoa harufu mbaya.Pia hupunguza umajimaji na harufu mbaya itokayo ukeni
6.Hukazanisha utupu wa mwanamke na kufanya sehemu hiyo kuwa ndogo

NB:Kufahamu namna ya kutumia miski kama dawa kutibu magonjwa yaliyotajwa hapo juu pamoja na wapi pa kupata miski halisi wasiliana na kituo chetu cha lmtm herbal centre kilichopo ilala mchikichini mtaa wa usangu jijini dar es salaam;
    Simu no;+255776217417,
               fax2email+255736601119
              email;lmtmherbal@rocketmail.com
USIACHE KULIKE PAGE YETU YA LMTM HERBAL CENTRE

Jumanne, 11 Februari 2014

FAIDA ZA PILIPILI KICHAA KIAFYA NA KITIBA

Pilipili kichaa inaweza kustawi sehemu mbalimbali na inahitaji siku 100 za ukuwaji.Hustawi zaidi kwenye mazingira ya joto na unyevunyevu.Mmea huu hukua kufikia urefu wa futi mbili hadi nne.Ina wingi wa vitamini A,pia ina vitamini B,vitamini E,vitamini C,Riboflavin,Potassium na Manganese.
- Jamii nyingi hususa Marekani na bara la Asia wana historia ya kutumia pilipili kichaa kama tiba.Ni dawa yenye nguvu sana na matumizi mengi,hutumika sana kwa kusafisha damu na kutoa sumu mwilini,pia hutumika kusisimua mzunguko wa damu na kuweka sawa uwiano wa tindikali(acid)mwilini.Pilipili kichaa imetumika kwa maradhi tofautitofauti ikiwemo moyo,gauts,kupooza,homa,kikohozi,tonsilatis,kichefuchefu na hemorhoids kwa miaka mingi huko Asia na mashariki ya mbali.

MAAJABU YA PILIPILI KICHAA;
1.Kutibu kidonda-Hii inaweza kuwa ni ajabu kwa walio wengi lakini ni tiba liyothibitishwa na imekuwa ikitumika miaka kadhaa iliyopita katika nchi mbalimbali.Sio tu kuzuia kutokwa na damu katika kidonda cha kujikata kama ilivyozoea kutumiwa na wengi huko majumbani kwa miaka mingi bali pia huzuia fangasi na bakteria kuingia katika uwazi wa kidonda hicho hutumika pia kuondoa sumu mwilini 2.Hufanya mwili kuweza kutumia vyema virutubisho vipatikanavyo kutokana na chakula3.Husaidia uyeyushaji wa mafuta mwilini/Kuchoma mafuta4.Pilipili ina antioxidants muhimu kama beta carotene,ina wingi wa vitamini A,C na K hebu tuziangalie vitamini hizo: a.Vitamini A husaidia kuweka sawa kinga ya mwili pia hutukinga na kansa na magonjwa ya moyob.Kazi ya vitamini C-ni kuzuia strock,magonjwa ya moyo,macho na kansa mbalimbali.Miili ya binadamu haiwezi kujitengenezea vitamini C,hivyo basi tunaweza kupata vitamini C kupitia chakula.c.Vitamini K-Husaidia katika ukuwaji wa mifupa,pia ni muhimu katika mzunguko wa damu.Pilipili zote huwa na Capsaicin ambayo kazi yake ni kupunguza maumivu,kuzuia kansa na magonjwa ya moyo.5.Inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu6.Huwasaidia watu wanene(over weight) au wanaougua ugonjwa wa kisukari.Hii ni kwa mujibu wa watafiti katika chuo kikuu cha Tasmania uliochapishwa katika American Joarnal of Clinical Neutition mwezi julai 2006.7.Inasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa INSULIN kwa 60% baada ya kula chakula8.Husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa RHEMATOID na ARTHRITIS kupata nafuu9.Husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja mwilini10.Husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua na kukufanya upumue kwa urahisi.11.Husaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya utumbo.
12.Husaidia kuongezeka kiwango cha METABOLIC ambayo husaidia kuchoma mafuta

13.Husaidia kuongezeka kwa kiwango cha METABOLIC kwa 23% ndani ya masaa matatu.14.Husaidia kupunguza cholestro na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu. KWA USHAURI,MASWALI;TEMBELEA PAGE YETU YA LMTM HERBAL CENTRE AU KUPITIA EMAIL; lmtmherbal@rocketmail.com,fax2email+255736601119NB:USISAHAU KULIKE PAGE YA LMTM HERBAL CENTRE.

Alhamisi, 30 Januari 2014

LMTM TIME JANUARY 25(IJUE TOFAUTI YA VVU NA UKIMWI)





FAIDA ZA ALIZETI KATIKA TIBA MBADALA






Wengi tunafahamu kuwa mbegu za alizeti hutoa mafuta ya kupikia lakini umuhimu wa zao hili hauishii hapo bali pia ni tiba ya matatizo na magonjwa mbalimbali ya binadamu.Alizeti inauwezo wa kusaidia;
1.Tatizo la kufunga choo
2.Kurudisha mwili katika afya yake ya kawaida
3.Inaimarisha misuli hasa kwa wazee
4.Kuumwa miguu
5.Malaria-chuma majani kilo moja,maji lita mbili na nusu,chemsha na kisha loweka kwa dakika 15.Tumia kutwa mara tatu.
6.Shinikizo la damu la juu na chini
7.TB
8.Vidonda vya tumbo
9.Kansa ya damu n.k
-Kulingana na wataalam na watafiti wa tiba mbadala alizeti imetumika kwa miaka mingi katika tiba ikichanganywa na madawa,miti kutibu maradhi mbalimbali.Hivyo basi mbali na mafuta yatokanayo na mbegu za alizeti kutumika kama kiungo ni dawa yenye uwezo mkubwa ikichanganywa na mimea mingine kutibu maradhi sugu mbalimbali.

-Kwa matumizi na tiba wasiliana nasi kupitia;
-email lmtmherbal@rocketmail.com,na fax2email+255736601119
-Pia usisahau kulike page yetu ya lmtm herbal centre

Jumatatu, 13 Januari 2014

IJUE HABATSOUDA NA UMUHIMU WAKE KATIKA TIBA YA MARADHI MBALIMBALI

Habatsouda ni punje nyeusi yenye umbo mthili ya ufuta ndani yake imebeba dwa yenye faida kubwa.Huko misri huitwa habbatul-barakh(punje ya baraka),vilevile huitwa kamun aswad.Huko Iran huitwa shaniuz ama huku Afrika Mashariki hujulikana kwa majina ya habalsoda,yai jeusi na zenyeu.
      Habalsoda ina viini vyenye adhari nzuri,ladha nzuri na faida kubwa.Ndani yake kuna fosfeti,chuma,fosforasi,kabohaidreti na mafuta 28%.Vilevile ina viua sumu(antibaotik)vyenye kuangamiza virusi,viini vya maradhi na vijidudu.Pia ina karotini inayozuia saratani,homoni inayoongeza nguvu za kiume na nishati mwilini.Pia inasafisha mkojo na kutoa safura.Ina vimeng'enyo (enzymes) na kizima-asidi(ant asid),pia ina viini vyenye kuburudisha na kuchangamsha kwa wakati mmoja.
     Ndani yake kuna faida na manufaa yanayomfanya mtu kutotumia madawa ya famasi.

                       MAGONJWA YANAYOTIBIWA KWA KUTUMIA HABALSODA KWA USHAURI WA WATAALAM WA TIBA MBADALA NI HAYA YAFUATAYO;
1.KUNYONYOKA NYWELE
   Kanda uga wa habalsoda katika juisi ya kachiri(komoni/rocket)pamoja na kijiko cha siki nyepesi na kikombe cha mafuta ya zaituni kisha sugua kichwa kwa mafuta hayo.(kwa maelezo zaidi wasiliana na daktari)
2.MAUMIVU YA KICHWA
   Chukua unga wa habalsoda,karafuu iliyosagwa nusu ya kiwango cha habalsoda na anisuni,changanya pamoja,chukua kiasi cha kijiko cha chai na ule na maziwa ya mgando.Waweza pia kusugua mahali panapouma kwa mafuta ya habalsoda.
3.UKOSEFU WA USINGIZI
   Chukua kijiko cha habalsoda changanya na glasi ya maziwa ya moto yaliyochanganywa na asali kunywa yakiwa ya vuguvugu.
4.CHAWA NA MAYAI YAKE
   Chukua unga wa habalsoda ukande kwenye siki mpaka uwe kama marhamu alafu jipake kichwani baada ya kunyoa nywele au sugua marhamu kwenye mashine ya nywele alafu kaa katika jua kwa muda wa robo saa.Usioshe kichwa mpaka baada ya masaa matano.
5.KISUNZI NA MAUMIVU YA SIKIO
   Tia tone la mafuta ya habalsoda katika sikio na kunywa na sugua sehemu za panda uso na nyuma ya kichwa kumaliza kisunzi.
6.UPAA NA MABAKA
   Kijiko cha unga wa habalsoda,siki kiasi cha kikombe kimoja mafuta ya kitunguu thaumu kikombe kidogo changanya na ujipake baada ya kunyoa nywele.
7.MALENGELENGE YA NEVA KATIKA NGOZI
   Jipake sehemu ya malengelenge mafuta ya habalsoda mara tatu kwa siku
8.MARADHI YA WANAWAKE NA UZAZI
   Dawa kubwa ya kurahisisha kuzaa ni habalsoda iliyochemshwa na kuchanganywa na asali.Tumia pia mafuta ya habalsoda katika kinywaji cha moto kwa maradhi yote ya wanawake.
9.MENO NA MAUMIVU YA FINDO NA KOO
   Chemsha habalsoda na utumie kwa kusukutua,kugogomoa husaidia sana maradhi yote ya mdomo na koo.Vivyo hivyo bugia kijiko cha habalsoda kwa kumeza na maji yenye vuguvugu kila siku na kupaka mafuta yake sehemu ya ndani ya koo.
10.MARADHI YA TEZI
   Chukua unga wa habalsoda na kanda kwa asali na sega la nyuki kila siku
11.CHUNUSI
   Chukua unga wa habalsoda ukande katika mafuta ya simsim pamoja na kijiko cha unga wa ngano.Jipake usoni jioni na asubuhi halafu osha kwa maji ya vuguvugu na sabuni na uwe unakunywa mafuta ya habalsida kwenye vinywaji vya moto.
12.MARADHI YA NGOZI
   Mafuta ya habalsoda,mafuta ya waridi/marashi jabali na unga wa ngano asili.Changanya kwa viwango sawa alafu ukande vizuri.Osha sehemu iliyoathirika kwa siki nyepesi alafu kaa kwenye jua na baadae ujipake dawa hiyo kila siku.Tahadhari epuka kula vyakula vinavyochochea hisia(aleji) mfano;samaki,maembe,mayai na mfano wake.
13.SUGU/CHUNJUA/WART
   Chukua unga wa habalsoda ukande katika siki nzito na sugua kwa kitambaa cha sufi au katani mahali penye sugu.
14.KUNG'ARISHA USO NA KUREMBESHA
   Kanda unga wa habalsoda katika mafuta ya zaituni kisha jipake usoni.
15.KUUNGANISHA MVUNJIKO HARAKA
   Supu ya adesi/dengu,kitunguu maji pamoja na yai la kuchemsha na kijiko kikubwa cha unga wa habalsoda changanya na supu hiyo kula siku baada ya siku.Sugua pia sehemu karibu na mvunjiko kwa mafuta ya habalsoda yenye vuguvugu.
16.MVILIO WA DAMU
   Chemsha kiganja kimoja cha habalsoda kisha chua sehemu iliyovilia damu na maji hayo kwa muda wa robo saa au zaidi.Baada ya hapo jipake mafuta ya habalsoda na usifunge
17.BARIDI YABISI(RHEUMATISM)
   Chua kwa mafuta ya habalsoda ya moto halafu kunywa mafuta ya habalsoda yaliyochemshwa na kuchanganywa na asali.
18.KISUKARI
   Unga wa habalsoda kikombe kimoja,manemane iliyosagwa kiasi cha kijiko kikubwa,habbarrshad nusu kikombe,koma manga iliyosagwa kiasi cha kikombe kimoja mzizi wa kabichi iliyosagwa baada ya kukaushwa kiasi cha kikombe kimoja na kijiko kidogo cha mvuje kula kiasi cha kijiko kimoja na mziwa ya mgando ili iwe rahisi kumeza.
19.SHINIKIZO LA DAMU(HIGH BLOOD PRESHA)
   Kila unywapo kinywaji cha moto tia matone machache ya habalsoda
20.UVIMBE WA FIGO
   Tengeneza kibandiko cha unga wa habalsoda iliyochanganywa katika mafuta ya zaituni na ubandike sehemu yenye maumivu ya figo pamoja na kubugia fundo la mafuta ya habalsoda kila siku.
21.KUVUNJA VIJIWE TUMBONI
   Chukua kikombe cha habalsoda kisha ukande katika asali na kitunguu thaumu na ule kabla ya chakula kila siku.
22.KUKOJOA KWA MAUMIVU
   Paka mafuta ya vuguvugu ya habalsoda kwenye kinena  kabla ya kulala pamoja na kunywa kikombe cha mafuta hayo kilichochanganywa na asali
23.KUKOJOA BILA KUKUSUDIA
   Habalsoda,maganda ya mayai yaliyosafishwa na kuokwa na kusagwa yatie kwenye maziwa na kunywa kiasi cha kikombe kimoja kila siku
24.JONGO(EDEMA)
   Weka kibandiko cha unga wa habalsoda kilicho kandwa katika siki juu ya kitovu na kula kijiko cha habalsoda asubuhi na jioni.
25.KIFUKO CHA NYONGO NA VIJIWE VYAKE
   Habalsoda kiasi cha kijiko kimoja,manemane robo kijiko na asali kikombe kimoja kula kila asubuhi na jioni.
26.WENGU
   Weka kibandiko cha habalsoda iliyokandwa na mafuta ya zaituni weka kibandiko katika ubavu wa kushoto kila jioni.Na wakati huo kula uwatu uliochanganywa na asali na mafuta ya habalsoda kidogo.
27.MARADHI YOTE YA KIFUA NA BARIDI.
   Mafuta ya habalsoda kijiko kikubwa itie kwenye maji yaliyochemka na kufuka moshi kisha uanze kuuvuta ule moshi huku umefunika kichwa ili ule moshi usiende upande mwingine fanya hivyo kila siku kabla ya kulala pamoja na kunya zaahatari iliyochanganywa na uga wa habalsoda
28.MOYO NA MZUNGUKO WA DAMU
   Kula asali iliyochanganywa na habalsoda kila siku.
29.MCHANGO(MSOKOTO WA TUMBO)
   Chemsha anisuni,binzari nyembamba(kamuni)na naanaa kwa kipimo sawa na tia asali kidogo tia matone ya habalsoda na kunywa kikiwa na uvuguvugu pamoja na kupaka mafuta ya habalsoda mahali panaposokota
30.KUHARA
   Juisi ya chirichiri iliyochanganya na unga wa habalsoda kijiko komoja kikubwa kunywa kutwa mara tatu.
32.UZIWI
   Chemsha habalsoda pamoja na karafuu kunywa bila kuongeza kitu
33.GESI NA MAUMIVU
   Kula unga wa habalsoda kijiko kimoja kabla ya kula kisha fuatisha glasi ya maji ya moto iliyotiwa asali ya muwa kiasi cha vijiko vitatu
34.ASIDI
   Habalsoda,asali na maziwa ya moto kumaliza asidi
35.UVIMBE WA TUMBO
   Unga wa habalsoda kijiko kimoja na kijiko cha urkusus changanya na juisi ya peas iliyochanganywa na kokwa zake
36.MARADHI YA MACHO
   Paka habalsoda sehemu za kandokando na macho na kope kabla ya kulala na kunywa matone kadhaa ya mafuta ya habalsoda katika kinywaji chochote cha moto au katika juisi ya karoti..
37.AMOEBA(AMIBA)
   Unga wa habalsoda kijiko kimoja,kitunguu thaumu kilichosagwa changanya katika kikombe cha juisi ya tomato iliyotiwa chumvi kidogo,kunywa kila siku kabla ya kula chakula.
38.KICHOCHO
   Kula habalsoda kijiko kimoja kila asubuhi na jioni na kujipaka mafuta yake
39.KUTOA WADUDU TUMBONI
   Kijiko kimoja cha unga wa habalsoda,punje tatu za kitunguu thaumu,kijiko kimoja cha mafuta ya zeti,pilipili manga kidogo na punje kumi za boga kisha fuatisha mafuta ya nyonyo/mbarika/mbono
40.UTASA
   Unga wa habalsoda,unga wa uwatu na mbegu ya figili kwa kipimo sawa kula kijiko kimoja asubuhi na jioni ikiwa imekorogwa katika nusu kikombe cha asali na baadae fuatisha na kikombe kikubwa cha maziwa.
41.TEZI KIBOFU(PROSTATE GLAND)
   Jipake habalsoda chini ya mgongo na chini ya korodani na kusugua kwa mzunguko na kula unga wa habalsoda kijiko kimoja iliyochanganywa na kijiko kidogo cha manemane katika nusu glasi ya asali iliyotiwa katika maji yenye vuguvugu
42.PUMU
   Nusa moshi wa mafuta ya habaloda na kula unga wake kabla ya kula chakula kila siku na jipake mafuta yake kifuani na kooni kabla ya kulala
43.KIDONDA(VIDONDA TUMBO)
   Mafuta ya habalsoda,kikombe cha asali na kijiko cha maganda ya koma manga yaliyokaushwa na kusagwa kula kabla ya chakula na baadae kunywa glasi ya maziwa yasiyotiwa chochote
44.SARATANI(CANCER)
   Paka mafuta ya habalsoda pamoja na kula unga wake kila umalizapo kula katika juisi ya karoti
45.NGUVU ZA KIUME
   Habalsoda kijiko kimoja changanya ndani ya mayai saba ya kienyeji.Hatakama una miaka120 utapata nguvu.

   NB;MADAWA HAYA HUPATIKANA LMTM HERBAL  CENTRE PEKEE
         ;USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA LMTM HERBAL CENTRE

Jumapili, 5 Januari 2014