Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 30 Mei 2014

IMARISHA UWEZO WA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA KULA MATUNDA NA MBOGAMBOGA


Ili mtu awe na afya bora na hatimaye aweze kumudu tendo la ndoa ni lazima mwili wake upate virutubisho kama vile;
a.wanga
b.mafuta
c.protini
d.vitamin na madini kwa kiwango sahihi kutoka katika chakula
   Moja ya sababu ya mtu kupoteza hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa ni msongo mzito wa mawazo.Msongo wa mawazo unaufanya mwili kushindwa kuzalisha kiwango tosha la vichocheo ya kufanya tendo la ndoa.Kwahiyo hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa inapungua.Sababu nyingine inayosababisha mtu kukosa hamu na nguvu ya tendo la ndoa ni vyakula.
   Ili mwanaume aweze kuwa na hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa lazma tezi dume lake liwe na afya bora.Madini ya zinki ambayo hupatikana kwa urahisi katika maharage,vitunguu,matango,karoti,spinachi,kabichi na matunda mbalimbali husaidia kufanya tezi dume kuwa imara.
    Baadhi ya vitamini kama;
   1.vitamini A inayopatikana kwa wingi katika spinachi,karoti,matikiti na maembe.Inaweza kubadili lehemu kuwa kichocheo madhubuti katika kufanya tendo la ndoa.
   2.vitamini B inayopatikana kwa wingi katika viazi,ndizi na maboga husaidia kutengeneza vichocheo katika tendo la ndoa
   3.vitamini E inayopatikana kwa wingi katika vyakula vya asili kama vile pumba za ngano,majani machanga ya mtama,ufuta na matunda ya aina mbalimbali kwa kiasi kikubwa inaimarisha maisha ya mu katika kufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu.Upungufu wa vitamini E mwilini unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume mwilini.
   Ulaji wa ndizi unasaidia kupunguza msongo wa mawazo kwa sababu ya kuwa na madini ya potassium kwa wingi ambayo husababisha mwili kuongezeka kwa wingi vichocheo vya tendo la ndoa.Kwa mwanaume kazi moja ya tezi za dume ni kutoa majimaji yaliyochanganyika na mbegu za kiume wakati wa kufanyika tendo la ndoa.
   Baadhi ya watu hutumia dawa au hormonies ili kuongeza nguvu ya kufanya tendo la ndoa.Matumizi ya aina zozote za dawa yana changamoto zake,ikiwemo madhara ya kiafya na kiuchumi hivyo watu wanashauriwa kujenga tabia ya ulaji bora na kufanya mazoezi ili kuweza kukabili tatizo hilo.Ulaji wa kudumu wa matunda na mbogamboga au juisi za asili unaimarisha afya na kumpa mtu nguvu na hamu ya kufanya tendo la ndoa. Hata hivyo ieleweke kuwa kuna baadhi ya watu kama vile wasiozalisha vichocheo,tiba yao sio chakula pekee bali ni lazma waende hospitalini kufanyiwa vipimo na kup[atiwa tiba sahihi kulingana na tatizo walilonalo.
  Tahadhari:matumizi holela ya madawa yanaweza kuleta madhara katika figo au kudhoofisha kabisa nguvu ya kufanya tendo la ndoa.

KWA MAONI,USHAURI TUWASILIANE KUPITIA;
MOBL:0776 217417,
fax2email +255736661119.
email;lmtmherbal@rocketmail.com