Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 29 Mei 2015

URINARY TRACT INFECTION(UTI) KWA WANAUME NA WANAWAKE





  Leo tuangalie tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo(UTI)kwa wanawake na wanaume.Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalam huitwa SIMPLE CYSTITIS au BLADDER INFECTION na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa PYLONEPHRITIS au KIDNEY INFECTION.
    Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa ESCHERICHIA COLI.Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa.Lakini watu wengi wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi japokuwa kuna visababishi vingine vichache.Bakteria wa Escherichia Coli hawapo peke yao huambatana na waitwao STAPHYLOCOCCUS,SAPROPHYTI CUS,PSEUDOM ONAS,ENTEROBACTER n.k
Maambukizi katika njia ya mkojo lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo na si pengine popote.Wapo wanawake wamekuwa wakiniulizia kuhusu tatizo la kutokwa na uchafu ukeni na kudhani ni ugonjwa huu,huo ni ugonjwa tofauti kabisa na tunaouchambua leo.
    Tunapozungumzia maambukizi katika njia ya mkojo,tuna maana ni kutoka eneo la nje ya utupu hadi kwenye kibofu na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo kitaalam huitwa LOWER URINARY TRACT INFECTION na ikihusisha eneo la juu ya kibofu jina hubadilika na kuitwa UPPER URINARY TRACT INFECTION.Mara nyingi maambukizi haya kwa wanawake hutokea wakati wa kujisafisha,kutonawa vizuri sehemu za siri na kuvaa nguo za ndani chafu.Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambazo huua bacteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bacteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi.  Upungufu wa homoni ya kike iitwayo OESTROGEN husababisha bakteria wasababishao maambukizi katika njia ya mkojo kuzaliana kirahisi.Matatizo haya ya maambukizi licha ya kuwapata zaidi wanawake huwakumba pia watoto wadogo kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vyao vya uzazi,njia ya mkojo na haja kubwa vipo jirani.
Watoto wa kiume ambao hawajatahiriwa nao hupata maambukizi rahisi kutokana na viungo vyao vya uzazi kuwa vifupi na wanaponawa maji yasiyo salama kwa watoto wa kiume huwa rahisi bakteria kubaki katika ngozi inayoning'inia(govi),hivyo kusababisha tatizo hili.Lakini pia wanaume watu wazima ambao hawajatahiriwa wanaweza kupata maambukizi kutokana na sababu ambazo tumezitaja hapo juu ambapo pia ni rahisi kwao kuambukizwa ukimwi kama watafanya ngono zembe na ndiyo maana tunasisitiza tohara kwa wanaume.
  Maambukizi yanayoshambulia mfumo wa mkojo zaidi ni bakteria wanaoishi katika mfumo wa haja kubwa kusafiri kwa bahati mbaya na kujikita katika mfumo wa mkojo.Bakteria wengine waambukizao njia ya mkojo ni wale watokanao na magonjwa ya zinaa kama kisonono,klamidia na fangasi wanapojamiiana bila kinga.
  -Ili kuepuka kupata maambukizi katika njia ya mkojo mara kwa mara ni vema kutumia kinga yaani kondom na kwa mwanamke kila anapomaliza kufanya ngono akojoe ili kuondoa bakteria walioingia au kukaa katika tundu ya mkojo wakisubiri kuingia.Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu,unywaji wa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na kutokunywa maji ya kutosha huchangia tatizo hili.Uwepo wa mawe katika figo na mirija ya figo hata ndani ya kibofu pia ni mojawapo ya chanzo cha maambukizi haya katika njia ya mkojo.

  DALILI;
  Baadhi ya dalili za mtu kuambukizwa bakteria katika njia ya mkojo kubwa ni maumivu wakati wa kukojoa,mkojo kuwa na rangi ya njano kupindukia na kuwa na harufu kali japokuwa siyo kila mwenye dalili hizo ana maambukizi katika njia ya mkojo au wengine huita URINARY TRACT INFECTION(UTI) wana ugonjwa huu.
  -Dalili nyingine za maambukizi ni maumivu,kutokwa na usaha au majimaji wakati wa kukojoa kabla au baada ya kukojoa kukiambatana na maumivu na kuhisi moto wakati wa kukojoa mkojo.Baadhi ya wanaume wakati mwingine hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo wakati wa kujisaidia haja kubwa.Wengine wenye maambukizi hujikuta wakipata vichomi katika njia ya mkojo au kuhisi kuwashwa sehemu hiyo,kuumwa kiuno au tumbo na kadhalika.Mgonjwa anaweza pia kukumbwa na homa kali mara kwa mara na mwili kuwa mchovu,kwa watoto hupoteza hamu ya kula na mwili kuonyesha kuchoka.
-Wagonjwa wengine hupata maumivu kwenye kibofu cha mkojo ambapo husikia maumivu ya chini ya tumbo usawa wa kitovu na huwa hayaishi,matatizo haya ya mfumo wa mkojo kama tulivyoona huko juu huwapata watu wote wanawake na wanaume.Watu wenye matatizo haya kila wakipima huambiwa wana UTI,kwa wanaume huhisi hata nguvu za kiume hupungua na wanawake hupoteza hamu ya tendo la ndoa.

  WAJAWAZITO;
-Kwa wajawazito ugonjwa huu unaweza kuhatarisha maisha yao na mtoto aliye tumboni,bakteria wanaweza kuingilia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhara mengine kama vile shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi wa kazi mbovu wa figo.

  TIBA;
-Maambukizi katika njia ya mkojo hutibika kwa dawa mbalimbali za kisasa na mbadala baada ya kufanyiwa vipimo na kuwa mgonjwa ana maambukizi hayo.Dawa ambazo anaweza kupewa ni kama vile Ciprofloxacin,Fosfomycin,Monurol,Furadantin,Sulfam ethoxazole,Co-trimax,Ampicillin,Gentamicin n.k lakini usitumie dawa yoyote bila kwanza kupata ushauri wa daktari.
-Katika kituo chetu tunayo dawa iitwayo LMTM-N7/SUZ,LMTM-S32/J na LMTM-RUN/4.5.1 ambazo zinauwezo mkubwa wa kutibu kwa wakati mmoja magonjwa yote ya zinaa(STD)

  USHAURI;
-Tunashauri kwa wanawake waepuke kujisafisha sehemu za siri kwa maji yarukayo kwa kasi,pia waepuke kupaka marashi sehemu hizo,au kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu kwani hizo huua bakteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bakteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi.
-Ujisafishapo baada ya kujisaidia unatakiwa uanzie mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bakteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo.Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi wanaweza kushauriana na daktari jinsi ya kutumia oestrogen ya ukeni ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi.Kwa wanaume maambukizi haya huathiri nguvu za kiume na kuenea hadi katika korodani na kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na kukufanya uwe mgumba.
-Maambukizi ya njia ya mkojo huweza kusababisha matatizo ya tezi ya kiume(prostate) kwani husababisha mrija wa mkojo kuziba ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bakteria kujenga makazi.Hali hiyo ikitokea mgonjwa lazma akamuone daktari ili aweze kuwekewa mrija wa kutolea mkojo.

KWA MASWALI,USHAURI NA TIBA;
MOBL;+255776 217417
fax2email+255 736 601119
email:lmtmherbal@rocketmail.com

Jumatano, 15 Aprili 2015

ZIJUE TIBA ZA MIMEA INAYOTUZUNGUKA



ALOVERA(LITEMBWE)




Alovera ni mmea wenye uwezo wa kutibu magonjwa mengi kama vile;
1.Malaria
2.Kisukari
3.Saratani
4.Mkanda wa jeshi
5.Vidonda tumbo
6.Baridi yabisi
7.Maumivu ya viungo
8.Homa ya matumbo
9.Mwili kuvimba
10.L/B/P
11.Madhara ya ukiumwa na wadudu
12.Bawasiri
13.Kuinua CD 4
14.Nguvu za kiume
15.Kuchelewa hedhi
16.Kurefusha maisha kwa wale wenye VVU
17.Hamu ya kula
18.Husaidia kuyeyusha chakula
19.Mkojo utokao kwa shida
20.Pumu
21.Ini
22.Figo
23.Ngozi na masikio kutoa usaha

Matayarisho ;Hutegemea aina ya ugonjwa unaotaka kuutibu



TANGAWIZI;
 Tangawizi ijapokuwa ni kiungo katika vyakula pia ni dawa yenye uwezo wa kutibu maradhi mbalimbali yanayomsibu binadamu.Baadhi ya maradhi hayo ni;
1.Tumbo-hutuliza maumivu ya tumbo yanayotokana na matatizo ya usagaji wa chakula
               -kuharisha,kuvimbiwa.(Inapotumiwa katika chakula husaidia usagaji wa chakula na inaleta hamu ya kula)
2.Kichefuchefu na kutapika-Huondoa kichefuchefu
3.Matatizo ya moyo-Huimarisha moyo na kumuepusha mtu maradhi ya moyo
4.Matatizo ya kupumua-Inapunguza kiwango cha mafuta mwilini
   -Huondoa homa ya mafua
   -Hutibu pumu
5.Maumivu-Maumivu ya misuli
                  -Maumivu ya kichwa,shinikizo la damu,mawazo,kizunguzungu na kukosa umakini
6.Maumivu wakati wa hedhi
7.Husaidia kutibu malaria na homa ya manjano
8.Nguvu za kiume na kuboresha manii
9.Vijiwe katika figo
10.Hufaa kutunzia nywele kwani huondoa uyabisi
11.Husaidia katika tiba ya saratani na kuzuia saratani
12.Husaidia kwa wenye kufunga hedhi na kusaidia kutoka


  NAZI;
Nazi ina Vitamin A,B na E
Baadhi ya faida za nazi ni;
a.Huimarisha utumbo
b.Upungufu wa damu
c.Husaidia mapafu
d.Huondoa uchovu wa mishipa pamoja na magonjwa ya mishipa
e.Kuondoa uchovu mwilini
f.Huondoa usahaulifu
g.Huimarisha viungo
h.Homa

MATUMIZI;Jinsi ya kutumia wasiliana na LMTM HERBAL CENTER
MOBL;+255776 217417
fax2email+255736601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com

JE WAJUA KABICHI NI DAWA?




Kabichi ni zao  linalolimwa mahala pengi sana hapa duniani.Mara nyingi mboga hii imekuwa ikichukuliwa kama ni aina fulani inayotakiwa kuliwa na watu wa chini au kutumika katika kachumbari tu.Huwa inatumika zaidi sehemu za jumuiya kama vile shule,magerezani na vyuoni kwani gharama yake ni ndogo hivyo mnunuzi anaweza kuhimili kuinunua kwa matumizi ya watu wengi.Mboga hii ina manufaa mengi sana mwilini lakini iwe ya rangi ya kijani,nyekundu au hata zambarau na sio ile iliyokaa sana sokoni hadi kusinyaa,hiyo haina manufaa kabisa kwa mwili wa binadamu.

FAIDA ZA KABICHI;
1.Huzuia saratani-Ulaji wa kabichi huzuia saratani ya matiti,utumbo mpana na saratani ya korodani(testes)kwa wanaume.Kwani ina madini yanayosaidia kupigana na visababishi vya saratani.Pia huzuia uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.
Mboga hii huondoa lehemu (cholesterol)katika damu,kwani huleta shinikizo kubwa la damu pale yanapojaa,pia huweza kusababisha kiharusi na moyo kupasuka.Hivyo kabichi husaidia kuondoa.
2.Kuondoa sumu mwilini-Kabichi ina Vitamin C kwa wingi kuliko hata machungwa,pia ina kampaundi za sifa,vitu hivi huisaidia sana kusafisha damu na kuondoa sumu mwilini.Pia huimarisha ini hivyo kulifanya lifanye kazi vizuri.
3.Ina Vitamin kwa wingi-Kabichi ina Vitamin A,B,C,E na K kwa wingi ambazo zina faida kubwa sana mwilini kama;
a.Vitamin A huisaidia kuimarisha ngozi na uwezo wa kuona.
b.Vitamin B huimarisha uwezo wa kutafakari na kuboresha utendaji wa kazi wa ubongo na kuzuia msongo wa mawazo.
c.Vitamin C huimarisha kinga ya mwili na kuzuia visababishi vya saratani
d.Vitamin E hufanya ngozi ya mwili kuwa nyororo
e.Vitamin K huimarisha mifupa na uhusika na ugandaji wa damu pale unapoumia.
Manufaa mengine ni kama vile kulinda mwili na maambukizi ya magonjwa mbalimbali,pia hutibu vidonda vya tumbo,kwani utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha tiba cha Stanford,iligundulika kuwa wagonjwa 13 walipona vidonda vya tumbo kwa kunywa juisi ya kabichi.Pia hupunguza tatizo la kufunga choo kwani ina kambakamba zinazosaidia kulainisha choo na vilevile ina madini ya salfa na chuma yanayosaidia kusafisha utumbo.
    JINSI YA KUANDAA KABICHI;
 Kabichi inapendekezwa sana kuliwa ikiwa mbichi kwa kuongezwa ndimu na chumvi ili kuleta ladha nzuri kama vile kachumbari,vilevile unaweza tu ukaichemsha supu yake lakini isiive sana kiasi cha kuua virutubisho vyake,inapendekezwakuchemka kwa dakika 4-5 tu.
  ANGALIZO;Ulaji wa kabichi uliopitiliza huweza kusababisha ugonjwa wa Rovu(goiter)kwa hiyo watu wenye tatizo la rovu wasile kabichi kwa wingi.

KWA MAWASILIANO NA MAELEKEZO ZAIDI YA JINSI YA KUTUMIA KULINGANA NA TATIZO UTAKALOKUWA NALO WASILIANA NA OFISI ZETU KUPITIA;
MOBL;+255776217417,
fax2email+255736601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com

Jumatatu, 12 Januari 2015

PROSTATITIS(TATIZO LA KIBOFU CHA MKOJO)





Tatizo hili watu wengi hulifahamu kama kibofu cha mkojo.PROSTATE-Ni kikokwa kidogo kilichopo chini ya kibofu cha mkojo.Kazi ya prostate ni kutoa majimaji kama maziwa ambayo kazi yake kubwa ni kubeba na kusafirisha mbegu za kiume kupitia njia ya mkojo(urethra)na kwenda kunakohitajika.
Jinsi umri wa mwanaume unavyosonga mbele PROSTATE huongezeka ukubwa(kuvimba).Hali hii husababishwa aidha na upungufu wa LYCOPENE(ambayo hupatikana kwa wingi kwenye nyanya)au maambukizi (infection)au sababu nyinginezo kama maambukizi ya vijidudu (FUNGI).Kuvimba kwa prostate husababisha kugandamiza kwa kibofu cha mkojo kiasi kwamba mkojo kidogo ukiwa ndani ya kibofu mtu hudhani kibofu kimejaa kumbe sio.
DALILI ZA MTU MWENYE PROSTATE NI;
1.Kubanwa na mkojo mara kwa mara
2.Kwenda haja ndogo mara kwa mara usiku
3.Damu kwenye mkojo au kwenye mbegu za kiume
4.Maumivu wakati wa kukojoa
5.Maumivu baada ya kukojoa au wakati mtu anamaliza kukojoa
6.Kushindwa kukojoa
7Maumivu wakati mbegu za kiume zinatoka
8.Maumivu kwenye hipsi,mgongo,nyonga au mapajani
9.Matone ya mkojo kutoka yenyewe au kushindwa kujizuia na kukuta mkojo umetoka
-Mtu mwenye tatizo hili anaweza kujihisi kama amepungukiwa nguvu za kiume(sprerm count)kitu ambacho kwa kiasi kikubwa sio kweli.Hali hii husababishwa na ile hali ya yale majimaji yanayosafirisha mbegu za kiume kutokuwepo kwa kuishia njiani.Hali ikizidi kuwa mbaya huweza kusababisha muathirika kufanyiwa upasuaji kwaajili ya kuondoa prostate hiyo au kusababisha mtu kupata saratani(PROSTATE CANCER)
USHAURI;Wanaume wanashauriwa kuwa na mazoea ya kula nyanya kwa wingi(iliwe bila kupikwa au kuongezewa kitu chochote kama chumvi),papai,zabibu na mapera kama kinga.ukiweza kula nyanya kwa wingi kila siku itakuwa ni vizuri zaidi.
 Hata hivyo habari nzuri ni kuwa katika kituo chetu cha LMTM HERBAL CENTRE tunazo dawa ya LMTM-RUN/4.5.1 na LMTM/S32/J zenye uwezo mkubwa wa kutibu tatizo hili likiwa bado katika hatua za awali.

KWA MASWALI,USHAURI NA TIBA;
MOBL;+255798353434
fax2email+255736601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com