Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 15 Aprili 2015

JE WAJUA KABICHI NI DAWA?




Kabichi ni zao  linalolimwa mahala pengi sana hapa duniani.Mara nyingi mboga hii imekuwa ikichukuliwa kama ni aina fulani inayotakiwa kuliwa na watu wa chini au kutumika katika kachumbari tu.Huwa inatumika zaidi sehemu za jumuiya kama vile shule,magerezani na vyuoni kwani gharama yake ni ndogo hivyo mnunuzi anaweza kuhimili kuinunua kwa matumizi ya watu wengi.Mboga hii ina manufaa mengi sana mwilini lakini iwe ya rangi ya kijani,nyekundu au hata zambarau na sio ile iliyokaa sana sokoni hadi kusinyaa,hiyo haina manufaa kabisa kwa mwili wa binadamu.

FAIDA ZA KABICHI;
1.Huzuia saratani-Ulaji wa kabichi huzuia saratani ya matiti,utumbo mpana na saratani ya korodani(testes)kwa wanaume.Kwani ina madini yanayosaidia kupigana na visababishi vya saratani.Pia huzuia uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.
Mboga hii huondoa lehemu (cholesterol)katika damu,kwani huleta shinikizo kubwa la damu pale yanapojaa,pia huweza kusababisha kiharusi na moyo kupasuka.Hivyo kabichi husaidia kuondoa.
2.Kuondoa sumu mwilini-Kabichi ina Vitamin C kwa wingi kuliko hata machungwa,pia ina kampaundi za sifa,vitu hivi huisaidia sana kusafisha damu na kuondoa sumu mwilini.Pia huimarisha ini hivyo kulifanya lifanye kazi vizuri.
3.Ina Vitamin kwa wingi-Kabichi ina Vitamin A,B,C,E na K kwa wingi ambazo zina faida kubwa sana mwilini kama;
a.Vitamin A huisaidia kuimarisha ngozi na uwezo wa kuona.
b.Vitamin B huimarisha uwezo wa kutafakari na kuboresha utendaji wa kazi wa ubongo na kuzuia msongo wa mawazo.
c.Vitamin C huimarisha kinga ya mwili na kuzuia visababishi vya saratani
d.Vitamin E hufanya ngozi ya mwili kuwa nyororo
e.Vitamin K huimarisha mifupa na uhusika na ugandaji wa damu pale unapoumia.
Manufaa mengine ni kama vile kulinda mwili na maambukizi ya magonjwa mbalimbali,pia hutibu vidonda vya tumbo,kwani utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha tiba cha Stanford,iligundulika kuwa wagonjwa 13 walipona vidonda vya tumbo kwa kunywa juisi ya kabichi.Pia hupunguza tatizo la kufunga choo kwani ina kambakamba zinazosaidia kulainisha choo na vilevile ina madini ya salfa na chuma yanayosaidia kusafisha utumbo.
    JINSI YA KUANDAA KABICHI;
 Kabichi inapendekezwa sana kuliwa ikiwa mbichi kwa kuongezwa ndimu na chumvi ili kuleta ladha nzuri kama vile kachumbari,vilevile unaweza tu ukaichemsha supu yake lakini isiive sana kiasi cha kuua virutubisho vyake,inapendekezwakuchemka kwa dakika 4-5 tu.
  ANGALIZO;Ulaji wa kabichi uliopitiliza huweza kusababisha ugonjwa wa Rovu(goiter)kwa hiyo watu wenye tatizo la rovu wasile kabichi kwa wingi.

KWA MAWASILIANO NA MAELEKEZO ZAIDI YA JINSI YA KUTUMIA KULINGANA NA TATIZO UTAKALOKUWA NALO WASILIANA NA OFISI ZETU KUPITIA;
MOBL;+255776217417,
fax2email+255736601119
email;lmtmherbal@rocketmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni