Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 11 Agosti 2013

WANACHOSEMA WATAFITI KUHUSU ASALI KWA AJILI YA TIBA



Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote.Vitabu vingi vya zamani vinazungumzia namna watu walivyokuwa wakitibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali.Moja ya vitabu vya zamani ni pamoja na kuruani Tukufu ambayo Mwenyezi Mungu anaitaja asali kama tiba(an-nahi 16:68-69).Sasa hivi kuna makala za kisayansi zaidi ya 1500 zilizoandikwa zikielezea kuhusu uwezo wa asali katika kutibu magonjwa mbalimbali.Wafaransa na warusi ni watu wanaofahamika kufanya utafiti mkubwa katika maabara kuhusu uwezo wa asali katika kutibu magonjwa mbalimbali.
Asali inasadikika kuwa na vitu 18 au zaidi ambavyo ni muhimu katika kutibu mwili, na wanasayansi wanaendelea kugundua vitu vingine kila siku.Moja ya vitu hivyo ni Meltin ambayo ni kitu kinacholeta kinga(prevalent substance)katika kutibu maumivu (mara 100 zaidi ya madawa haya ya kemikali na yenye hydrocortisol).Pia ndani ya asali kuna Adopin ambayo pia ni muhimu katika kutibu maumivu.Katika asali kuna apamin,compound X,hyaluronidase,phospholiase AZ,histamine(inayotibu alleg)na kitu kiitwacho Mast Cell Degranulating Protein(MSSDR).Baadhi ya vitabu vinavyofahamika kuandikwa na watafiti kuhusu uwezo wa asali kutibu ni pamoja na kile cha Bees Don't Get Arthritis kilichoandikwa na Fred Malone na Bee Balance cha Amber Rose.Mtafiti mmoja anayataja maeneo matatu abayo asali inayatibu kirahisi kuliko tiba zingine kwa kunywa na kupaka.
Moja,anasema ni maumivu ya viungo na uvimbe.Anasema asali husaidia kutibu magonjwa ya rheumetoil na osteoarthritis kwa kuondoa maumivu na uvimbe.Magonjwa mengine ya minofu na misuli kama scleroderma yametibika kirahisi kwa asali.Pia mtafiti anasema matatizo mengine yasiyohusiana na viungo(joints)au misuli ,kama vile ukerative colits na hata athma,vinatibiwa kwa asali.Hili linawezekana kwa sababu ya uwezo wa asali wa kuchochea endegenous cortisol/kutokana na hypothalamus-pituitary-ardenal axis.
Mbili,mtafiti anasema ni uwezo wa asali kutibu majeraha yasiyopona muda mrefu (chronic injuries).Kwa kifupi majeraha,yakiwemo ya kuungua (bursits and tendonitis)yameonekana kutibiwa vizuri kwa asali kuliko dawa hizi zenye kemikali.Maumivu ya mgongo na shingo au maeneo mengine pia watu wanashauriwa kuyatibu kwa asali kabla ya kukimbilia madawa mengine.
Tatu,mapele na makovu (keloids and scartessine)yanatibiwa haraka kwa asali.Makovu hupotea na hata rangi huweza kupotea pia.Makovu ndani ya mwili kama vile kovu linalotokana na operesheni linaweza pia kupata ahueni kwa kutibu eneo la jeraha.
Mtafiti huyu anasema kwamba jinsi ya magonjwa kupaka asali katika eneo lenye matatizo inategemeana na ukubwa wa tatizo.Kama ni dogo yaweza kuwa mara mbili kwa siku au zaidi hadi mgonjwa anapopata nafuu.Kuna baadhi ya watu hupata mzio(allegy) kwa asali na hawa hushauriwa kuwa yellow jackets au wasps.Utafiti uliofanywa mwaka 1998 nchini India,ulionyesha mafanikio makubwa kuhusu kutibu vidonda,hasa vilivyotokana na kuungua.Katika utafiti huo asali mbichi ilionekana kufanya kazi hata zaidi ya dawa kama silver sulfadiazine.Watafiti wanasema kuwa majeraha yaliyokuwa yakitibiwa kwa asali yalipata ahueni haraka.Pia iligundulika kwamba jeraha linalotibiwa kwa asali halisababishi kuambukiza na maumivu huwa kidogo kwa mgonjwa.
Ukaja utafiti wa mwaka 1999 uliofanyika Yemen.Huu pia ulionyesha kuwa asali mbichi isiyochanganywa na maji ama sukari guru 'inatisha' katika kutibu majeraha yatokanayo na operesheni.Utafiti ulionyesha kuwa vidonda vya kawaida na hususa ni vya operesheni vya watu waliokuwa wakifungwa(dressing) kwa asali walipona haraka kulinganisha na wale waliotumia dawa za hospitali(standard antiseptic therapy).Watu wenye vidonda vya mshono waliotibiwa kwa asali,walipona kabisa kabisa kwa siku 11 tu wakati wale waliotibiwa kwa dawa hizi za hospitalini(antiseptics)iliwachukuwa zaidi ya siku 20.Miaka kadhaa iliyopita utafiti mwingine ulifanyika Israel nao ukaonyesha kwamba asali ni kiboko pia katika kutibu majeraha yaliyo wazi.Utafiti huoulifanywa kwa watoto ambao iligundulika kwamba watoto ambao vidonda vyaovilishindwa kupona baada ya kutibiwa kwa viuavijasumu(antibiotics)hadi kuhisiwa kwamba wana vidonda ndugu,ilichukua siku 21 tu vidonda hivyo kupona na kufunga kabisa.
Pia mwezi april mwaka 2000 gazeti la Nursing Times liliandika kwamba asali pia ilikuwa inatibu kwa haraka vidonda vitokanavyo na bakteria wanaoshambulia damu (serious bacteria blood/infection).Mgonjwa  mmoja mvulana mwenye umri wa miaka 15 alikuwa na madonda kadhaa kwenye miguu yake ambayo yalikuwa yamegoma kupona licha ya kutibiwa kwa umakini wote(intesive therapy)zaidi ya miezi tisa hospitalini kwa tiba ya kawaida(standard dressings).Baada ya kuamua kutibiwa kwa asali mbichi madonda yake yalianza kuonyesha mafanikio na baada ya wiki 10 tu akapona kabisa.Kutokana na utafiti huu,watafiti na bodi ya usajili wa madawa ya Australia ilipitisha matumizi ya dawa itokanayo na asali ya ''Medihoney'' kwa ajili ya matumizi ya nyumba kwenye vidonda na magonjwa ya kuambukiza.
Dawa hii inatokana na asali mbichi(crude unprocessed honey)inayopatikana kwenye misitu ya New Zealand.Kuhusu namna asali inavyotibu haraka vidonda ,imegundulika kwamba ina uwezo wa kuweka mpaka mkali ambao huzuia kidonda kutoshambuliwa tena na bakteria.Vilevile asali huweka mazingira ya unyevu kwenye kidonda ,hali inayowezesha chembe za ngozi kukua juu ya kidonda bila kusababisha makovu .Vilevile asali inasaidia kukua kwa minofu chini ya tabaka la ngozi.Pia ndani ya asali kuna kitu kinaitwa anti-inflammatory effect,ambacho kinapunguza maumivu kwa mgonjwa(tofauti na tiba zingine).Vilevile asali ina kitu ambacho kinasaidia kupambana na bakteria wanaoleta magonjwa kwa kuwa na kitu kinachoitwa hydrogen peroxide.Hii ni kwa mujibu wa Peter Molan,profesa mshiriki wa bailojia katika chuo kikuu cha Waikato,New Zealand na mtu ambaye ni mtaalamu wa tiba ya asali kwa vidonda.Lakini inasisitizwa kwamba asali ambayo ni nzuri kwa kutibu vidonda ni mbichi na si hizi zinazochemshwa ama kupitia viwandani na kuuzwa kwenye super markets.

KWA MAONI,MASWALI NA USHAURI TUWASILIANE KUPITIA;
fax2email+255736601119
email:lmtmherbal@rocketmail.com
NB:KWA WALE WANAOPENDA KUWASILIANA KWA SMS,FUNGUA SEHEMU YA UJUMBE MFUPI KATIKA SIMU YAKO KISHA ANDIKA NENO LMTM ACHA NAFASI,ANDIKA SWALI LAKO NA KISHA UTUME KWENDA NAMBA 15522 NA SWALI LAKO LITAJIBIWA.PIA USISAHAU KULIKE PAGE YETU NA KUTUANDIKIA KUPITIA www.facebook.com/lmtmherbalcentre
                                 USISUMBUKE LMTM IPO KWA AJILI YAKO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni