Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 15 Aprili 2016

TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA JINSI YA KUKABILIANA NALO

 




Waathirika hawa wamekuwa wakipoteza fedha nyingi na mara nyingine hujikuta wakiingia katika matatizo makubwa ya kiuchumi baada ya kukutana na vipeperushi au matangazo ya dawa za kuongeza nguvu za kiume .
Wengi hujikuta wakitapeliwa na waganga feki ambao wamejaa mjini na vijijini.Katika mitaa utaona mabango mengi ya waganga wa kienyeji wasio na sifa wala usajili wakijitangaza kuwa na dawa za kuongeza nguvu za kiume.
  Mara nyingi dawa hizo siyo za kutatua tatizo bali ni kutafuta nguvu za muda.Kukurupuka na kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume kiholela ni hatari kwani nyingi ndio chanzo cha kuumiza mwili na kuathiri viungo kama figo.
  Tendo la uume kuwa na nguvu na kuweza kusimama kina mtiririko wa matukio mengi ya kimwili na huwa ni hatua moja kwenda nyingine.Kitendo cha kusimama kinahusisha mfumo wa fahamu kama ubongo,uti wa mgongo na mishipa ya fahamu,mfumo wa damu ambao ni moyo,damu na mishipa na mfumo wa tezi zinazomwaga vichocheo kama homoni.
  Zipo kemikali nyingi za kibaiolojia za mwilini zikiwamo protini,virutubisho na vitamini mbalimbali tunavyopata katika lishe ,husaidia pia katika tendo hili.
Kwa kawaida sehemu za uzazi wa kiume huwa na misuli laini kama sponji ambayo huwa na mishipa midogo mingi ambayo imejikunja kunja kama mizizi ya mmea.
   Wakati wa kusimama damu iliyosafi humiminika kupitia mishipa ya ateri ambayo hutanuka kuruhusu damu ya kutosha kupita kwenda katika misuli laini kama sponji ambayo huwa imetulia kuruhusu damu kuingia katika mishipa hiyo.Wakati huohuo ile mishipa inayotoa damu chafu kurudi kusafishwa yaani  vein ,huwa zimebanwa ili damu hiyo isitoke katika misuli laini ya uume.
  Mchepuko wa kupata hisia za kujamiiana  ni kituo kilichopo ndani ya uti wa mgongo ,ni matokeo ya eneo la uzazi sehemu ya kiume kusisimuliwa.
Baadhi ya mambo yanayosababisha mtu kukosa nguvu za kiume ni magonjwa kama vile;
-Kisukari
-Maradhi ya mishipa ya damu
-Shinikizo la damu

-Uwapo wa maradhi ya kisukari kisichodhibitiwa kwa muda mrefu huweza kusababisha mishipa inayopeleka damu katika uume kuharibika.Sukari iliyo juu huiharibu mishipa hii ya damu na kuifanya iwe migumu.

-Shinikizo la damu likiwa kali mara kwa mara huweza kuleta uharibifu katika mishipa ya damu ambayo ni midogo iliyotanda kwa wingi katika uume.

  Mambo mengine ni;
-Utumiaji wa tumbaku,
-Uvutaji sigara,
-Ulevi uliopindukia,
-Utumiaji wa madawa ya kulevya.
 Vitu hivyo pia huweza kuharibu mishipa ya damu katika uume.

   Mambo mengine ni magonjwa ya tezi ya koo inayotoa homoni za ukuaji mwili na kutengeneza kidogo kwa homoni muhimu ya kiume ambayo ni Testosterone.
Maradhi mengine ni ugonjwa wa kutetemeka ,unene na uzito kupita kiasi,ugonjwa wa akili na matibabu ya muda mrefu ya saratani ya tezi dume.
   Tatizo la nguvu za kiume linaweza kutibiwa kwa matibabu mbalimbali baada ya kufanyiwa uchunguzi yakinifu.
Baada ya uchunguzi daktari anaweza kukupatia dawa au kukupa maagizo kama vile kufanya mazoezi ,kula vyakula fulanina kubadili mitindo kadhaa ya kimaisha.Kama tatizo litakuwa linasababishwa na magonjwa mengine dqaktari anaweza akaanza kutibu magonjwa hayo na afya yako kurejea upya vizuri.

 Hatahivyo kwa wale ambao hawana matatizo mengine yoyote ila nguvu zao zimepungua LMTM HERBAL CENTRE tunazo dawa aina mbalimbali za mimea zenye uwezo wa kutatua nguvu za kiume kwa kiwango cha juu.
Moja ya madawa hayo ni LMTM/fg/olv.


KWA MAWASILIANO ZAIDI;
lmtmherbal@rocketmail.com
mobl:0798353434

Maoni 2 :

  1. Cela fait un moment que je suis sur des sites de blogs et aujourd’hui, j’ai le sentiment que je devrais partager mon histoire, car j’étais aussi une victime. J'avais le VIH pendant 6 ans et je n'avais jamais pensé obtenir un traitement, ce qui m'a empêché de me marier avec l'homme avec lequel je devais me marier, même après deux ans de relation, il a rompu avec moi quand il découvre que j'étais séropositif. J'ai donc entendu parler du Dr Itua sur le site de blog qui traitait une personne et cette personne a raconté comment elle avait guéri et laissé ses coordonnées, j'ai contacté le Dr Itua. Il l'a confirmé et j'ai décidé d'essayer. aussi et utiliser ses médicaments à base de plantes, c’est ainsi que mon fardeau a complètement cessé Mon fils aura 2 ans bientôt et je suis reconnaissant envers Dieu et reconnaissant envers son médicament aussi. Itua peut aussi bien guérir la maladie suivante… Cancer, VIH, herpès, hépatite B, inflammation inflammatoire du foie, diabète, fibromes, retrouvez votre dos, Si vous l'avez (A juste le joindre à drituaherbalcenter@gmail.com ou le numéro Whatsapp. + 2348149277967), il peut également vous conseiller sur la façon de gérer certains problèmes liés aux relations conjugales. C'est un homme bon.

    JibuFuta
  2. Yeah hio Kali sana aafu haina madhara yoyote

    JibuFuta